Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI.
1. Mpatie mtoto dawa zilizoagizwa na daktari
Baada ya kugundua kuwa mtoto ana UTI dawa zilizoagizwa zinapaswa kutumika na kuendelea kuangalia maendeleo ya mtoto, dawa hizo zitumike kwa uhakika na kwa mda wake mtoto anapopaswa kupewa dawa hizo, kwa hiyo ni lazima kuangalia na matokea hasi ya dawa na mtoto anaweza kubadikishiwa dawa ambayo inapatana na mwili wake na kuendelea na matibabu yake ya kawaida.
2.Elimu inabidi utolewa kwa mama na walezi wa mtoto namna ya kuepukana na Maambukizi ya UTI kwa kufanya yafuatayo, kutawadha kutoka mbele kwenda nyuma, kumsafisha mtoto vizuri baada ya kujisaidia, kumtahiri mtoto kaama ni wa kiume, kumbadilisha mtoto nepi pindi tu anapijisaidia na anapokojoa ,kwa hiyo mtoto hasikae na nepi kwa mda mrefu maana bakteria kutoka kwenye mkojo urudi kwenye kibofu Cha mkojo na kukua na kuongezeka hatimaye usababisha maambukizi mapya.
3.Mtoto akiwa na UTI na Yuko kwenye matibabu hakikisha anapewa chakula Cha kutosha chenye mlo kamili na pia kama anatapika hakikisha unatibu kutapika Ili mtoto aweze kula chakula na chakula niendelee kukaa mwilini na kufanya kazi pamoja na dawa na hakikisha mtoto ananyonya vizuri Ili kuhakikisha kuwa dawa zinafanya kazi vizuri, na maendeleo ya mtoto yanakuwa Kawaida.
4. Hakikisha joto la mwili, msukumo wa damu, mapigo ya moyo na upumuaji wa mtoto vinakuwa sawia kwa kupima mara kwa mara kwa sababu maambukizi yoyote kwenye mwili usababisha hali y mwili kubadilika na kuleta kitu kingine ambacho ni matokeo ya maambukizi. Mfano joto la mwili likipanda kwa sababu ya ya UTI mtoto anaweza kuwa na degedege kwa hiyo tunapaswa kuhakikisha kuwa kila hali kwenye mwili Iko sawa kama haiko sawa tujitahidi kuiweka sawa Ili kuepusha madhara mbalimbali yanayoweza kutokea kwa sababu ya maambukizi.
5. Kama mtoto amepata changamoto ya UTI anapaswa kuwa na maji ya kutosha mwilini maana maambukizi kwa mtoto upunguza kiwango Cha maji mwilini na mtoto anaweza kuelekea pabaya, kwa hiyo kwanza mama na waangalizi wa mtoto wanapaswa kuangalia kiasi Cha maji mwilini kwa kuangalia kiasi Cha maji kinachoingia na kinachotoka kwa kufanya yafuatayo.
_ kuangalia kiasi kinachoingia kwa kuangalia anakunywa maji kiasi gani, uji , maziwa,juice na vitu vyote vinavyopungia mwilini kwa mfumo wa maji.
- kuangalia kiasi Cha maji yaliyotoka kwa kuangalia jinsi alivyokojoa yaani amekojoa kiasi gani,au kama anatoa jasho ,au labda anaharisha au kutapika.
Kama kiasi kinachoingia ni kikubwa zaidi ya kinachotoka mtoto anaweza kuendelea na dawa na uangalizi Ila kama kinachotoka ni kikubwa ya kinachoingia mtoto aongezwmewe maji.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la kichwa , Kiharusi, Tumor ya ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi, kama vile Kisukari au maambukizi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za Dengue,ni Dalili ambazo huwa kwenye makundi matatu na kuwepo kwa makundi hayautegemea kuongezeka kwa tatizo kwa sababu tatizo likiongezeka bila kutibiwa na dalili uongezeka na kufikia kwenye sehemu isiyo ya kawaida kwa mg
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa kisukari unaopelekea kukosa fahamu ni tatizo linalohatarisha maisha kisukari ambalo husababisha kupoteza fahamu. Ikiwa una kisukari, sukari ya juu ya damu (hyperglycemia) au sukari iliyopungua sana (hypoglyc
Soma Zaidi...Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maradhi ya macho,dalili na matibabu yake
Soma Zaidi...Je na wewe unasumbukiwa na kunggoka jwa kucha. Tatizo limekunaza una muda gani nalo?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi visababishi vya maambukizi kwenye milija na, ni mambo yanayosababisha maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi ambayo kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili inashuka.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za mtu aliyegongwa na nyoka, nyoka ni kiumbe ambacho Kina sumu kali na sumu ikiingia mwilini mtu huwa na dalili mbalimbali
Soma Zaidi...