Navigation Menu



image

Ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

Ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.

1. Dondakoo ni ugonjwa unaosababishwa na sumu ya bakteria ambaye kwa kitaalamu huitwa corynebacterium diphtheria, bakteria huyu ushambulia sehemu za pua, koo na wakati mwingine maumivu kwenye masikio hali hii upelekea mgonjwa kushindwa kupumua na wakati mwingine kushindwa kumeza, kwa sababu ugonjwa huu usababishwa na bakteria kuna dawa mbalimbali za antibiotics zinaweza kuponya ugonjwa huu, antibiotics hizo ni kama vile penicillin au erythromycin.

 

2. Ugonjwa huu ushambulia hasa watoto na unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwingine kwa njia zifuatazo kama vile  mtu akipiga chagua yale maji maji yakimgusa mtu mwingine hasa kinywani mtu huyo anaweza akapata, kwa hiyo wakati wa kupiga chafya tunapaswa kuwa makini au tunapopiga chafya tunapaswa kupigia kwenye vitambaa ili kuepuka kusambaza ugonjwa kutoka sehemu moja kwenda kwa mwingine, au kama mama au mlezi wa watoto wadogo wanapaswa kuwa makini sana wasije kuambukiza watoto.

 

3. Ugonjwa huu pia unaweza kusambaa kwa njia ya kutumia vitu vyenye bakteria kama vile kunywea maji kwenye kikombe au glass ya mtu mwenye Maambukizi, au kutumia kijiko bila kuosha kutoka kwa mtu mwenye Maambukizi kwa hiyo bakteria usambaa kutoka kwa mwenye Maambukizi kwenda kwa hasiye na Maambukizi, kwa hiyo kila mtu anapaswa kutumia vifaa vyake hasa hasa vile vinavyoongozwa moja kwa moja kinywani au ni vizuri kuosha vyombo kwa maji moto ili kuweza kuua wadudu wanaosambaza na Kuleta madhara.

 

4. Pia hawa wadudu wanaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwingine kwa kutumia vitu kwa pamoja kama vile taulo na nguo zenye jasho kutoka kwa mtu mwenye Maambukizi na vile vile watu wanaokula peni, penseli na vfutio ambavyo vimetumbukizwa kinywani na mtu mwenye maambukizi na ambaye hana Maambukizi naye akija kutumia na kuweka mdomoni anaweza kupata, kwa hiyo kila mtu anapaswa kutumia vifaa vyake hasa kwa watoto ambao wako chekechekea wanapaswa kuangaliwa kwa makini ili kuepuka kuongeza kwa Maambukizi.

 

5. Kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua kuwa ugonjwa huu upo kwenye jamii na usipotibiwa mapema unaweza kuleta madhara makubwa kwa hiyo tunapaswa kuwapeleka watoto  watoto wapewe chanjo mapema ili kuweza kuepuka madhara  mbalimbali ambayo yanaweza kutokea pia jamii inapaswa kujua Dalili zote za ugonjwa huu ili kuweza kuwahi mapema kwenda hospitalini na pia watu wajifunze kujua jinsi ugonjwa huu unavyoenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 963


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Ishara na dalilili za Mtoto mwenye kuhara
postii hii inazungumzia dalilili za Mtoto mwenye Kuhara. Kuhara maana yake ni kutokwa na kinyesi chenye maji matatu au zaidi, pamoja na au bila damu ndani ya masaa 24. Kuhara kunaweza kusababishwa na maambukizo ya bakteria na virusi, ugonjwa wa matumb Soma Zaidi...

Aina za kisukari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za kisukari Soma Zaidi...

Samaani nilikuwa nauriza ninasumburiwa na fanga ya mdomoni naomba ushauri
Fangasi mdomoni wanaweza kuwa tatizo endapo hawatatibiwa mapema. Wanaweza kuongeza majeraha kwenye kinywa. Soma Zaidi...

Watu walio hatarini kupata UTI
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya makunfi ya watu walio hatarini kupata UTI Soma Zaidi...

Dalili za mtu aliyekula chakula chenye sumu
Post hii inahusu zaidi mtu aliyekula chakula chenye sumu, chakula chenye sumu ni chakula ambacho kikitumiwa na mtu yeyote kinaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu hata kifo. Soma Zaidi...

UGONJWA WA HOMA YA VIRUSI VYA ZIKA (ZIKV) VINAVYO SABABISHWA NA KUNG'ATWA NA MBU
Mnamo mwaka 2016 World Health Organization (WHO) iliitisha kikao cha dharura mnamo mwezi tarehe 1 mwezi wa pili mpaka tarehe 13 mwezi wa nne. Soma Zaidi...

KISUKARI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dalili na sababu za mawe kwenye in yaani liver stone au intrahepatic stones
Katika post hii utakwend akujifunza kuhusu tatizo la kuwa na vijiwe kwenye ini vijiwe hivi hufahamika kama intrahepatic stones. Soma Zaidi...

Huduma kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa
Posti hii inahusu zaidi msaada kwa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa, ni huduma anayopewa mtoto mwenye Maambukizi kwenye mifupa. Soma Zaidi...

Dalili za malaria
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu kwa kitaalamu anaitwa Anopheles.na anasambazwa na mbu jike pale anapotafuta chakula hasa wakati akiwa na mimba. Mbu hawa hupenda kuishi kwenye mnyasi, madibwi haswa kwenye maji yaliyo simama. Soma Zaidi...

Dalili za jeraha kali kwenye ubongo
Posti hii inahusu zaidi dalili za jeraha kali kwenye ubongo, ni majeraha ambayo utokea kwenye ubongo pale ambapo mtu anapata ajali au amepigwa na kitu chochote kigumu kichwni, zifuatazo ni dalili za jeraha kali kwenye ubongo Soma Zaidi...

Madhara ya minyoo
Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa madhara ya minyoo kwenye mwili wa binadamu. Yafuatayo Ni madhara ya minyoo; Soma Zaidi...