Posti hii inahusu zaidi dalili za jeraha kali kwenye ubongo, ni majeraha ambayo utokea kwenye ubongo pale ambapo mtu anapata ajali au amepigwa na kitu chochote kigumu kichwni, zifuatazo ni dalili za jeraha kali kwenye ubongo
1. Maumivu makali ya kichwa utokea ambayo ni tofauti na ya jeraha la kawaida, maumivu hayo uweza kudumu zaidi ya maasaa ishilini na manne ingawa bado mgonjwa anakuwa abatumia madawa ya kupunguza maumivu, mabadiliko katika kuona pengine mgonjwa uona kwa shida kubwa na hata kushindwa kufungua macho, na pengine mgonjwa anashindwa kabisa kusimama hali hii usababishwa na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa nevu unaoelekea kwenye ubongo.
2.Kubadilika kwa mapigo ya moyo.
Kwa sababu ya neva za kwenye ubongo zinakuwa hazifanyi kazi vizuri Kuna mabadiliko yanaweza kutokea kwa mgonjwa ambayo yanahusiana na mapigo ya moyo, pengine mapigo ya moyo uenda mbio sana, pengine uenda taratibu sana kwa hiyo mapigo hayo yanakuwa hayopo kwenye mfumo mmoja wa kwenye mbio au taratibu Bali uchanganya mgonjwa wa namna hii anapaswa kumpelekwa hospitalin mara Moja kwa huduma zaidi.
3.Vile vile na upumuaji wa mgonjwa ubadilika.
Upumuaji ubadilika kwa Sababu mgonjwa upumua haraka haraka na kwa mda fulani mgonjwa upumua pole pole au pumzi huwa fupi na pengine huwa ndefu ,kama una mgonjwa wako na amepata hali ya namna hii unapaswa kumpeleka hospitalini mara Moja Ili kuweza kupatiwa matibabu zaidi, hali hii usababishwa na mshutuko kwenye ubongo ambao ufanya na mifumo mingine mwilini kubadilika kwa hiyo mgonjwa huyu asibakizwae nyumbani.
4.Damu au maji maji yasiyo na rangi kutoka masikioni au puani.
Hali hii utokea hasa kwa wagonjwa wenye majeraha makali kwenye ubongo kwa Sababu Kuna sehemu ambazo zinakuwa zimearibika kwa ndani ambazo upelekea kutoa maji ambayo utokeazea kupitia kwenye masikio au pengine kwenye pua, kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hii tutambue kuwa jeraha kwenye ubongo ni kali na mgonjwa anapaswa kupata matibabu ya haraka.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Tonsillitis kwa kiswahili hujulikana kama mafundomafundo ambayo hutokea pande mbili karibu na Koo na huwa na uvimbe na zikikaa kwa muda bila matibabu hutoa usaha.Dalili na dalili za ugonjwa wa tonsillitis ni pamoja na
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa Dondakoo na namna unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na sababu zinazosababisha kinjwa au mdomo kutoa harufu mbaya?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu dalili za figo.figo husawazisha maji mwilini pamoja na kuchuja mkojo.
Soma Zaidi...Post yetu inaenda kuzungumzia kuhusiana na Saratani ya Matiti ni Saratani ambayo hutokea katika seli za matiti. Baada ya Saratani ya Ngozi, Saratani ya matiti ndiyo Saratani inayojulikana zaidi hugunduliwa kwa wanawake Mara nyingi. Saratani yaÂ
Soma Zaidi...Katika somo hili na yanayofuata utajifunz akuhusu ini. Post hii ina muendelezo wa post zinazofuat. Katika mfululizo huuutajifunz akuhusu ini na maradhi yake na kujiking nayo.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na mambo hatari yanayosababisha ugonjwa wa moyo.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Maambukizi ya sikio mara nyingi ni maambukizi ya bakteria au virusi ambayo huathiri sikio la kati, nafasi iliyojaa hewa nyuma ya ngoma ya sikio ambayo ina mifupa midogo ya sikio inayotetemeka. Maambukizi ya si
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe wa tishu za matiti kwa wavulana au wanaume, unaosababishwa na kutofautiana kwa homoni za estrojeni na testosterone. Pia unaweza kuathiri matiti moja au zote mbili, wakati mwingine bila usawa. Watoto wachanga,
Soma Zaidi...Saratani ya kibofu cha nyongo ni Saratani inayoanzia kwenye kibofu cha nyongo. Nyongo yako ni kiungo kidogo, chenye umbo la peari upande wa kulia wa tumbo lako, chini ya ini lako. Kibofu cha nyongo huhifadhi nyongo, Kioevu cha usaga
Soma Zaidi...