Post hii inahusu zaidi sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa,ni sababu ambazo uweza kuchangia kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa.
Sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa.
1. Sababu ya kwanza vifaa vinavyotumika kuzalisha watoto.
Kuna wakati mwingine vifaa vinavyotumika kuzalisha watoto usababisha kuchubuka kwa mtoto inawezekana kabisa ni kwa kuchubuka kwa ndani au kuchubuka kwa ngozi ya nje, Kuna Kipindi mtoto anakuwa ameshatoa kichwa ila kutoka nje huwa ni shida na hata kama mama akisukuma kwa namna gani mtoto hawezi kutoka hali inayosababisha vifaa mbalimbali kutumika Ili kuweza kumtoa mtoto nje na kuokoa maisha ya mtoto na Mama kwa hiyo katika kimvuta mtoto atoke usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa kwa hiyo ni vizuri kabisa wataalamu wa afya na wahudumu wa mtoto aliyevutwa kwa kutumia vyuma kuangalia mara kwa mara Ili kuweza kugundua kama michubuko ni ya ndani au ya nje na kuweza kutumia matibabu.
2. Pia michubuko utokea mara nyingi kwa watoto wanaozaliwa kwa kutanguliza matako, kwa kawaida mtoto anapaswa kutanguliza kichwa ikitokea mtoto akatanguliza matako, au miguu usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa,kwa sababu matako na miguu uweza kuzaliwa ila Kuna Kipindi mabega na mikono ushindwa kutoka, katika kupambana ili kuweza kutoa mikono na mabega au pengine kichwa usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa, na pia sio michubuko tu kwa wakati mwingine ulemavu wa mikono na mabega uweza kutokea kwa watoto, kwa hiyo kwa akina mama wanaojifungua ikitokea mtoto alikuwa ametanguliza matako au miguu na akazaliwa kwa shida kwa kupambana ni vizuri kabisa kuangalia mabadiliko yoyote na kumwambia wataalamu wa afya Ili kuweza kuepuka madhara mengine zaidi.
3. Mtoto kutanguliza mabega.
Kuna wakati mwingine mtoto anaweza kutanguliza kichwa na kichwa kikazaliwa ila mabega yakakwama kwenye mfupa wa mama ambao kwa kitaamu huiitwa pubic bone, kwa hiyo katika kupambana kuzalisha mabega Ili mtoto atoke usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa, kwa hiyo ni vizuri kabisa kujua dalili za mtoto aliyetanguliza mabega Ili kuweza kutafuta mbinu za kuzalisha mama huyo au kutafuta wataalamu zaidi, na dalili ambazo ujitokeza ni kama zifuatazo.
Mama huwa na wasiwasi mkubwa kuliko kawaida na pia uhisi kitu ambacho sio cha Kawaida kwa hiyo kwa wahudumu wa afya ni vizuri kabisa kuwa karibu na mama Ili kuweza kumweka mama kwenye hali nzuri na ya kwamba kila kitu kitakuwa sawa.
4.Kichwa cha mtoto kutolingana na kiuno cha mama kwa pale mtoto anapopaswa kupitia.
Kwa kawaida kichwa cha mtoto ni lazima kabisa kulingana na kiuno cha mama kwa pale mtoto anapopaswa kupitia, hali ambayo usababisha mtoto kutumia nguvu nyingi Ili kutoka nje ,hali hii kwa kitaamu huiitwa disproportionate pelvic, kwa hiyo kabla ya mama kujifungua ni lazima kujua hali halisi ya mtoto anapotaka kujifungua kama anaweza kupita au hawezi kupita kwa kufanya hivyo tunaweza kuepuka matatizo mbalimbali kwa watoto kama vile kuchubuka na ulemavu mwingine kama huo.
5. Na tatizo jingine mama kukaa kwenye Kipindi cha kujifungua kwa mda mrefu , yaani kwa kitaamu huiitwa prolonged labor.
Ni hali ambayo mama huwa na uchungu wa mda mrefu na pia anakaa kwenye uchungu kwa mda huo inawezekana ukawa mchache ule ambao haiwezekani mtoto kuzaliwa, kwa hiyo mtoto uchoka na kwa pengine usababisha kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa,
6. Vile vile Kuna hali ya uchungu kuwa mkali na kichwa cha mtoto hakishuki chini, kwa kitaamu huiitwa obstruction labour.
Hii ni Sina ya labor ambapo uchungu unakuwepo wa kutosha lakini kichwa cha mtoto hakishuki, kwa sababu uchungu upo na mtoto anapambana kutoka ila kichwa hakishuki kwa hiyo hali hiyo usababisha kuchoka kwa mtoto na pia mtoto uweza kupata michubuko,hali hii pia usababisha mama kupasuka kizazi na kusababisha kupoteza mtoto na pia kuleta matatizo kwa mama na pengine kizazi kikisha pasuka usababisha kutolewa hali hii inaweza kumfanya mama kushindwa kupata naomba ya watoto aliokusudia kupata.
7. Pengine hali inayosababisha kupata michubuko kwa watoto ni pamoja na uchungu kuwa mkubwa zaidi na WA mda mfupi, kwa kitaamu huiitwa precipitate labor.
Ni aina ya uchungu ambao utokea kwa akina mama kwa kawaida utokea kwa mda mfupi na pia mama uweza kujifungua kwa mda mfupi huo, kwa kawaida uchungu huo utumia masaa matatu tu, na pia mtoto uweza kuzaliwa, kwa hiyo mtoto ni kama vile anatoka kwa spidi kubwa na kujibamiza kwenye mifupa mbalimbali ya kiuno cha mama na kusababisha hali ya michubuko.
6. Kwa hiyo akina mama wanapaswa kuwa makini katika Kipindi cha ujauzito kwa sababu Kuna vitu vingine ambavyo usababisha madhara kwa watoto na vile vile akina mama wanapaswa kuhudhuria Kipindi cha mahudhulio yote wakati wa ujauzito Ili kuweza kugundua dalili za hatari na mambo ambayo usababisha michubuko na matatizo mengi mbalimbali .
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 1539
Sponsored links
👉1
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2
Simulizi za Hadithi Audio
👉3
kitabu cha Simulizi
👉4
Kitabu cha Afya
👉5
Kitau cha Fiqh
👉6
Madrasa kiganjani
Namna ya kuchoma chanjo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuchoma chanjo, ni njia ambazo utumika kutoa chanjo kwa watoto na watu wazima kwa utaratibu uliowekwa. Soma Zaidi...
Dalili za shambulio la hofu
Shambulio la hofu ni tukio la ghafla la hofu kali ambayo husababisha athari kali za kimwili wakati hakuna hatari halisi au sababu inayoonekana. Mashambulizi ya hofu yanaweza kuwa ya kutisha sana. Mashambulizi ya hofu yanapotokea, unaweza kufikiri kwamba Soma Zaidi...
Huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Post hii inahusu zaidi tiba na huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri. Soma Zaidi...
Nini husababisha mdomo kuwa mchungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu Soma Zaidi...
Ajali ya jicho
Post hii inahusu zaidi ajali ya jicho na visababishi vyake, ajali ya jicho ni pale jicho linavyoingiliwa na uchafu na vitu vingine ambavyo havistahili kuwa kwenye jicho Soma Zaidi...
Ukiwa unalima sana unaweza kukonda
Unadhanivkufanya kazi kunaweza kukusababishia maradhi ama mwili kudhoofu, ama kukonda. Umeshawahivkujiuliza wanao nenepa huwa hawafanyi kazi? Soma Zaidi...
Kazi ya protin na vyakula vya protini mwilini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya kazi ya protin na vyakula vya protini mwilini Soma Zaidi...
Zijue kazi za ovari
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa ovari kwenye mwili wa mwanamke. ovari ni sehemu ambapo mayai ya mwanamke hutunza, kwa hiyo kila mwanamke huwa na ovari ambayo husaidia kutunza mayai. Soma Zaidi...
Namna ya kumfanyia usafi Mgonjwa kwa mwili mzima.
Posti hii inahusu namna ya kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima, ni njia ambazo utumika kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima au kumwosha Mgonjwa hasa wale walio mahututi na hawawezi kuamka kitandani. Soma Zaidi...
Namna ya kumsafisha mgonjwa kinywa
Posti hii inahusu namna ya kumsafisha mgonjwa kinywa,ni njia unazopaswa kufuata wakati unamsafisha mgonjwa kinywa hasa wale walio mahututi. Soma Zaidi...