Posti hii inahusu namna ya kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima, ni njia ambazo utumika kumfanyia mgonjwa usafi mwili mzima au kumwosha Mgonjwa hasa wale walio mahututi na hawawezi kuamka kitandani.
Namna ya kumwosha Mgonjwa.
1.Kwanza kabisa tunajua kuwa kama mgonjwa hajiwezi na hawezi kuamka mara nyingi usahaulika kwa upande wa usafi, nimeshuhudia mara nyingi wagonjwa wa hivi ukiwaosha hali zao zinabadilika na anapata nafuu na mgonjwa hasipooga kwa mwezi mzima anaweza hasipone haraka kwa hiyo tunapaswa kuwasafisha wagonjwa kama ifuatavyo.
2. Kwanza kabisa unaondoa mashuka ya juu ya mgonjwa na hakikisha hakuna Watu ambao hawahusiki na labda msaidizi tu na siku zote tumia maji ya moto na pia ondoa mito na bakiza kidogo ambayo inaweza kumfanya aweze ku kukaa vizuri.
3.Anza kutoa mashuka ya upande mmoja wakati mgonjwa umemlaza upande na mashuka hayo umeyasogeza kwa upande ambao ameulalia na chukua maji na sabuni weka kwenye Dodoki na anza kusafisha upande mmoja na pia hakikisha chini kuna mpira ili kuepuka kulowanisha kitanda na suhuza sehemu hiyo kwa kitambaa ambacho kimekamuliwa vizuri na hakikisha upande unatakata.
4.Mgeuze vizuri mgonjwa kwa upande wa pili na Isha upande huo vizuri kwa kuweka maji na sabuni kwenye Dodoki na sugua vizuri na baadae suuza kwa kitambaa kisafi kilichokamuliwa na ukimaliza upande wa pili, nenda kwenye sehemu za siri weka maji kwenye kutimbaa pangusa vizuri pia suuza nenda kwenye miguu na fanya hivyo hivyo ila kama mgonjwa anaweza kujifanyia usafi kwenye sehemu za siri mwache afanye mwenyewe.
5.Baada ya hapo mpake mafuta na ondoa mashuka machafu yaliyokuwepo wakati unamsafisha mvalishe nguo na pia mtandikie vizuri na mgonjwa akifanyiwa hivyo mara kwa mara kama alikuwa mahututi na hali yake itakuwa nzuri kabisa na wakati mgonjwa unamsafisha maji lazima yabadilishwe kutoka sehemu moja kwenda nyingine
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowPost hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia vijana wakati wa kubarehe, ni njia za kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na mwelekeo ,
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari, ni wagonjwa waliopata maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi malengo ya kumsafisha mgonjwa nywele zake, ni sababu ambazo upelekea kumsafisha mgonjwa nywele kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujikinga na kisukari
Soma Zaidi...Maumivu ya shingo ni malalamiko ya kawaida. Misuli ya shingo inaweza kuchujwa kutokana na mkao mbaya - iwe inaegemea kwenye kompyuta yako kazini au kuwinda benchi yako ya kazi nyumbani.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vitamin
Soma Zaidi...Degedege ni ugonjwa unaoshambulia sana watoto chini ya miaka mitano,na uwaletea matatizo mengi pamoja na kuwepo kwa ulemavu na vifo vingi vinavyosababishwa na ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kqa mgonjwa aliyeingiliwa na kitu au uchafu kwenye sikio.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko
Soma Zaidi...