image

Pilipili kali

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za pilipili kali

Pilipili kali.

 Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi.

 

Pilipili zote zina vitamin A, C na K lakini pilipili nyekundu zimezidi wenzie. Wataalamu wa afya wanazungumza kuwa antioxidant, vitamin A na C vilivyomo kwenye pilipili husaidia katika kuzuia maradhi ya saratani na baadhi ya maradhi yanayohusiana na kuzeheka, na pia husaidia katka kuboresha mfumo wa kinga. Pia vitamin K husaidia katika kuganda kwa damu, kuimarisha mifupa pia husaidia katika kulinda seli.

 

Pilipili nyekundu ni chanzo kizuri cha carotenoid ambayo hutambulika kama lycopene, hii ni mujarabu sana katika kuzuia mwili kupata maradhi ya saratani ya kibofu, njia ya uzazi kwa kinamama na saratani ya kongosho.pia kuna carotenoid inayotambulika kama cryptoxanthin hii nayo hujulikana kwa uwezo wake wa kupambana na kuzuia mwili kupata saratani ya mapafu inayohusiana na uvutaji wa sigara.

 

Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pilipili husaidia katika kurekebisha mapigo ya moyo na kuongeza joto la mwili kwa muda wa dakika 20 baada ya kuila. Hii inaonesha kuwa mwili utakuwa na uwezo wa kuunguza mafuta na cholesteral za ziada kwa muda huo. Pia tafiti nyingine zinaonesha kuwa pilipili husaidia katka kupunguza athari za vidonda vya tumbo kwani husaidia katika kuuwa bakteria ndani ya tumbo.

 

Ndani ya pilipili kuna antioxidant iitwayo piperine. Wataalamu wa afya wanadai kuwa ulaji wa antioxidant husaidia katika kuimarisha afya ya mtu. Piperine inatambulika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti na kulinda uharibifu wa seli. Pia ulaji wa pilipili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo.

 

Kwa ufupi pilipili husaidia sana kwa afya ya mlaji. Pia pilipili husaidia katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi ya kisukari, saratani na maradhi ya moyo. Afya ya ubongo, kuimarisha mapigo ya moyo pamoja na kupunguza mgando wa mafuta kwenye mirija ya damu. Pilipili husaidia katika kuufanya mwili uweze kunyonya virutubisho muhimu kutoka kwenye chakula.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1695


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Maumivu ya tumbo baada ya kula
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Stafeli
Soma Zaidi...

Nini maana ya protini
Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa Soma Zaidi...

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
Zijuwe dawa za kuongeza nguvu za kiume, na vyakula salama vya kuongeza nguvu za kiume Soma Zaidi...

MATUNDA YENYE VITAMINI C KWA WINGI
Matunda yenye vitamni C kwa wingi ni machungwa, maembe, ndimu na limao, endelea kusoma Soma Zaidi...

Vijuwe virutubisho vilivyomo kwenye parachichi.
Posti hii inahusu zaidi virutubisho vilivyomo kwenye parachichi, tunajua sana kuwa parachichi ina virutubisho vingi ambavyo vinaweza kuleta faida nyingi kwenye mwili kama yalivyo matunda na vyakula vingine. Soma Zaidi...

Vinywaji vyakula salama kwa mwenye Presha ya kupanda
Je umesha wahi kujiuliza kuwa ni vinywaji vipi mwenye presha ya kupanda anafaha kutumia, Unadhani ni maji, mvinyo wa pombe, chai na kahawa. Bila shaka ungependa kujuwa zaidi kuhusu jambo hili. Makala hii ni kwa ajili yako Soma Zaidi...

Faida za ubuyu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ubuyu Soma Zaidi...

Faida za kula nazi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nazi Soma Zaidi...

Faida za kula Nazi
Nazi ni katika matunda bora sana kiafya, Soma faida zake kwa afya yako Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Chungwa
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Karoti
Soma Zaidi...