Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya protini
NINI MAANA YA PROTINI
Protini ni chembechembe zinazotokea kwa njia ya asili (bila ya kutengenezwa) na zimetokana na asidi za amono (amino acid) zilizounganishwa kwa kutupia bondi za peptide. Neno protini asili yake ni lugha ya Kigiriki ”proteios” likiwa na maana ya kuwa ni kitu kinachopewa nafasi ya kwanza. Yaani protini ni viinilishe “nutrients” ambazo ni muhimu sana mwilini kuliko viinilishe vingine. Neno hili limeanzaka kutumiwa karne ya 19 mwaka 1838 na Mkemia kutoka Swedih Jöns Jacob Berzelius.
Protini huweza kutofautiana namna zilivyo kutoka kiumbe kimoja na chingine, pia protini huweza kutofautiana kutoka kiungo kimoja kwenda kingine. Kwa mfano protini za kwenye macho ni tofauti na zile za kwenye moyo, ini na figo. Kila kiumbe hai kina protini, na pia protini huhusika katika michakato tata kwenye miili ya viumbe hai, kwa mfano protini huhusika katika kutengeneza antibodies ambazo hutengeneza kinga na kupambana na maradhi na wadudu shambulizi kama bakteria na virusi. Protini hutengeneza enxymes ambazo ndizo hutumika katika kumeng’enya chakula. Pia protini hutengeneza homoni (hormones)
Baada ya kukila chakula chenye protini chakula kinaanza kumengenywa kinapofika kwenye tumbo na utumbo, kisha hufyonzwa kwenye utumbo mdogo na kuingia kwenye mirija ya damu. Pindi chembechembe za protini zinapoingia kwenye damu, damu huanza kusafirisha protini kwenda maeneo mbalimbali ya mwili yanayohitajia protini. Huko protini zitaingia kwenye seli za mwili. Ndani ya seli mchakato kwa kuvunjwa vunjwa protini ili kutumiwa zaidi hufanyika. Ndani ya seli mchakato huu jhufanyka kwenye sehemu inayotambulika kitaalamu kama ribosomes
Miili ya wanyama haina uwezo wa kuhifadhi protini kwa matumizi ya baadaye. Hivyo kama mtu atakula protini nyingi, mwili utaibadili protini kuwa fati na baadaye kutumika kutengeneza nishati ndani ya mwili. Na endapo mtu hataweza kupata protini za kutosha mwili utaanda kuangalia maeneo yenye protini ndingi kama misuli, kisha mwili utaanza kuvunja protini iliyomo mule na kuipeleka maeneo mengine na hapa mtua ataanza kukonda na kupoteza nyama na hatimaye kufariki kama hatapata chakula chenye protini.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2796
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 kitabu cha Simulizi
Rangi za majimaji yanayotoka kwenye uke na maana yake kiafya
Je unajuwa kuwa majimaji yanayotoka ukeni yanatueleza mengi kuhusu afya yako, rangi za majimaji ya ukeni na damu ya hedhi Soma Zaidi...
Vyakula vizuri kwa vidonda vya tumbo
Hii ni orodha ya vyakula salama na vizuri kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula samaki
Soma Zaidi...
Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo, na vyakula salama kwa vidonda vya tumbo
Makala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Soma Zaidi...
Naombakujua kujua Kama huu uyoga unasaidia kansa Kama kwawazee
Mpaka sasa hakuna dawa ya kuponyesha saratani wala kinga ya saratani. Hata hivyo vipo vyakula ambavyo vinakadiriwa kuwa hupunguza hatari ya kuweza kupata saratani. Je unadhani uyoga ni moja ya vyakula hivyo? Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula Chungwa
Soma Zaidi...
Tufaha (apple)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula apple/tufaha Soma Zaidi...
Kazi za madini ya Shaba mwilini.
Post hii inahusu zaidi madini ya Shaba mwilini,ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini, kama ifuatavyo Soma Zaidi...
Tangawizi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za tangawizi Soma Zaidi...
Rangi za matunda
Fida za matunda huanzia kwenye rangi zake, je unajuwa kama rangi ya matunda inaeleza jambo? Soma Zaidi...
je ni vipi vyakula vyenye protini kwa wingi?
Makala hii iatakuletea aina kuu tano za vywkula vyenye protini nyingi zaidi. Kama ulikuwa unajiuliza kuwa ni vyakula ipi hasa vinaweza kukupatia protini kwa wingi ni vipi, makala hii ndio majibu yako kwa swali hilo. Soma Zaidi...
Faida za kiafya za topetope (accustard apple/sweetsop)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula topetope Soma Zaidi...