Je unajuwa kuwa majimaji yanayotoka ukeni yanatueleza mengi kuhusu afya yako, rangi za majimaji ya ukeni na damu ya hedhi
/p>
Majimaji yanayotoka kwenye uke ikiwemo damu ya hedhi kitaalamu yanajulikana kama vaginal discharge yanaweza kuwa na rangi mbalimbali unaweza pia kujiuliza lamda utakuwa unaumwa, kwani muda mwingine unaweza kuona yanatoka yakiwa na rangi ya tofauti kabisa. Kama ulivyo mkojo hubadili rang halikadhalika hata majimaji yanayotoka ukeni huweza kubadili. Makala hii itakwenda kukueleza maana za kiafya kutokana na rangi za majimaji haya:-
Majimaji haya yana umuhimu mkubwa sana katika kulinda afya ya mwanamke na ujauzito. Miongoni mwa kazi zake ni:-
1.kuondoa uchafu mwilini mwa mwanamke
2.Kuondoa seli zilizokufa mwilini
3.Kulinda mimba dhidi ya bakteria, fangasi na virusi
4.Kulinda mwili wa mwanamke dhidi ya vimelea vya maradhi visiingie kwenye mfumo wa kizazi kwa kupitia ukeni
5.Kuweka mfumo wa kizazi katika usalama na ubora wake.
Kiasi cha majimaji yanayotoka ukei huweza kutofautiana kwa rangi kulingana na siku katika mzunguruko wake wa hedhi. Kwa mfano:-
1.siku ya 1 - 5 hapa ni mwanzo wa hedhi, kwa mwanake aliye katika umri wa kupata hedhi majimaji yanayotoka kwenye uke wake yatakuwa ni mekundu ama yenye damu.
2.Siku ya 6 - 14 hii ni baada ya kukata kwa hedhi, hapa mwanamke hataona majimaji mengi kwenye uke kwake. Ila kadiri siku zinavyoenda yataanza kubadilika na kuwa kama mawingu ama rangi nyeupe pia yanaweza kuwa na rangi ya nnjano na kunatanata.
3.Siku ya 14 - 25 hapa yai linakuwa limesha toka, hivyo majimaji yanaanza kuwa na utelezi mwingi na kufanana na yale majimai meupe ya yai baada ya kulivunja. Na baada yamuda yanarudi kuwa na mawingu, meupe ama njano.
4.Siku ya 25 - 28 majimaji haya ytakuwa mepesi sana na ni machache sana.
Ok tumeshaona mabadiliko hayo ya majimaji yanavyobadilika kulingana na siku. Sasa hebu tuone babadiliko haya ra angi yanatuambia nini kiafya:-
1.rangi nyekundu:-
Hii ni damu ya hedhi, mara nyingi damu hii inakuwa ni angaβvu na yenye kufanana na rangi ya kutu. Hii ni kawaida kwa wanawake wote hivyo inaashiria afya ya kawaida. Na endapo itatoka kwa siku nyingi zaidi ya wiki, kiafya haionyeshi usalama. Ni vyema kumuona daktari aliye karibu nawe.
2.rangi nyeupe
Majimaji meupe yaaweza kuwa na rangi kama ya cream ama njano iliyo pauka. Kama mwanamke hana dalili zozote basi rangi hii inaonyeka mwanamke huyo yupo katika afya njema.
Hata hivyo ikiwa majimaji haya ni meupe na yameshikamana kama maziwa ya mgando au yakiwa yana harufu kali inaweza kuashiria kuna maambukizi ya vimelea vya maradhi kama fangasi na bakteria.
Ila kwa mara nyingi majimaji meupe yakiwa mazito, yana harufu kali hali hii inahusiana na maambukizi ya fangasi. Hali hii inaweza kusababisha miwasho.
3.Rangi ya ngajo na kijani
Kama majmaji haya yana rangi ya njano huenda hakuna tatizo ila yakiwa ni njano iliyowiva ama njano iliyona ukijani ama majimaji haya yakiwa ni ya kijani hii huashiria maambukizi ya bakteria ama magonjwa ya zinaa, fika kituo cha afya kama yatakuwa yanatoa harufu mbaya.
4.rangi ya kahawiya
Majimaji ya rangi hii yanakuwa na damu kwa mbali. Hali hii ni kawaida kama itatokea siku chache kabla ya kuingia hedhi. Pia inaweza kuashiria mimba changa. Na majimaji haya yatakuwa yanatokea baada ya kukutana kimwili, hii inaashiria kuwa kuna michubuko imetokea kwenye uke na kusababisha mipasuko midogo iliyokuwa ikivija damu..
5.majimaji yaliyo safi.
Katika hali ya kawaida majimaji yanayotoka ukeni yana kuwa ni safi na yenye weupe na yenye kuteleza kama vile majimaji meupe yanayotoka baada ya kupasua yai.
6.rangi ya kijivu
Majimaji ya rangi ya ijivu sio ya kawaida hivyo yanaashiria kuwa kuna sida katika afya ya mwanamke na mara nyingi ji maambukizi ya bakteria wanotambulika kama bacterial vaginosis. Dalil nyingine za baktera hawa bi:-
1.Maumivu
2.Miwasho
3.Harufu mbaya
4.Kuwa na wekundu kuzunguka mashavu ya uke na kwenye mlango wa uke.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 5931
Sponsored links
π1 Kitabu cha Afya
π2 kitabu cha Simulizi
π3 Simulizi za Hadithi Audio
π4 Kitau cha Fiqh
π5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
π6 Madrasa kiganjani
Namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa matumizi mbalimbali
Posti hii inahusu zaidi namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa ajili ya matumizi mbalimbali, Ili kutumia mmea wa mchai chai zifuatazo ni mbinu za kuandaa mmea huu. Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula spinach
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach Soma Zaidi...
Fahamau protini na kazi zake, vyakula vya protini, na athari za upungufu wake.
unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo Soma Zaidi...
Zijuwe kazi na faida za Vitamini C mwilini
Vitamini C ni moja kati ya vitamini muhimu sana katika kuboresha ufanyaji kazi wa mfumowa kinga mwilini yaani immune system. Katika post hii utakwenda kujifunza kazi za vitamini C mwilini Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula ukwaju
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula uyoga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula uyoga
Soma Zaidi...
Faida za kula fyulisi/peach
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula fyulisi/ peach Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula ukwaju
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula Nyanya
Soma Zaidi...
AINA ZA VYAKULA NA UPUNGFU WA VIRUTUBISHO
zijuwe aina za vyakula Soma Zaidi...
Faida za nazi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nazi Soma Zaidi...
Vyakula murajabu kea mwenye presha ya kushuka
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula murajabu kea mwenye presha ya kushuka Soma Zaidi...