Navigation Menu



image

Mishipa ya machozi kufunga kwa mtoto.

Posti inahusu nzaidi kufunga kwa mishipa ya machozi ya mtoto kwa kawaida mishipa ya mtoto inapaswa kufunguka baada ya mwaka mmoja lakini kwa wengine ubaki imefungwa hata baada ya mwaka mmoja na kusababisha madhara mbalimbali kwa mtoto.

Sababu za mishipa ya machozi kufunga kwa mtoto.

1.Kama tulivyotangulia kusema kwamba mishipa ya watoto wadogo uanza kufunguka pale anapofikisaha wiki 2 mpaka miezi 3 ama  lakini kwa watoto wengine mishipa huu ubaki  imefungwa na kusababisha madhara makubwa kwa mtoto katika makuzi yake, kwa hiyo kuna sababu mbalimbali ambazo ufanya mishipa hiyo kufunga na kusababisha madhara makubwa kwa mtoto kama ifuatavyo.

 

2. Pengine kuna valve ambazo zipo kwenye mwisho wamishipa ya machozi kutofunguka kama inavyotakiwa.

Kwa kawaida kwa mtoto ni lazima valve zote ambazo ziko kwenye macho zinapaswa kufungunguka kwa wakati wake lakini nyingine hubakia zimefungwa hali ambayo Usababisha mishipa ya machozi kwa mtoto kufunga na kusababisha madhara  kwa mtoto na kwa jamii inayotunza mtoto huyu kwa hiyo tatizo liligunduliwa linaweza kutibiwa ambapo upasuaji unaweza kufanyika ili kufungua hizo valve.

 

3. Kuwepo kwa uwazi sehemu ambapo machozi upitia 

Kwa sababu ya kuwepo kwa uwazi kwenye sehemu ya machozi yanapopitia kwa kitaalamu huitwa eylid usababisha mishipa ya machozi kufunga, kwa hiyo ili tatizo la kuwepo kwa uwazi usababishwa na maumbile ya mtoto au kuna Maambukizi ya macho ambayo Usababisha kuwepo kwa uwazi huo.Na pia hili tatizo linaweza kusaidiwa kwa kuwepo kwa upasuaji na kuziba sehemu hiyo.

 

4. Mishipa ya machozi kuwa nyembamba kuzidi kawaida.

Kwa wakati mwingine kuna kipindi mishipa ya machozi inakuwa kweli nyembamba kupita kiasi hali ambayo Usababisha kufunga kwa mishipa ya machozi kwa watoto, kwa hiyo basi ni vizuri kabisa kumpeleka mtoto hospitalini ili kuweza kuona tatizo mliko wapi na kuweza kulifanyia kazi kwa hiyo mishipa nya machozi kwa kawaida inapaswa iwe mipango.

 

5.Kuwepo kwa Maambukizi kwenye macho.

Kwa wakati mwingine maambukizi ndicho chanzo kikuu cha kuwepo kwa Ugonjwa huu, kwa sababu kama kuna Maambukizi ni vizuri kuyatibu ili kuweza kuruhusu mishipa ya machozi iweze kufunguka na mtoto aweze kuwa kama watoto wengine.

 

6. Kuuumia kwenye eneo la mishipa ya machozi na  mifupa ya pua kuziba.

Kwa wakati mwingine mtoto anaweza kuumia kutokana na vitu mbalimbali kwenye eneo la mishipa ya machozi na kusababisha kufunga kwa mishipa ya machozi na kwa wakati mwingine kama kunakuwepo na kuziba kwenye mishipa ya pua pia usababisha kuziba kwa mishipa ya machozi.

 

Dalili za mishipa ya machozi kufunga kwa mtoto.

Pengine tunaweza kujiuliza juwa ni Dalili zipi zinazoonyesha kubwa kuna tatizo kwenye mishipa ya machozi kwa sababu tatizo lenyewe liko ndani na hatuwezi kuliona kwa nje, kwa hiyo Dalili ni kama ifuatavyo.

 

1. Macho kuwa na maji maji.

Kwa kawaida kama mishipa ya machozi imefungwa kitu cha kwanza utaona macho ya mtoto yanatoa maji mara kwa mara na pia mtoto anakaa bila raha kwa wakati mwingine macho yanakuwa yanawasha na mtoto anajikuna kwa hiyo hali hii umfanya mtoto kujihisi vibaya hata kama anacheza na wengine na kwa wakati mwingine wanakuwa wanamnyanyapa kwa sababu ya kutokwa na majimaji machoni.

 

2. Na pia macho ya mtoto mda wote yanakuwa yanatoka na Matongo tongo.

Kwa kawaida uchafu kwenye macho unakuwa hauna sehemu ya kuchujiwa kwa hiyo Matongo tongo utoka machoni, na kwa wakati mwingine ni kwa sababu ya kuwepo na Maambukizi kwenye jicho ndio yanasababisha hali ya kuwepo kwa Matongo , kwa hiyo mtoto anakosa raha na kujitenga na wengine kwa sababu ya tatizo la kuwepo kwa Matongo tongo kwenye macho

 

3. Uchafu mwingi kutoka machoni na pengine unakuwa na harufu mbaya.

Kwa wakati mwingine kunakuwepo na uchafu mwingi kwenye macho ambapo mtoto ukaa anapangusa uchafu kwa kitambaa kama ameshakuwa na uwezo huo kwa wakati mwingine mtoto anakuwa na mafua yanayoambatana na uchafu kutoka kwenye macho.

 

4.Na pia presha ya macho inawezekana kutokea ikiambatana na upofu 

Kama tatizo halijafanyiwa ufumbuzi na kuweza kutibiwa upofu wa macho unaweza kutokea kwa mtoto na kusababisha madhara makubwa zaidi. Kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi ni vizuri kufanya mawasiliano na wataalamu wa afya ili kuweza kupata matibabu kwa mda mwafaka.






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2014


Sponsored links
πŸ‘‰1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Ni ipi siku ya kupata ujauzito, na nitajuwaje kama nimepata ujauzito?
Hapa utajifunza siku nzuri kushoriki tendo la ndoa kupata ujauzito, dalili za siku hiyo na kuitafuta kwa mahesabu Soma Zaidi...

Siku za kupata mimba
Nitakujulisha siku ya kupata mimba na sifa zake, na namna ya kuweza kuitafuta Soma Zaidi...

Faida za uzazi wa mpango kwa watu wenye ugonjwa wa Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, ni faida wanazozipata waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi. Soma Zaidi...

Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za maumivu ya tumbo chini upande wa kulia Soma Zaidi...

Zijue Dalili za hatari kwa Mama mjamzito
Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa Mama mjamzito, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama mjamzito, hizi Dalili zisipofanyiwa kazi mapema zinaweza kuleta shida kwa Mama kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua Dalili hizi na kuchukua hatua endapo zitajio Soma Zaidi...

Dalili Za hatari ambayo zinaweza kusababisha ugumba
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zilijitokeza zinaweza kusababisha ugumba hasa kwa wanawake, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa makini kwa Dalili hizi hasa kwa wadada, kama kuna uwezekano wa matibabu tibu mapema ili kuepuka tatizo la kuwa mgumba. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuacha kupiga punyeto.
Post hii inakwenda kukupa njia za kukusaidia kuacha punyeto. Soma Zaidi...

Mimi nilipima na kipimo mwenyewe nkakuta mistari miwili iliokoza lkn nikifanya tendo nakua naumia sana tatizo ni Nini docta
Je anapatwa maumivu 😭 makali wakati wa tendo la ndoa ama ukiwa katika hedhi? Soma makala hii hadi mwisho Soma Zaidi...

ukeni psnawasha pia sehemu za mashavu panamchubuko umetoka je tatizo Ni nini
Soma Zaidi...

Dalili za ongezeko la homoni ya estrogen
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa homoni ya estrogen imeongezeka, hizi dalili zikitokea mama anapaswa kuwahi hospital ili kuweza kupata matibabu au ushauri zaidi. Soma Zaidi...

Sababu za kuwepo fangasi ukeni
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa Ugonjwa wa fangasi,ni sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha fangasi. Soma Zaidi...

Mama mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa?
Mama mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka siku ya kujifungua Kama mume wake pamoja na yeye akiwa Hana maambukizi ya zinaa na Kama akiona dalili zozote zile za hatari ndio hataruhusiwa kushiriki tendo la ndoa. Soma Zaidi...