Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa Mama mjamzito, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama mjamzito, hizi Dalili zisipofanyiwa kazi mapema zinaweza kuleta shida kwa Mama kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua Dalili hizi na kuchukua hatua endapo zitajio
Dalili za hatari kwa Mama mjamzito
1. Kutokwa na damu ukeni.
Kutokwa na damu kunaweza kuwa sio dalili mbaya, kwani si jambo la kuogopa na ni hali inayoweza kumtokea mjamzito. Lakini tunatarajia damu hii sio nyingi. Endapo damu hii itaambatana na maumivu makali ya tumbo, ama kizunguzungu ama maumivu makali ya kichwa, ni vyema kufika kituo cha afya. Pia endapo damu hii itakuwa nyingi kiasi cha kuhitaji kujisitiri pia ni vyema kufika kituo cha afya kwa uangalizi.
2. Dalili ya hatari nyingine kwa Mama mjamzito ni mtoto kushindwa kucheza tumboni, kwa kawaida uhai wa mtoto akiwa tumboni ni kuhisi kuwa mtoto anacheza pindi mtoto akishindwa kucheza hiyo ni Dalili ya hatari , wakati mwingine ni mabadiliko ya Mama kama vile uchovu na sababu nyingine nyingi, kwa hiyo mama akisikia mtoto amepitisha siku bila kucheza anapaswa kwenda hospitalini mara moja ili aweze kupata msaada zaidi.
3. Kuvimba miguu kwa wajawazito.
Na hili ni mojawapo ya Dalili ya hatari kwa Mama , ambapo maji mengi yanayoka kwenye seli yanakuja kwenye tisu na pengine ni kwa sababu ya kupungua kwa protini kwenye mwili na sababu nyingine nyingi kwa hiyo Mama akiona amevimba miguuni anapaswa kwenda hospitalini ili kupata matibabu na maelekezo zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya pia wauguzi wanapaswa kuwaambia wakina Mama kuwa pindi waonapo Dalli hizi wanapaswa kwenda moja kwa moja hospitalini.
4.Maumivu akali ya kichwa kwa Mama mjamzito.
Mama mjamzito akipatwa na maumivu makali ya kichwa anapaswa kujua wazi hali yake ya kuwa ni ya hatari kwa hiyo anapaswa kwenda hospitalini kwa sababu kuumwa sana kichwa kunaweza kusababishwa na presha au mabadiliko yoyote ya mwili ambayo yasipotibiwa kwa wakati yanaweza kuleta kitu kingine kisicho cha kawaida. Kwa hiyo wauguzi na wataalam wengine wa afya wanaswa kuwaambia ukweli kuhusu Dalili hizi za hatari.
5. Kwa kawaida tunajua wazi kubwa akina Mama wajawazito wanapaswa kutunzwa vizuri na kuhakikisha kubwa wasipatwa na janga lolote ambalo linaweza kumfanya awe dhaifu kwa hiyo tunapaswa kujua Dalili za hatari na kuwapeleka hospitali mara moja bila kuchelewa na pia wanapaswa kwenda kliniki mara kwa mara ili kuweza kujua maendeleo ya afya zao na pia jamii iliyowazunguka inapaswa kujua Dalili hizi na kuwawaisha hospitalini bila kuchelewa
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi vipimo muhimu kabla ya kubeba mimba,ni vipimo vya moja kwa moja kutoka maabara na vingine sio vya maabara.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na mathara yanayosababisha Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke
Soma Zaidi...Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maelekezo muhimu kwa mama au mlezi wa mtoto mgonjwa. Ni maelekezo muhimu hasa wakati wa kutoa dawa kwa mtoto.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi imani potofu kuhusu uzazi wa mpango, ni imani walizonazo Watu kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...Kuuma mwa matiti ni moka ya Ichiro kuwa huwenda ni ujauzito. Hii haimaanishi etindio mjamzito, zipo dalili nyingi za ujauzito. Hata hivyo kuona dalili za ujauzito haimaanishi umepata tayari ujauzito. Kwanza fanya vipimondipo Upate uhakika
Soma Zaidi...Kuna njia nyingi zinatajwa zinapima mimba kama chumvi, sukari, mafuta na sabuni. Hata hivyo zipo njia zaidi ya 10 za kiasili za kupima ujauzito. Utajifunza hapa zote
Soma Zaidi...