image

Karanga (groundnuts)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga

. Karanga (ground nuts)

Karanga ni katika vyakula vya asili na ni kiungio cha mboga kwa jamii nyingi sana Tanzania na dunia kwa ujumla. Kama vilivyo vyakula vingine karanga ni katika vyakula vyenye virutubisho vingi. Ndani ya karanga kuna fotale, vitamin E, madini ya copper na arginine. Pia karanga ni chanzo kizuri cha omega-3 fatty acid, vitamin E na ijulikane kuwa fatty acid ni muhimu sana kwa afya ya moyo.

 

Ndani ya kjaranga kuna antioxidant iitwayo phenolic, polyphenol na resveratrol hizi husaidia katika kulinda mwili dhidi ya stress yaani misongo ya mawazo, na husaidia pia katika kulinda mwili dhidi ya maradhi ya saratani. Pia husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini yaani mfumo wa kupambamba na maradhi na mashambulizi ya magonjwa.

 

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa aina ya mafuta (fat) yaliyomo kwenye karanga ni mafuta ambayo ni salama kwa afya ya moyo. Kitaalamu aina ya fat iliyomo kwenye karanga ni monosaturated fat na polyunsaturated fat kwa ufupi fat hizi ni salama kwa afya ya moyo na mfumo mzima wa usukiumwaji wa damu. Kwani fat hizi husaidia katika kupunguza cholesterol kwenye damu hivyo hupunguza hatari ya kupata maradhi ya moyo.

 

Karanga pia ni chanzo kizuri cha protini. Itambulike kuwa protini ni katika virutubisho muhimu na vinavyotakiwa kwa kiwango kikubwa ndani ya miili yetu. Seli za mwili zinahitaji protini kuweza kukuwa na kutengenezwa upya. Ukuaji wa mwili na uponaji wa vidonda na majeraha unahitaji protini.. watoto wanatakiwa wapewe vyakula vya protini kwa kiasi kikubwa zaidi ili kuwezesha maendeleo ya ukuaji wao.

 

Tofauti na protini mwili unahitaji madini kwa kiwango kinachohitajika. Katika karanga kuna aina mbalimbali za madini kama vile magnesium, phosphorus, potassium, zinc, calcium na sodium. Madini yote haya husaidia katika ukuaji wa mwili na mwili kufanya kazi vyema.

 

Mafuta ya karanga yana fatty acid ambayo hutambulika kuwa inaongeza lipoprotein ndani ya mwili inayojulikana kama “good cholesterol” yaani cholesterol iloyo safi. Hii ni muhimu katika kuimarisha afya ya moyo na ubongo. Pia madini ya copper yaliyomo kwenye karanga husaidia katika kuzuia maradhi ya moyo yaani “coronary heart diseases”. pia vitamin B1 (thiamine) ni virutubisho muhimu katika kulinda mwili dhidi ya ufanyaji dhaifu wa kazi wa moyo. Yaani “cardiac failure”. na pia husaidia katika kuimarisha afya ya moyo.

 

Karanga husaidia katika kuboresha ngozi. Virutubisho vilivyomo kwenye karanga pamoja na vitamin C husaidia katika kuilinda ngozi dhili ya mikunjo mikunjo, madowa madowa na kuifanya ngozi iwe ang’avu, yenye majimaji na iyoyokuwa na ukavu au mikunjomikunjo. Uwepo wa anti-ageing phytohemical inayotambulika kama reseveratrol husaidia katika kumfanya mtu asizeheke kwa haraka.

 

Karanga husaidia katika kuimarisha afya ya mifupa, kutokana na uwepo wa madini kama potassium, calcium, sodium, magnesium na phosphorus. Pia kwa wajawazito nivyema wakatumia chakula hiki kwani kuna protini na madini kwa ajili ya afya ya mama na mtoto





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1867


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula mayai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mayai Soma Zaidi...

Fahamu vyakula vya nyuzinyuzi
Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Spinachi
Soma Zaidi...

Vyakula salama kwa mwenye kisukari
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula salama kwa mwenye kisukari Soma Zaidi...

daarasa la afya
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Nini maana ya protini
Unaijuwa maana ya virutubisho vya protini, na kazi zake mwilini. Soma zaidi hapa Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula maini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maini Soma Zaidi...

Je ni kweli vitunguu saumu vinashusha presure
Kitunguu saumu ni tiba mbadala ya presha yabkushuja. Hakitatui tatizo yaani hakiponyeshi, ila husaidia katika kushusha presha iliyo panda. Soma Zaidi...

Vyakula hatari kwa mjamzito hasa mimba changa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya hatari kwa mjamzito hasa mimba changa Soma Zaidi...

Faida za kula kunde, maharage, njegere, mbaazi na njugu mawe
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula kunde, maharage, njegere, mbaazi na njugu mawe Soma Zaidi...

Faida za kula tango
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango Soma Zaidi...

Habari ndugu naomba kuuliza eti mtu akipaliwa na asali anakufa?
Post hii inakwenda kukujulisha hatari za kupaliwa na asali ama kitu kingine kama muulizaji alivyouliza. Soma Zaidi...