Nadharia ya uchumi kiislamu

1.

Nadharia ya uchumi kiislamu

1.Nadharia ya uchumi wa Kiislamu
Mfumo wa uchumi katika Uislamu ni utaratibu utokanao na Qur-an na Sunnah juu ya uzalishaji, umilikaji, usambazaji, na utumiaji wa mali na huduma pamoja na miiko yake. Kwa msingi huo, uchumi huo umejengwa juu ya fikra ya ukati na kati (Iqtisaad), hivyo umetofautiana na mifumo mingine iliyobuniwa na watu.


Dhana (concept) ya ukati (Iqtisaad) katika shughuli za kiuchumi ni kule kutoa uhuru kwa mtu binafsi (sekta binafsi) kuchuma na kumiliki mali ili iwe motisha kwake ya kuchapa kazi wakati huo huo serikali ikisimamia na kutoa miongozo katika uzalishaji na ugawaji, na vile vile kuwa na sekta zake (sekta za umma) ili kila mwana jamii apate haki za kimsingi. Mifumo iliyobuniwa na watu imeathiriwa na udhaifu wa kibinaadamu wa kuelemea upande huu au ule.



Ipo mifumo ya kiuchumi kama vile ubepari ambao umeelemea mno katika ubinafsi kiasi ambacho umepuuza kabisa haki za kijamii. Katika mfumo huu (ubepari) umma hauna chake; mali, huduma na shughuli mbali mbali hubinafsishwa. Wachache chini ya mfumo huu ndio hunufaika na rasilimali za Taifa. Hujilimbikizia mali, na motisha yao ya uzalishaji ni ile faida waipatayo. Serikali kuu ya mfumo huu wa kibepari hushirikiana na wachache hao waliohodhi mali, kuwanyonya walio wengi.



Pia, kuna mfumo wa uchumi wa Kikomunist au Kijamaa ambao nadharia yake imeelemea mno katika 'usawa' wa sare kiasi cha kudhoofisha mno motisha ya watu binafsi na hivyo kupelekea kukosekana kwa ufanisi katika uzalishaji. Katika mfumo huu mali na shughuli mbali mbali hutaifishwa (toka milki ya watu binafsi kuwa milki ya taifa).


Ukweli ni kwamba huwa si mali ya taifa kama inavyotangazwa bali mbiu ya 'usawa', na 'mali ya umma', chini ya mfumo huu, ni mwavuli tu uliokinga kikundi cha watu kilichojipa mamlaka ya uendeshaji wa nchi kwa sura ya chama au serikali kwa maslahi ya kikundi hicho. Kikundi hicho ndicho humiliki na kutafuna mali huku wananchi wengi wakiendelea kudhulumiwa kwa sababu mbali mbali. Hivyo hakuna usawa ulio chini ya mfumo huu bali ni ubinafsi ule ule ambao huhamishwa toka kwa mtu binafsi kwenda kwenye kikundi fulani.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 87

Post zifazofanana:-

KUAMINI MALAIKA WA ALLAH (S.W.)
Soma Zaidi...

HADITHI YA CHONGO WATATU WATOTO WA WAFALME
Soma Zaidi...

NECTA FORM TWO CHEMISTRY PAST PAPERS
Soma Zaidi...

Kulaaniwa Bani Israil
Pamoja na kuteuliwa na Allah(s. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka sura kwenye quran na fadhila za sura mbalimbali kwenye quran
Soma Zaidi...

Kufunga Mwezi wa ramadhani kisheria
Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Furqaan (25:64-76)
Soma Zaidi...

AINA ZA VYAKULA NA UPUNGFU WA VIRUTUBISHO
zijuwe aina za vyakula Soma Zaidi...

Faida za kula Ukwaju
Zitambue faida kubwa za kula karanga kwa ajili ya afya yako Soma Zaidi...

Kamaralzaman akiwa katika ndoto ya kweli
NDOTO AMA KWELI? Soma Zaidi...

Kuamini qadar na qudra katika uislamu
Kuamini Qadar ya Allah (s. Soma Zaidi...

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Soma Zaidi...