Haki za kijamii
Pamoja na haki za kiuchumi, Uislam unampa mwanamke haki za kijamii zifuatazo:
Kwanza, mwanamke amepewa uhuru kamili wa kuolewa na mwanamume ampendaye. Ndoa ya Kiislamu haisihi iwapo mwanamke atalazimishwa kuolewa kinyume na ridhaa yake. Vile vile hapana ruhusa ya kumkataza mwanamke asiolewe na mwanamume ampendaye ndani ya mipaka ya sheria ya Kiislamu.
Pili, mwanamke amepewa haki zote za kisheria za kumuacha mumewe ambaye amekosa nguvu za kiume (impotent), ambaye ni katili kwake na ambaye anamchukia.
Tatu, mwanamume ameamrishwa kutumia madaraka aliyopewa juu ya mkewe kwa huruma na upendo. Kama Qur'an inavyoagiza:
"... basi kaeni nao kwa wema ..." (4: 19). Wala msisahau kufanyiana Ihsani baina yenu ..." (2:237).
Na Mtume (s.a.w) amesema: 'Wabora wenu ni wale walio wema kwa wake zao na watu wao (katika familia)". Kama mwanamume atatumia vibaya madaraka yake, mwanamke ana kila haki ya kukiendea chombo cha sheria na kumshitakia mumewe ambaye hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Nne, wanawake wajane na waliotengana na waume zao wanahaki na uhuru kamili wa kuolewa tena. Haki hii haijapatikana kwa jamii nyingi ulimwenguni.
Tano, kuna usawa kamili kati ya wanaume na wanawake kwa upande wa sheria za madai na jinai. Sheria ya Kiislamu haibagui wala haipendelei mwanamume au mwanamke katika kulinda haki za watu na haki zajamii kwa ujumla. Kwa mfano hukumu ya Kiislamu kwa mwizi ni kukatwa mkono, awe mwanamume au mwanamke kama inavyobainishwa katika Qur'an;
Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, malipo ya yale waliyoyachuma. Ndiyo adhabu itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye He/dma (5:38).
Kuhusu adhabu ya wazinifu tunafahamishwa: Mzinfu mwanamke na mzinfu mwanamume mpigeni kila mmoja katika wao mj/eledi mia. Wala isiwashikeni kwa ajili yao huruma katika kupitisha hukumu hii ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu hiyo kundi la Waislam. (24:2).
Sita, vile vile wanawake nao kama wanaume wanaruhusiwa kutoa ushahidi mahakamani au pale ushahidi wao unapohitajika. Bali katika kipengele hiki itatubidi tuwe wazi kwa kujibu maswali mbali mbali yanayoweza kuulizwa kama vile:
Kwa nini wanatakiwa mashahidi wawili wanawake badala ya shahidi mmoja mwanamume? Je, hii ma maana kuwa Uislamu unamhesabu mwanamke kuwa ni nusu ya mwanamume? La! Hasha. Kama katika suala Ia urithi, ukitazama kwa sura ya nje unaweza kudhani kuwa mwanamke ameonelewa na mwanamume kapendelewa kwa mwanamume kupewa mara mbili ya mwanamke. Hivyo hivyo katika suala Ia ushahidi, kwa kutakiwa wanawake wawili haina maana kuwa Uislamu unamuona mwanamke kuwa ni nusu ya mwanamume. Lau ingekuwa hivyo, Uislam ungeweza kuukataa ushahidi wake moja kwa moja. Na katika karne ya 7A.D iliposhuka Qur'an hata huko kuukubali ushahidi wa mwanamke kulionekana ni kioja na kuruka mipaka.
Na mshuhudishe mashahidi wawili katika watu wenu wanaume. Lakini ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili; katika wale mnaowakubali kuwa mashahidi. Ili kama mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwingine "(2:282).
Ushahidi unaotajwa katika aya hii unahusiana na mikataba ya mambo ya fedha. Mashahdi wanatakiwa wawe ama wanaume wawili au mwanamume mmoja na wanawake wawili. Na sababu ya kuwaweka wanawake wawili imetajwa nayo ni kuwa akisahau mmoja mwenzake atamkumbusha. Swali Ia kujiuliza hapa ni kuwa kwa nini ihofiwe kuwa mwanamke ndiye atakayesahau na siyo mwanamume? Tatizo lililopo hapa kwa kiasi fulani linatokana na kasoro za kutafsiri neno "tadhila" kama kusahau. Neno "tadhila" halina maana ya kutokuwa na kumbukumbu (memory). Kwani mara nyingi wanawake hukumbuka zaidi kumbukumbu zao za kuzaliwa kuliko hata wanaume. Katika Uislam mwanamke ambaye kwa kawaida atakuwa anatimiza majukumu yake kama mke au mama aweza kujishughulisha na hayo kiasi Cha kumfanya asiwe hadhiri sana wakati wa majadiliano yanayohusu kuandikiana mikataba ya masuala ya fedha, masuala ambayo hahusiki nayo mara kwa mara.
Hii ni kwa kawaida, lakini haina maana kuwa kila mwanamke lazima atakuwa hivyo. Hata hivyo kwa sababu lengo Ia sheria ni kulinda haki za watu, sheria imeweka hadhri hiyo iii kuhakikisha kuwa haki za watu zinahifadhiwa. Na lengo si kumdhalilisha mwanamke. Kwani Iau ushahidi wa mwanamke ungekuwa unakataliwa tu kwa sababu mwanamke ni kiumbe dhalili basi Hadith zilizopokewa kutoka kwa wanawake zingekataliwa. Lakini Hadith zilizopokewa kutoka kwa Bibi Aisha kwa mfano ni sehemu ya msingi wa sheria yenyewe. Ni upi ushahidi mzito zaidi, wa kupokea Hadith au wa kuandikishiana mikataba ya pesa? Yote hayo yanaonesha kuwa lengo ni kuhifadhi haki za watu zisipotee kwa sababu ya kughafilika na siyo kumdunisha mwanamke.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 493
Sponsored links
👉1
kitabu cha Simulizi
👉2
Kitabu cha Afya
👉3
Simulizi za Hadithi Audio
👉4
Kitau cha Fiqh
👉5
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6
Madrasa kiganjani
Sanda ya mwanaume na namna ya kumkafini
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Shahada nguzo ya kwanza ya uislamu, sifa zake na umuhimu wake.
Soma Zaidi...
Jinsi ya kujitwaharisha Najisi hafifu na najisi ndogo
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi hafifu na najisi ndogo. Soma Zaidi...
Maana ya Ndoa na Faida zake katika jamii
4. Soma Zaidi...
Mambo yanayoharibu swala yaani yanayobatilisha swala.
Post hii itakufundisha mambo ambayo yatasababisha swqla yako isikubaliwe. Soma Zaidi...
darsa nzuri zenye kuelimisha hasa katika ndoa ya kiislam.
Assalaam alykum warahmatullah wabarakatuh. Soma Zaidi...
Ni zipi Nguzo za Udhu au Kutawadha
Soma Zaidi...
Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa Soma Zaidi...
Ufumbuzi wa tatizo la riba.
Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba. Soma Zaidi...
Aina za talaka zinazo rejewa
Soma Zaidi...