Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu.
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti
(i) Dhana ya mafanikio
Katika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu.Mafanikio hayapimwi kwa mali. Katika uchumi wa Kitwaghuti mafanikio maana yake ni mafanikio ya kiuchumi. Ni kiasi gani cha mali mtu amefanikiwa ku kip ata .J ins i atakavyojilimb ikizia mali n divyo itakavyoonesha “mafanikio” yake. Katika Uislamu kufuzu kwa kweli ni kupata radhi za Mwenyezi Mungu na kufeli kukubwa ni kule kukosa radhi hizo. Hivyo ili binaadamu afanikiwe hana budi kuishi kwa uadilifu.
Mtazamo huu unaathiri pia mizani yake ya wakati. Muislamu anapozitumia rasilimali zilizomo katika ardhi hafikirii tu mahitaji yake ya binafsi ya sasa bali pia matokeo ya vitendo vyake kwa vizazi vijavyo.
Kwa mtazamo huu mtu anakuwa hana haki ya kufuja mali au rasilimali za ardhi, kwa vile anazingatia maslahi yake katika maisha haya, huko akhera na maslahi ya viazazi vijavyo. Mafanikio katika Uislamu ni kule kulijua lengo la maisha hapa ulimwenguni, kuwa na kumbukizi ya kisimamo mbele ya Mola siku ya hesabu, kukinai moyoni na kuona kila kitu cha ulimwengu huu kuwa ni cha kawaida. Kujitahidi kuyaendea mambo mema bila ya kuchelea chochote na kujiepusha na yale yote yanayoweza kumtoa mtu au kumkhasirisha katika maisha yajayo hata kama yana “manufaa” kwa mtazamo wa wengi katika maisha haya. Kujali shida na matatizo ya wengine na kuweza kutoa kwa ajili ya kuwasaidia wengine kwa kadiri ya wasaa uliopo.
Kuwa na huruma, mapenzi na bashasha isiyobagua taifa, kabila, nasabu wala ukoo wa mtu. Kutokuwa na chuki, majivuno, kibri, utesi, usengenyi, ulimbukeni, kujiona, kujitukuza au kujidhalilisha na kujitweza kwa yeyote yule anayemulikwa na jua iwe kihali au kimali. Aliyetajiri wa Nafsi ni yule ambaye fursa yoyote aliyonayo haiwi kero na huzuni kwa wengine bali huitumia mwisho wa uwezo wake kupambana na taratibu potofu na kandamizi zinazotawala jamii yake. Hii ndiyo Dhana ya mafanikio katika Uislamu.
(ii) Dhana ya umilikaji mali
Katika Uislamu mmiliki wa hakika wa mali ni Mwenyezi Mungu, mwanaadamu kama Khalifa wa Allah hapa duniani anamiliki mali kwa dhamana tu siyo kwa hakika na kwa sababu hiyo ataulizwa jinsi alivyotumia hiyo mali.
Pamoja na hivyo mali katika Uislamu si kitu kiovu bali kinachosisitizwa ni kuwa ichumwe na kutumiwa kwa kuzingatia maelekezo ya Mwenyezi Mungu.
Kuhusu kutafuta mali Qur-an inatueleza kama ifuatavyo: “Na utafute – kwa yale aliyokupa Mwenyezi Mungu makazi mazuri ya akhera wala usisahau sehemu yako ya dunia”. (28:77)
(iii)Dhana ya bidhaa
Katika uchumi wa kitwaghuti kitu chochote chaweza kuwa ni bidhaa maadamu kinaweza kutumiwa na mtu. Kwa mfano pombe pamoja na madhara yake huitwa bidhaa kwa kuwa hutumiwa na baadhi ya watu.
Katika uchumi wa Kiislamu “bidhaa” huitwa ama “Atwayyibaati” au “Rizk”. Atwayyibaat ni kitu kizuri, safi, Twahara. Rizk ni neema, au hidaya itokayo kwa Allah (s.w). Hivyo katika uchumi wa Kiislamu bidhaa ni vile vitu halali tu kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Kisichokuwa halali si bidhaa. Kwa mfano pombe ni haramu hivyo si bidhaa.
(iv)Dhana ya Matumizi
Kwa kuwa Allah ndiye Muumba wa watu na rasilimali zote katika ulimwengu, sera ya uchumi wa Kiislamu haimpi mtu fursa ya kufuja mali apendayo pamoja na uhalali atakaokuwa nao katika dhamana ya milki ya mali hiyo. Kinyume chake, katika uchumi wa Kitwaghuti mtu anayo fursa ya kufuja mali apendavyo maadam ni mmiliki wa mali hiyo.
(v) Mizani ya wakati katika tabia ya mtumiaji
Mtu anapofanya maamuzi yoyote hujiuliza nini matokeo au matazamio ya kitendo hiki au uamuzi huu baada ya saa moja au wiki moja au mwezi mmoja au mwaka mmoja au miaka mitano au kumi n.k. Kipimo cha wakati katika uchumi wa Kitwaghuti na ule wa Kiislamu ni tofauti. Katika ujahili mtu hujiuliza mali kiasi gani awe amepata atakapofikia umri fulani, kinyume chake Muislamu anapofikiria jambo lolote, pamoja na masuala ya uchumi, kipimo chake cha wakati hukipa upeo mpana sana. Hujiuliza, je hiki kitendo ninachofanya kitakuwa na matokeo gani siyo tu kwa wiki hii au mwezi huu au mwaka huu au ujao bali kina matokeo gani siku ya kiyama.
Muislamu anaamini kuwa ipo siku ya malipo na kwamba kuna pepo na moto. Watu watahesabiwa na kulipwa kwa mujibu wa matendo yao. Kila mtu binafsi atasimamishwa peke yake mbele ya Mwenyezi Mungu na kupewa hisabu yake. Imani hii ina athari kubwa kwa Muislamu na maamuzi yake anayochukuwa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 718
Sponsored links
👉1
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2
Kitau cha Fiqh
👉3
kitabu cha Simulizi
👉4
Simulizi za Hadithi Audio
👉5
Kitabu cha Afya
👉6
Madrasa kiganjani
Nini maana ya ndoa katia uislamu na ni upi umuhimu wake
Hapa utajifunza maana ya ndoa kulingana na uislamu na umuhimu wake katika jamiii Soma Zaidi...
Waislamu wanaolazimika kufunga
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kusimamisha Swala
Kusimamisha Swala. Soma Zaidi...
Namna ya kutayamamu hatuwa kwa hatuwa
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi yavkutayamamu. Soma Zaidi...
Jinsi ya kuelekea qibla katika swala.
Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla. Soma Zaidi...
Mgawanyo na matumizi ya mali katika uislamu
6. Soma Zaidi...
haki za mwanamke za kisiasa katika uislamu
Haki ya Kushiriki Katika Siasa. Soma Zaidi...
IBADA YA HIJA NA NAMNA YA KUITEKELEZA
Soma Zaidi...
Sifa za uchumi wa kiislamu na njia halali za uchumi na umiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...
NI LIPI HASA LENGO LA KUFARADHISHWA SWALA ZA FARADHI NA KUWEPO KWA SWALA ZA SUNNAH (SUNA)
Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Soma Zaidi...