picha

Zijuwe hatuwa za ukuwaji wa ujauzito na dalili za ujauzito katika miezi mitatu, miezi sita na miezi tisa

Zijuwe hatuwa za ukuwaji wa ujauzito na dalili za ujauzito katika miezi mitatu, miezi sita na miezi tisa



HATUA ZA UKUWAJI WA MIMBA NA DALILI ZAKE




Ujauzito umegawanyika katika hatua kuu tatu, au vipindi vikuu vitatu ambavyoni:-
1.trimester ya kwanza (first trimester)
Hiki ni kipindi katia ya wiki 1 mpaka 12 yaani ndani ya miezi mitatu ya kwanza. Kipindi hiki mjamzito awe makini sana kwani ni kipindi ambacho kutoka kwa ujauzito ni rahisi sana. Kipindi hiki ndicho ambacho mtoto anaanza kukuwa ubongo, uti wa mgongo na viungo vingine ama moyo na masikio. Tafiti zinaonyesha kuwa takribani asilimia 85 ya mimba zinazotoka huwa zinatoka katika kipindi hiki. Hata hivyo wanaotowa mimba pia hutoa katika kipindi hiki.



Mabadiliko ya mwili katika kipindi hiki
A.Uchovu
B.Kukosa haja kubwa
C.Kichefuchefu
D.Maumivu ya kichwa



Nini hakitakiwi kufanyika katika kipindi hiki?
A.Wacha kuvuta sigara
B.Wacha kunywa pombe
C.Wacha kutumia dawa kiholela bila ya ushauri wa daktari
D.Kuwa makini sana kwani kosaadogo ujauzito upo hatarini
E.Punguza kuchwa chai kupitiliza
F.Punguza kula samaki kwenye magobeta jaamii ya tondo




2.Trimester ya pili (second trimester)
Kipindi hiki ni kati ya wiki 13 mpaka 27 yaani kuanzia mwezi wa 3 mpaka wa 6 kwenda wa saba. Katika kipindi hiki mwanamke atafanyiwa vipimo vya utrasound kuangalia mkao wa mtoto na kama yupo katika afya njema. Katika kipindi hiki hata jinsia ya mtoto itaweza uonekana kwa ambaye anataka kuiona kwenye kipimo cha utrasound. Hapa mtoto anaweza kuishi nje ya mwili wa mama yake kuanzia wiki ya 23. na endapo mtoto atazaliwa hapa atakuwa njiti hivyo vifaa maalumu vitahitajika kumlea kabla ya kuanza kuishi huru. Katika kipindi hiki mama mjamzito atasikia vurugu za mtoto tumboni, kupiga mateke, kugeuka na nyinginezo.



Katika kipindi hiki karibia dalili zote za ujauzito za mwanzo hupotea. Nguvu itarudi vyema na utawza kulala usingizi mnono usiku. Katika kipindi hki tumbo litaanza kuonekana kukuwa. Katika kipindi hiki jiepushe sana yafuatayo:-
A.Kuvaa nguo za kubana
B.Kuwa na hasira mara kwamara. Yaani jitahidi kkutafuta furaha, kaa na maafiki cheka na furahia.
C.Usikibane tumbo hata likiwa kubwa vipi.



Katika kipindi hiki unawezakuhisi kuingulia mra kwa mara, na maumivu ya miguu. Hamu ya kula inawea kuongezeka, na uzito pia kuongezeka katika kipindi hiki. Katika kipindi hiki mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya mgongo. Hata hivyo anaweza kujihisi kama ana mafua ama pua zimeziba ila akifina hakuna kitu. Pia anaweza kuiona mishipa inatokeza kwa nje hasa kwenye miguu.



Katika kipindi hiki mama mjamzito ataanza kusikia mijongeo ya mtoto. Hata hivyo mtoto ataweza kuitambuwa sauti ya mama yake na watu wa karibu sana na mama yake. Baadhi ya viungo vinavyoweza kuonekana kwenye utrasound katika kipindi hiki ni kama figo, mapafu, moyo na ubongo na jinsia. Katika kipindi hiki mama mjamzito anaweza kupimwa kisukari cha mimba kuanzia wiki ya 26 mpaka 28.





3.Trimester ya tatu (third trimester)
Kipindi hiki huanzia wiki ya 28 mpaka 40, yaani kuanzia miezi 7 kwa makadirio. Katika kipindi hiki mara kwa mara utahitajika kumuona daktari kwa vipimo zaidi. Daktari atakuwa anakuangalia maendeleo yako kwa jumla na afya ya ujauzito wako. Atakuwa anakucheki:-
A.Anapima mkojo kuangalia protini
B.Atakuwa analkuangalia shinikizo la damu (presha)
C.Atasikiliza mapigo ya moyo wa mtoto
D.Atakuwa akipima njia ya uzaziatakuwa acheki miguu na mikono kama itakuwa inavimba.



Pia daktari anaweza kukupima uwepo wa bakteria wanaoitwa Group B streptococcus (GBS) kwenye uke. Uwepo wa bakteria hawa unaweza kuhatarisha afya ya mtoto anayezaliwa. Katika kipindi hiki ni vyema kuanza kufuatilia habari za kujifungua, mazoezi ya kujifungua na namna ya kujiandaa.



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 5136

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji

Post hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya shida ya upumuaji, ni madhara madogo madogo ambayo utokea kwa watumiaji wa matatizo ya kupumua.

Soma Zaidi...
Zijue Athari za kuweka vitu ukeni.

Posti hii inahusu zaidi athari za kuweka vitu ukeni, tunajua kwa wakati huu kadri ya kukua kwa sayansi na teknolojia watu wanaendelea kugundua mbinu mbalimbali ili waweze kuwafurahisha wapenzi wao wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo kabla ya kupata hedhi

Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba.

Soma Zaidi...
Ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango.

Posti hii inahusu zaidi ukweli kuhusu njia za uzazi wa mpango, sio kwa imani potofu ambazo Watu utumia kuelezea uzazi wa mpango.

Soma Zaidi...
Huduma kwa wanaopata hedhi zaidi ya mara moja kwa mwezi

Posti hii inahusu zaidi huduma kwa wanaoingia kwenye siku zao zaidi ya mara moja kwa mwezi.

Soma Zaidi...
Huduma kwa mama ambaye mimba imetoka moja kwa moja.

Post hii inahusu zaidi huduma kwa mama ambaye mimba imetoka moja kwa moja, aina hiyo ya mimba kwa kitaalamu huitwa complete abortion.

Soma Zaidi...
Ni zipi njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume

Somo hili linakwenda kukuletea njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume

Soma Zaidi...
Mtoto anaanz kucheza kwa mda gan

Kuna watoto wengine huanza kucheza mapema kuliko watoto wengine. Tunapozungumzia kucheza kwa mtoto aliye tumboni yaani mimba hapa inatubidi tuangalie kwa undani zaidi, je ni muda gani mtoto ataanza kucheza?

Soma Zaidi...
je mwana mke ana weza kubeba mimba kama hayupo kwenye siku zake za hatali ama

Mimba haipatikani kila siku, na pia mimba huingia kwa siku moja na katika muda mmoja. Baada ya mimba kutungwa hakuna tena nafasi ya kutungwa mimba nyingine.

Soma Zaidi...