zijuwe faida za kula njegere kiafya na umuhimu wa kula jegere pia jifunze njegere zina kazi gani mwilini?
Njegere ni katika mboga jamii ya kunde. Njegere ni katika mboga tamu kama hujawahi jaribu kuila, tafuta siku ujaribu. Lakini mboga hii ukiacha mbali na utamu wake njegere zimekuwa zikitajwa sana katika njanja za afya. Hivi unazijuwa faida za kula njegere?. hakika ni nyingi sana faida za njegere kiafya, kimwili na hata kwa utamu. Makala hii inakwenda kukuletea faida za kiafya za kula njegere.
Faida za kula njegere
1.Njegere zina virutubisho vingi sana ukilinganisha na mboga nyingi. Njegere zina vitamini A, vitamin K, Vitamini B na Vitamini C. pia njegere zina madini ya chuma, manganense, phosphorus, na folate. Pia negere zina protini na kamakamba. Katika mboga njegere ni katika mboka iliyokusanta protini kwa wingi sana.
2.Husaidia katika kudhibiti kiwango cha sukari mwilini. Yaani husaidia katika kudhibiti matumizi ya sukari ndani ya mwili wako. Husaidia kuwapa nafuu watu wenye isukari type 2 diabetes. Hali hii husaidia katika kuboresha afya ya moyo.
3.Njegere husaidia katika kuboresha afya ya mfumo wa mmengβenyo wa chakula. Kama unasumbuliwa na kukosa haja kubwa basi njegere ndio mtatuzi wako. Njegere husaidia katika kuondoa vimbe zilizopo kwenye njia ya chakula na kufanya choo kiwe kizito na rahisi kupita kwa urahisi. Njegere husaidia katika kuzuia saratani ya utumbo mkubwa na kusaidia katika kuondosha chakula chote kupitia haja.
4.Njegere huliunda mwili dhidi ya maradhi hatari kama saratani, maradhi ya moyo na kisukari. Kwa sifa hii njegere ni mboga pekee ambayo unatakiwa uile mara nyingi sana kwa lengo la kujikinga na maradhi haya. Hata hivyo kwa ambaye ni mgonjwa tayari mboga hii itamsaidia kupunguza uzito wa tatizo.
A.Husaidia kuzuia maradhi ya moyo: njegere zina madini ya magnesium, potassium na calcium. Ulaji wa chakula chenye madini haya kwa wingi husaidia katika kuzuia shinikizo la juu la damu (presha ya kupanda) ambayo ndio chanzo kikuu cha maradhi ya moyo. Pia ndani ya njegere kula flavonols, carotenoids na vitamini C. wa pamoja husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa sababu huzuia uharibifu wa seli.
B.Husaidia kuzuia saratani: njegere zina uwezo wa kuzuia uotaji wa vimbe ndani ya mwili ambazo ndio mizizi ya saratani. Pia ndani ya njegere kuna saponin nichembechembe inayojulikana kama kipingamizi cha saratani. Hata hivyo vitamini K ndani ya njegere vinatambulika vyema kuwa na msaada mkubwa katika kuzuia aina mbalimbali za saratani.
C.Nyuzinyuzi na protini katika njegere husaidia sana katika kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu, na matumizi ya sukari mwilini.pia vitamini B, K, A, C na madini ndani ya ngegere husaidi katika kulinda mwili dhidi ya kisukari.
5.Njegere husaidia katika kuboresha afya ya mifupa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kupambana na saratani
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa faida kuu 5 za kula karanga mbichi katika afya ya mwili wako.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za mchaichai/lemongrass
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukupa elimu juu ya vyakula na vinywaji vilivyo salama kwa mtu mwenye kisukari, na ni vyakula vipi ni hatari kwa mwenye kisukari. Pia utajifunza njia za kujilinda na kupata kisukari.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa maziwa
Soma Zaidi...