Mambo ya kuangalia kwa mtu aliyepoteza fahamu
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtu aliyepoteza fahamu, kama mtu amepoteza fahamu Kuna mambo muhimu yanapaswa kuangaliwa kwa makini kama ifuayavyo.
Mambo ya kuangalia kwa aliyepoteza fahamu.
1. Kwanza kuangalia kama mgonjwa anapumua.
Kitu Cha kwanza kuangalia kama mtu amepoteza fahamu ni kuangalia kama mgonjwa anapumua, kama hapumui unaangalia mdomoni kama Kuna kitu labda kimeziba mdomoni pia angalia puani labda Kuna michanga imeziba hasa kwa waliopata ajali, ukikuta Kuna kitu chochote unapaswa kukitoa Ila uwe mwangalifu unapotoa vitu mdomoni usije ukavisukuma kwenye mfumo wa hewa, kwa hiyo hakikisha mgonjwa wako anapumua ndipo uendelee na mambo mengine.
2. Kuangalia kiwango Cha damu kinachotoka , kwa hiyo mgonjwa kama anatokwa na damu nyingi zinapaswa kuzuia kwa kufunga sehemu ambapo damu zinatokea, kama damu zinaendelea kutoka mgonjwa anapaswa kumpelekwa hospitalini haraka ipasavyo Ili kuongeza kiwango Cha damu. Kama ni kidogo mgonjwa anaweza akafungwa na huduma nyingine zinaweza kuendelea.
3. Kuangalia chanzo Cha kupoteza fahamu.
Baada ya kufanya hayo yote tunapaswa kujua chanzo Cha kupoteza fahamu ni nini? Kama ni mshutuko wa Moyo au kama ni kushuka kwa sukari au kama ni tatizo la moyo na mambo mengine ambayo usababisha kupoteza fahamu, ukisha tambua chanzo Cha kupoteza fahamu unaanzia kutibu kadri ya chanzo, mfano kama ni kushuka kwa sukari mpe mgonjwa vitu vya sukari au kama ni kuishiwa maji mwilini mgonjwa anapaswa kuongezewa maji na mengineyo.
4. Kama unaona hali ya mgonjwa haiwezekani kutibiwa kwa kutumia huduma ya kwanza mpeleke mgonjwa haraka sana hospitalini Ili aweze kupatiwa matibabu zaidi.kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa ugonjwa wa kupoteza fahamu upo na sababu nyingine zinaweza kutibiwa kwa kutumia huduma ya kwanza lakini hali ya mgonjwa isipobadilika mgonjwa anapaswa kumpelekwa hospitalini haraka Ili apatiwe matibabu zaidi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 web hosting 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Mabadiliko yanayotokea wakati wa kubarehe kwa wsichana
Post hii inahusu zaidi mabadiliko katika umri wa kubarehe kwa wsichana, ni kipindi ambacho watoto huelekea ujana, utokea Kati ya miaka kuanzia Kumi na kuendelea.
Soma Zaidi...Zijue faida za mate mdomoni
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa mate mdomoni, mate ni majimaji ambayo hukaa mdomoni na husaidia katika kazi mbalimbali mdomoni.
Soma Zaidi...Njia za kujikinga na vidonda vya tumbo
Kama unahitaji kujuwa namna ya kuweza kujikinga na vidonda vya tumbo, basi makala hii ni kwa ajili yako. Hapa utaweza kuzijuwa hatuwa zote za kujikinga na kupata vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na kwikwi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na kwikwi
Soma Zaidi...Umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu
Post hii inahusu zaidi umuhimu wa pua kama mojawapo ya mlango wa fahamu.pua ni mlango wa fahamu ambao uhusika na kupumua.
Soma Zaidi...