Namna ya kumsaidia mtoto mwenye degedege

Namna ya kumsaidia mtoto mwenye degedege

Degedege ni ugonjwa unaoshambulia sana watoto chini ya miaka mitano,na uwaletea matatizo mengi pamoja na kuwepo kwa ulemavu na vifo vingi vinavyosababishwa na ugonjwa huu.

Zifuatazo ni njia za kumsaidia mtoto kama amepatwa na degedege,

1. Mlaze mtoto kwenye sehemu ambayo itazuia kungata ulimi, kwa sababu mtoto akiachwa na degedege atasikia maumivu  kwenye ulimi na anaweza kushindwa kunyonya au kula

 

2. Kama Kuna makohozi yoyote yanayombana kifuani au kohoni inabidi yatolewe kwa sababu yanaweza kuingia kwenye mfumo wa hewa na kuleta matatizo mengine

 

3.mpatie mtoto dawa ambazo zinahitajika kwa ajili ya kuzuia degedege, dawa hizi ziwe zimeagizwa na daktari hizo dawa zipo hospitalini na uponyesha ugonjwa huu.

 

4. Hakikisha kwamba kiasi Cha sukari kwenye mwili ni Cha kawaida, kama sukari haiko kwenye kiwango chake jaribu kufanya iwe kwenye kiwango na pia angalia kiasi Cha madini kwenye mwili

 

5. Angalia kama joto la mwili liko kawaida, kama  haliko kawaida mpatie dawa za kushusha joto la mwili, angalia pia msukumo wa damu, pia upumuaji,mapigo ya moyo yanaendaje, hakikisha kila kitu kwenye mwili Kiko kawaida

 

6. Hakikisha mtoto Yuko sehemu nzuri ambayo hawezi kuanguka na hakikisha mtoto anaangaliwa mda wote Ili kuepuka madhara mbalimbali yanayoweza kutokea wakati anahudumiwa

 

7. Endelea kuangalia chanzo Cha degedege kama ni maambukizi kutokana na magonjwa nyemelezi au ni bakteria au ni virusi, kama ni ugonjwa wowote inabidi kutibiwa mara Moja.

Angalisho kama mtoto bado ana degedege usimpe kitu chochote Cha kula kwa kupitia mdomoni maana chakula kinaweza kuingia kwenye mfumo wa hewa.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views: 4846

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Roghage/ vyakula vya kambakamba

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya roghage

Soma Zaidi...
Je unaweza ukapona macho kama huoni vizuri kwa sababu ya vitamini A,

Jiamini A ni katika vitamini inayojulikana sana kuboresha na kuimarisha afya vya macho na uoni. Tafiti zinaonyesha kuwa kuna kundi kubwa la watoto wanaopata tayizobla kutokuona kutokana na ukosefu wa vitamini A vya kutosha.

Soma Zaidi...
Vipi kuhusu kibofu kukaza sana na unapokula unahisi kama tumbo kujaa zaidi je hii nidall yamimba?

Dalili za mimba zinaweza kuwa tata sana kuzijua mpaka upate vipimo. Kwa mfano unaweza kupatwa na maumivu yakibofu. Je unadhani nayo ni dalili ya mimba?

Soma Zaidi...
Aina za kuungua

Post hii inahusu Aina za kuungua, kuungua ni Hali ya kubabuka kwa ngozi ya mwili na kusababisha madhara mbalimbali

Soma Zaidi...
Malengo ya kutibu ukoma

Posti hii inahusu zaidi malengo ya kutibu ukoma, ni malengo ambayo yamewekwa na wizara ya afya ili kuweza kutokomeza ukoma kwenye jamii

Soma Zaidi...
Haya hayawezi kuambukiza UKIMWI

Somo hili linakwenda kukuletea Mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI

Soma Zaidi...