Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEUNGUA
Kuungua kupo kwa aina nyingi. Mtu anaweza kuungua kwa umeme, moto wa kuni, moto wa gesi ama mvuke unaotoka kwenye mashine kama bomba la pikipiki. Pia mtu anaweza kuungua kutokana na miripuko kama baruti. Pia mtu anaweza kuunguwa kwa kemikali. Namna zote hizi zina utoaji huduma wake. Hapa nitaelezea kwa ufupi kuungua kwa moto.
Mtu anapoungua na moto angalia kwanza ni kwa kiasi gani ameungua. Kama ameungua sana ama eneo kubwa ni vyema kuwahi kutoa taarifa kituo cha afya kilicho karibu, ama kumuwahisha mgonjwa. Pia kuwa makini sana kama ameungua usoni, kwenye makalio ama miguu ama mikono au sehemu za siri.
Kama ameungua kawaida unaweza kumpatia huduma ya kwanza kisha uaendelea kumuangalia mgonjwa kama itahitajika kumpeleka kituo cha afya. Mtu aliyeungua unaweza kumpatia huduma ya kwanza kwa njia zifuatazo:
1.mwagilizia maji kwa muendelezo kwenye jeraha kwa muda wa dakika 15. ikishindikana kufanya hivi
2.Pepea sehemu yenye jeraha, ila usitumie barafu kwani linaweza kusababisha athari zaidi.
3.Unaweza kumpa mgonjwa dawa za maumivu kupunguza maumivu
4.Safisha jeraha kwa kimiminika cha iodine, ama aloevera gel. Na katu usimpake mafuta ya aina yeyote.
5.Unaweza kumpaka asali kwenye jeraha
6.ili kulinda jeraha dhidi ya kuvamiwa na bakteria mpake mmgonjwa kimiminika cha antibiotic
7.Lizibe jeraha kwa kulifunga na bendeji ama kitambaa kilicho safi na hakikisha hukazi sana wakati wa kufunga.
8.Angalia hali ya mgonjwa kisha umpeleke kituo cha afya kilicho karibu kwa uangalizi zaidi
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo yanayoweza kuadhiri Uponyaji wa jeraha.jeraha huleta maumivu makali sana, vilevile Uvimbe, kutoa usaha. Pia jeraha hutofautiana katika kupona kwa mtu mzima na Mtoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi matokeo ya maambukizi kwenye milija na ovari, ni matokeo apatayo mtu mwenye maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kuharisha hii ni chanjo wanayopewa watoto wadogo chini ya miaka mitano kwa lengo la kuzuia kuharisha chanjo hiyo kwa kitaalamu huitwa Rotarix.
Soma Zaidi...Huduma ya kwanza ni huduma anayopewa mgonjwa au mtu yeyote aliyepata ajali kabla ya kumpeleka hospitalini
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi huduma Kwa mgonjwa mwenye maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo,ni huduma maalumu ya kumsaidia mgonjwa aliyepata maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sehemu ambazo zinapaswa kudungwa chanjo, hizi ni sehemu zile zilizopendekezwa kwa ajili ya kuchoma chanjo kwa kadiri ya kazi ya chanjo.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujilinda dhidi ya mapunye
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo mbalimbali ambayo husababisha kizunguzungu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kujikinga na kisukari
Soma Zaidi...