Namna ya kurithisgha hatuwa kwa hatuwa.

Hspa utajifunza sasa jinsi ya kugawa mirathi kutokana na viwango maalumu.

Ugawaji wa mirathi
-Mume ana nusu (1/2) = 1/2
-Mama ana sudusi. (1/6) = 1/6
-Ndugu wengine wa kwa mama wana thuluthi (1/3) = 2/6

 


Hapo utaona kuwa mafungu yote sita yamegawanywa yakaisha na ndugu wa kwa baba na mama hawakupata kitu. Hapa itabidi ile Thuluthi waliyoipata ndugu wa kwa mama wagawane sawa sawa na ndugu wa kwa baba na mama maana nao wanayo haki ya ndugu wa kwa mama kama wao na wala hakoseshwi kwa sababu ya unasaba wake.

 

Mifano ya namna ya kurithisha
Wakikutana warithi na pakawa hapana amzuiliaye mwenziwe na ikawa wote ni asaba, wataigawanya mali iliyopo sawa sawa kwa kadri ya idadi yao. Kwa mfano: Akifa mtu, akawa ameacha vijana wanamume wanne, mali yote itagawanywa mafungu manne sawa sawa na kila mmoja apewe fungu lake.

 


Ama wakikutana asaba wanaume na wanawake, bali kila mwanamume atahesabiwa kuwa ni wanawake wawili na mali itapigwa mafungu kila mwanamume mmoja apewe mafungu mawili na kila mwanamke apewe fungu moja. Kwa mfano: Amekufa mtu kaacha watoto sita, wanne wanaume na wawili wanawake. Wanaume wanne watahesabiwa kuwa ni sawa na wanawake wanane. Kwa hiyo mali itagawanywa katika mafungu kumi yaliyo sawa sawa. Wanaume watapata mafungu mawili kila mmoja na wanawake watapata fungu moja moja.

 


Iwapo warithi ni mchanganyiko wa wenye mafungu maalum na asaba, itabidi kutafuta kigawe kidogo cha shirika (Kigawe kidogo cha shirika - KDS) ili kupata mafungu yatakayogawiwa kwa kila mrithi kwa kadiri ya haki yake anayoistahiki. Hebu tuangalie mifano kadhaa ya mgawanyo wa mirathi.

 


Mfanol:
Amekufa mke na kuacha
(i)Mume.
(ii)Mtoto mwanamume.
(iii)Baba.

 


Wenye mafungu maalum kati ya hawa ni: (i)Mume - ana robo (1/4) madhali yupo mtoto.
(ii)Baba - ana sudusi(1/6) madhali yupo mtoto.

 


Asaba: Mtoto mwanamume na atachukua kitakachobakia. Ugawaj i:
Mafungu yatakayotolewa ni: (1/4), (1/6). Hesabu ndogo ambayo
inaweza kutolewa mafungu ya urithi ni 12 yaani KDS ya 4 na 6. Kwa hiyo mali ya urithi itagawanywa kwenye mafungu 12 yaliyo sawa sawa na ugawaji utakuwa kama ifuatavyo:

 


(i)Mume atapata 1/4 ya 12 = 114x 12 = 3 Yaani atachukua mafungu 3 katika mafungu 12.
(ii)Baba atapata (1/6) ya 12 = (1/6) x 12 = 2. Yaani atachukua mafungu 2 kati ya mafungu 12.

 


Mfano 2:
Amekufa mume na kuacha wafuatao:
(i)Mke mmoja.
(ii)Mama.
(iii)Mjukuu mmoja wa kike (binti wa mtoto mwanamume).
(iv)Mtoto mwanamume.
(v)Watoto watatu wanawake.

 


Kama mali iliyoachwa na marehemu ni shilingi 1,200,000/= utarithisha wahusika kama ifuatavyo:
Wenye mafungu maalum kati ya hawa ni:
(i)Mke ambaye atapata thumuni 1/8 kwa sababu wapo watoto.
(ii)Mama atapata sudusi 1/6 ya mali kwa sababu wapo watoto.
(iii)Mjukuu hapati kitu kwa sababu wapo watoto ambao humzuilia.

 

(iv)Mtoto mwanamume na watoto wanawakewatagawana mali iliyobakia, wakiwa hao asaba mwanamume achukue sawa na
wanawake wawili (2:1)

 


Njia mbili zifuatazo zinaweza kutumika katika kurithisha wahusika: (a) Hisabu ndogo inayoweza kutolewa mafungu ni 24. Yaani KDS
ya 8 na 6. Kila fungu litakuwa na thamani ya shilingi 50,000 -(1,200,000/24)
Mke atapata 1/8 ya 24 = 3 yaani atapata 3 x 50,000/=
Mama atapata 1/6 ya 24 (1 x 24) = 4 yaani atapata 4 x 50,000 = 200,000/=
Asaba watarithi mali iliyobakia ambayo ni 1,200,000 - (150,000 ~ 200,000) = 850,000.

 

Mali hii itagawanywa katika mafungu 5 (kumbuka: Mwanamume atapata sawa na wanawake wawili). Hivyo, kila mtoto wa kike atapata: Shs. 1/5 x 850,000 = 170,000
Mtoto wa kiume atapata shs. 2/5 x 850,000 (au 2 x 170,000) = 340,000

 


(b)Njia ya pili ni kutafuta sehemu ya mali atakayopata kila mwenye fungu maalum. Kama mali inayorithiwa ni shs. 1,200,000/=
(i)Mke atapata 1/8 ya 1,200,000 = I X 1200000/8 = 150,000/=
(ii)Mama atapata 1/6 ya 1,200,000 = I X 1,200,000/6 = 200,000/
(iii)Asaba watagawana mali iliyobakia ambayo ni 1,200,000 - 350,000 = 850,000.
Kuna mabinti watatu na kijana mmoja ambaye ni sawa na mabinti wawili. Hivyo mali iliyobakia itagawanywa katika mafungu 5 ambapo kila binti atapata: I X 850,000/5 = 170,000/=
Kijana atapata sawa na mabinti wawili sh. 2 x 170,000 = 340,000/=

 


Kuongeza mafungu (Awl)
Iwapo idadi ya mafungu yatakayogaiwa kwa warithi wenye mafungu maalum ni kubwa kuliko mafungu yaliyopatikana kwa njia ya (KDS), idadi ya mafungu itabidi iongezeke ili kila mmoja apate haki yake. Hebu tuangalie mifano ifuatayo:

 


Mfano 1:
Amefariki mke na kuacha warithi wafuatao:
(i)Mume.
(ii)Dada wawili wa kwa baba na mama.
Wote hawa wana mafungu maalum:
(i)Mume atapata (1/2) kwa sababu hapana mtoto.
(ii)Dada wawili watapata thuluthi mbili (2/3) kwa sababu wako zaidi ya mmoja.
KDS ya 2 na 3 ni 6, hivyo:
(i) Mume atapata nusu (1/2) ya mafungu 6 = 3.

 

(ii) Dada wawili watapata thuluthi mbili (2/3) ya mafungu 6 = 4.
Utakuta kuwa jumla ya mafungu yanayohitajika ni 7(3 + 4) badala ya 6.
Hivyo mali ya marehemu itagawanywa katika mafungu yaliyo sawa sawa. Katika hayo mume atapata mafungu 3 na kila dada atapata mafungu 2.

 


Mfano 2:
Amefariki mke na kuacha warithi wafuatao:
(i)Mume.
(ii)Mama.
(iii)Dada mmoja wa kwa baba na mama.
Wote hawa wana mafungu maalum:
(i)Mume atachukua (1/2) kwa sababu hapana mtoto.
(ii)Mama atachukua (1/3) kwa sababu hapana mtoto na dada aliyopo ni mmoja tu.
(iii)Dada atapata (1/2) yuko peke yake.

 


Mgawanyo:
KDS ya 2 na 3 ni 6.
(i)Mume atapata (1/2) ya mafungu 6 = mafungu 3.
(ii)Mama atapata (1/3) ya mafungu 6 = mafungu 2.
(iii)Dada atapata (1/2) ya mafungu 6 = mafungu 3
Jumla ya mafungu yanayohitajika ni 8, badala ya 6. Hivyo itabidi mafungu mawili yaongezwe kwenye (KDS) ili kila mrithi apate haki yake.
Sehemu ya maskini na jamaa wa karibu katika mirathi:

 


Waumini wana usiwa kuwa japo ni wazi kuwa mali ya urithi ni haki ya warithi kwa mujibu wa sheria, hawana budi kuwahurumia mayatima, maskini na jamaa wa karibu kwa kuwapa kitu kutokana na urithi japo kidogo na hasa watakapohudhuria wakati wa kugawanya.

 

Na wakati wa kugawanya wakihudhuriajamaa na mayatima na maskini, wapeni kitu katika hayo (mali ya urithi) na waambieni kauli njema. (4:8)

 

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/08/16/Tuesday - 10:08:48 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 641

Post zifazofanana:-

Warithi wasio na mafungu maalumu katika uislamu
Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi. Soma Zaidi...

Jinsi ambavyo mtu anazuiliwa kurithi mali ya marehemu
Endapo mtu yupp katika orodha ya wanaotakiwa kutithi, anaweza kuzuiliwa kurithi kwa kuzingatia haya. Soma Zaidi...

Mgawanyo wa mirathi kutoka kwenye Quran
Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo. Soma Zaidi...

Namna ya kurithisgha hatuwa kwa hatuwa.
Hspa utajifunza sasa jinsi ya kugawa mirathi kutokana na viwango maalumu. Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi
Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu. Soma Zaidi...

Maana ya mirathi katika uislamu
Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake. Soma Zaidi...

Mafungu ya urithi katika uislamu
Hspa utajifunza viwango maalumu vya kutithi mirathi ys kiislamu. Soma Zaidi...

Hawa ndio wanaoruhusiwa kurithi
Hii ni orodha ya watu ambao wanaweza kurithi malibya marehrmu. Soma Zaidi...