picha

Haya ndio yanayobatilisha Hija

Haya ndio yanayobatilisha Hija

Kubatilika kwa Hija
Hija itabatilika iwapo Haji ataacha kutekeleza moja wapo ya matendo yafuatayo:



(i) Ihram au nia ya Hija na kuwa katika hali ya Ihram ikiwa ni pamoja na vazi lake kwa wanaume na kuchunga masharti ya Ihram. Mtu akivunja masharti ya Ihram Hija haibatiliki lakini analazimika kufidia kwa kuchinja mnyama au kulisha maskini au kufunga. Ila kufanya tendo la ndoa ndani ya Ihram hubatilisha Hija kabisa.
Sa’i kati ya Safaa na Marwa.



(ii) Kuhudhuria katika uwanja wa Arafat siku ya mwezi 9 Dhul- Hija kati ya kuchomoza jua la mwezi 9 dhul-Hija na alfajir ya mwezi10 Dhul-Hija.



(iii) Tawaful Ifadha (Tawafu ya Nguzo).


Lengo la Hija
Kama tulivyojifunza katika masomo yaliyopita, lengo la ujumla la kuamrishwa kusimamisha nguzo tano za Uislamu, Shahada, kusimamisha Swala, Kutoa Zaka, Kufunga Ramadhani na Kuhiji Makka - ni kumuandaa mja aweze kuishi kulingana na lengo la kuumbwa kwake na kuletwa hapa duniani. Lengo la kuumbwa mwanaadamu limebainishwa katika Qur-an kuwa ni kumwabudu Allah(s.w.) katika kila kipengele cha maisha yake (Rejea Qur’an 51:56).



Ibada ya Hijja ni kilele au ni Chuo Kikuu cha kukamilisha maandalizi ya kumfikisha Muumini katika lengo la kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) katika kila kipengele cha maisha na kumuwezesha Muumini kuisimamisha dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa juu ya dini zote.



Namna Hija inavyomuandaa Muumini kuwa Khalifa waAllah katika jamii
Katika sehemu hii tutaangalia falsafa ya kila kitendo cha Ibada ya Hija kuanzia maandalizi ya safari mpaka mwisho wa safari na kuonesha namna ya kila kitendo cha Hijja kinavyomuandaa mja kuwa mcha-Mungu aliyetayari kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kwa hali na mali.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 2696

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰3 ai web app     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     πŸ‘‰6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

MALI ZISIZORUHUSIWA KUTOLEWA ZAKA

*Suala la kumilikiwa binaadam (utumwa), japokuwa linaendelea kutajwa kwenye Sharia (katika vitabu), ni suala ambalo haliko.

Soma Zaidi...
Warithi wasio na mafungu maalumu katika uislamu

Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi.

Soma Zaidi...
Haki za maadui katika vita (mateka wa kivita)

Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mambo yanayoharibu Udhu (yanayobatilisha udhu)

Post hii inakwenda kukufundisha mambo ambayo hubatilisha udhu yaani mam,boa mbayo yanaharibu udhu.

Soma Zaidi...