Ni zipi sifa za imamu wa swala?
Sifa za Imamu Imamu ni kiongo kuongoza swala:
1. Mwenye zi. Mtu yeyote mwenye sifa zifuatazo anaweza
kuweza kuisoma Qur-an vizuri na mwenye
kuielewa vizuri.
2. Anayefahamu na kuelewa vizuri hadithi na Sunnah.
3. Mwenye tabia njema na siha nzuri.
4. Mwenye umri mkubwa (sifa hizi zizingatiwe kwa mfuatano wake).
Kama itatokea kwenye msikiti mmoja kuna watu wengi wenye sifa hizi, itabidi ipigwe kura. Pia kiongozi au mtu mwenye mamlaka katika jamii atakuwa ndiye mwenye haki ya kuwa Imamu. Hali kadhalika mtu akiwa nyumbani kwake, atakuwa ndiye mwenye haki ya kuwa Imamu. Sifa hizi zinabainishwa katika Hadithi ifuatayo:
Abu Mas ’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Yule aliye na uwezo mkubwa zaidi wa kusoma Kitabu cha Allah (Qur-an) atakuwa Imamu wao. Kama watakuwa sawa kwa kusoma Qur-an basi atakuwa Imamu yule aliye na ujuzi mkubwa wa Hadithi, na kama wako sawa basi yule aliyetangulia kuhajiri (kuham a kutoka Makka kw enda Madina) na kama wako sawa katika kuhajiri, basi yule aliye na umri mkubwa kuliko wote ndiye atakayekuwa Imamu. Hakuna mtu atakaye kuwa Imamu wa yule aliyemzidi madaraka (au yule aliye na mamlaka juu yake) na wala hatakaa katika nyumba yake kwa kumpa heshima mpaka apate ridhaa yake. Na hakuna mtu atakayekuwa Imamu katika nyumba au familia ya mwingine. (Muslim).
Imamu wa msikiti atakapochaguliwa hapatakuwa na mwingine kuswalisha bila ruhu sa yake. Ni vibaya mno kujipachika Uimamu mahali bila ya ridhaa ya watu unaowaongoza. Aliyejipachika Uimamu swala yake haitasihi.
Ibn Umar amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema kuwa watu w atatu ambao sw ala zao hazitakubaliwa ni: “Yule anayeswalisha w atu na huku hawamtaki, anayekuja kwenye swala nyuma (kuja kwenye swala baada ya wakati kupita, pia kuswali mwenyewe nyuma ya mstari), na yule anayemfanya mwanamke huru kuwa mtumwa”.(Abu Daud, Ibn Majah).
Kumfuata Imamu baada ya kuwekwa ni jambo la lazima. Hata kama Imamu huyo atafanya makosa au dhambi kubwa kiasi gani kabla Waislamu hawajamtoa na kumweka mwingine itabidi lazima wamfuate kutokana na Hadithi ifuatayo:-
Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah (s.a.w) amesema, “Jihadi ni wajibu chini ya Amir yeyote akiwa mcha-Mungu, au si mcha-Mungu na hata kama atakuwa amefanya madhambi makubwa, na swala ni wajibu nyuma ya kila Imamu akiwa mcha-Mungu au si mcha-Mungu na hata akiwa amefanya madhambi makubwa ”. (Abu Daudi)
Inavyotakiwa, kama Imamu ataonekana kuwa anakiuka miiko ya Kiislamu kwa kutenda yale yaliyokatazwa katika Uislamu, kama vile zinaa, ulevi, wizi, n.k. itabidi Waislamu wamtoe kwenye Uimamu na kuweka Imamu mwingine mwenye sifa zilizotajwa. Kabla ya kuchagua mwingine watawajibika kumfuata Imamu huyo huyo muovu.Hekima yake ni kuepusha ugomvi, mifarakano baina ya waislamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 web hosting 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Je ni nani mwenye haki ya kutaliki
Hapabutajifunza endapp mwanamke anahitaji kuachwa ni nini anatakiwa afanye.
Soma Zaidi...Jinsi ya kumuandaa maiti baada ya kufa
Haya ni maandalizi ya kumuandaa maiti baada ya kufariki.
Soma Zaidi...Zijuwe funga za sunnah na jinsi ya kuzifunga
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu funga za sunnah na jinsi ya kuzigunga.
Soma Zaidi...Jinsi ya kusherehekea siku ya idi katika uislamu
Uislamu umeweka taratibu maalumu za kuzifata katika kusherehekea siku ya idi.
Soma Zaidi...Jinsi ya kutoa zakat al fitiri na umuhimu wa zakat al fitri kwa waislamu
Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii.
Soma Zaidi...