5.
5. Swala ya Tarawehe
Swala ya Tarawehe ni miongoni mwa Sunnah zilizokokotezwa. Swala hii huswaliwa katika mwezi wa Ramadhan tu wakati wowote kati ya kipindi baada ya swala ya Isha na kuingia kwa swala ya Alfajiri. Umuhimu wa swala hii umedhihiri katika Hadithi ifuatayo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akisisitiza swala ya usiku katika mwezi wa kufunga (Ramadhani), bila ya kuifaradhisha kwao. Alikuwa akisema: Atakaye swali katika usiku wa mwezi wa kufunga, akiwa na imani na akitarajia malipo (kutoka kwa Allah (s.w), dhambi zake zilizotangulia husamehewa. (Muslim)
Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali Tarawehe katika sehemu ya pili ya usiku (katika wakati ule ule wa Tahajjud). Mtume (s.a.w) aliswali Tarawehe pamoja na masahaba katika jamaa siku tatu, kisha akaacha na akawa anaswalia nyumbani kwake kama tunavyofahamishwa katika Hadithi ifuatayo:
‘Aysha (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alikwenda msikitini usiku na akaswalisha Tarawehe na watu wakaswali naye. Asubuhi watu wakasimuliana habari hiyo. Mtume (s.a.w) siku ya pili alikwenda kuswalisha watu wakajaa msikitini. Alifanya hivyo hivyo siku ya tatu. Asubuhi siku ya nne watu wakapeana habari na wakajazana zaidi msikitini kwa ajili ya sw ala ya Tarawehe lakini Mtume (s.a.w) hakw enda
kuswalisha. Baadhi ya watu walisema kwa sauti “swalah”, lakini Mtume (s.a.w) hakwenda msikitini mpaka Alfajir. Alipomaliza sw ala ya Alfajir aliwakabili watu na kuwaeleza: “Jambo lenu halikuwa limefichikana kwangu, lakini nilichelea kuwa kama ningaliendelea mfululizo na swala hiyo ya Tarawehe huenda ingalifanywa kuwa ni faradhi kwenu na huenda m ungalishindw a kuitekeleza ”. (Muslim)
Pamoja na Hadithi hii, pia Mtume (s.a.w) aliwasisitiza Waislamu kuswali swala za Sunnah majumbani mwao na kuwahakikishia kuwa kufanya hivyo kuna malipo makubwa zaidi. Swala ya Tarawehe iliendelea kuswaliwa na kila mtu nyumbani kwake katika kipindi chote cha Mtume (s.a.w) na kipindi cha Khalifa wake wa kwanza (Abu Bakar). Khalifa wa pili, Umar bin Khattab, alianzisha tena kuswali swala ya Tarawehe kwa jamaa msikitini kama inavyoendelea mpaka hivi leo.
Idadi ya Rakaa za Swala ya Tarawehe
Kumekuwepo na maelezo tofauti kuhusiana na idadi ya rakaa za Swala ya tarawehe kutoka kwa wanazuoni tofauti. Lakini kutokana na Hadithi iliyosimuliwa na Mama Aysha (r.a) na kupokelewa na Maimamu wa Hadithi, Mtume (s.a.w) hakupata kuswali zaidi ya rakaa 11 katika mwezi wowote ule. Hadithi ya Jabir (r.a) iliyopokelewa na Ibnu Khuzaimah na Ib n Hibban, Mtume ameripotiwa kuswali rakaa nane za tarawehe na rakaa tatu za witri pamoja na Masahaba wake na kisha siku iliyofuatia akawa hakutoka kwenda kusalisha.
Ama kuhusiana na kuswali rakaa ishirini, ni kweli kuwa Khalifa Umar, Uthman na Ali (r.a) waliswali kwa rakaa hizo. Imamu Ibnu Hibban amesema kuwa mwanzoni ilikuwa ni rakaa kumi na moja isipokuwa kisomo (kisimamo) kilikuwa kirefu kiasi cha watu kuchoka. Hivyo baadaye ikaamuliwa kuwa idadi ya rakaa iongezwe na kisomo kipunguzwe na kuwa cha wastani ingawaje jambo hili halikuingiza Swala ya Witri, kutoka hapo kwenye rakaa 20 ilifika kwa badhi ya wengine akiwemo Imamu Malik hadi rakaa 36 ikiwa kisomo kimezidi kufupishwa. Iliyo sunnah ni kuswali tarawehe kwa rakaa 11-8 za kisimamo cha usiku cha kawaida na rakaa 3 za witri. Kwa kuwa mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Qur-an inahimizwa sana kuwa Waislamu wahitimishe Qur-an yote alau kwa kusoma juzuu moja kila siku. Tarawehe ni swala sawa na swala nyingine hivyo kusihi kwake kunafungamana na kupatikana khushui, masharti na nguzo zote za swala. Ama hizi tarawehe zinazoswaliwa katika misikiti mingi mbazo Imamu hupata sifa kwa kuswali mbio mbio pasipo na mazingatio wala utulivu ni kinyume kabisa na utaratibu wa swala. Watu wengi ambao huharakisha kumaliza swala ya tarawehe kwa kiasi cha kutokamilisha nguzo za swala hawapati malipo yoyote kutokana na swala zao. Bali kwa kuwa watu hawa wanaifanyia swala mchezo hapana cha kutarajia zaidi ya adhabu kali waliyoahidiwa na Allah (s.w):
“Basi adhabu itawathibitikia wanao swali, ambao wanapuuza swala zao”. (107:4-5)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 3573
Sponsored links
👉1
Simulizi za Hadithi Audio
👉2
Madrasa kiganjani
👉3
Kitabu cha Afya
👉4
kitabu cha Simulizi
👉5
Kitau cha Fiqh
👉6
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Dua ya kuzuru makaburi, na utaratibu wa kuzuru makaburi
Kuzuru makaburi ni katika matendo ya sunah yaani unapata thawabu kwa kwenda klizuru kaburi. Soma Zaidi...
Kujitwaharisha kutokana na najisi
Post hii itakufundisha namna ya kutwaharisha Najisi. Soma Zaidi...
Vipi funga yaani swaumu itapelekea uchamungu na kutekeleza lengo
Funga inavyomuandaa mtu kuwa mcha-Mungu. Soma Zaidi...
Wanaowajibika kuhijji
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Sifa nyingine za kuchaguwa mchumba ambazo watu wengi hawazijui
Hizi ni sifa za ziada za mchumba katika uislamu. Sifa hizi wengi hawazijui ama hawazingatii. Soma Zaidi...
Fiqh.
Kipengele hichi tutajifunza chimbuko la fiqh na maana ya figh. Soma Zaidi...
Ni zipi nguzo za swaumu na masharti ya Swaumu
Soma Zaidi...
Kwanini funga imefaradhishwa mwezi wa ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kujiepusha na ria na masimbulizi
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...