Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume

Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Uteuzi wa Uthman bin Al-'Afan khalifa wa Tatu baada ya Mtume

Uchaguzi wa Uthman bin Afan


Uchaguzi wa Uthman bin Affan Kuwa Khalifa wa Tatu Uislamu sio dini iliyofungwa katika mabano bali ina sifa ya kwenda na wakati kwa maana kuwa maamuzi yake ilimradi yamo katika mfumo wa Uislamu yanakubalika. Hali ilivyokuwa wakati alipotawafu Mtume(s.a.w) imetofautiana na ile ya wakati alipotawafu Abubakar. Wakati wa kifo cha Abubakar, Umar alikuwa amejitokeza kuwa ndiye Khalifa bila upinzani lakini wakati wa kifo cha Umar hali ilikuwa tofauti. Walikuwepo watu wengi wenye sifa zinazolingana hivyo alichokifanya Umar ni kuteua jopo la wagombea sita wa ukhalifa ambao walikuwa Uthman, Ali, Saad bin Waqqas, Talha, Zubair na Abdur-Rahman bin Auf.26 Agizo lingine alilotoa ni kuwa katika muda wa siku tatu baada ya kifo chake wawe wameshaamua wao wenyewe nani miongoni mwao awe
Khalifa.


Jopo hili lilikaa kwa muda mrefu bila kufikia uamuzi ndipo Abdur-Rahman bin Auf aliposhauri kuwa kati yao mmoja ajitoe ili aweze kutoa uamuzi. Alipokosa jibu alijitoa mwenyewe na akaanza kazi ya kutafuta maoni ili kukamilisha uteuzi. Talha hakuwepo hivyo wagombea walibaki wanne. Imetokea kuwa Ali alimpendekeza Uthman na Uthman alimpendekeza Ali. Zubair na Saad walimpendekeza Uthman. Baada ya kushauriana na Maswahaba wengine na kwa kuzingatia muda wa siku tatu Abdur-


Rahman bin Auf alitoa uamuzi asubuhi ya siku ya nne na kumtangaza Uthman kuwa ndiye Khalifa. Abdur-Rahman bin Auf (r.a.) alianza kumpa baiโ€™at (mkono wa ahadi ya utii) na kutambua Ukhalifa wake ndipo Waislamu waliokuwa msikitini wakafuatia na kwa namna hii Uthman akawa Khalifa wa tatu. Talha aliporudi Madinah, Uthman alimshauri achague moja kati ya mawili, achukue nafasi ya Ukhalifa au ampe mkono wa ahadi ya utii. Talha alikubali kumpa mkono wa ahadi ya utii.


Utaratibu huu pia umo katika mkondo wa Uislamu na ni aina ya tatu ya utaratibu unaokubalika wa kupata viongozi katika Uislamu.




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 687

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰3 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Mtume Muhammad s.a. w akutana na Bahira
Mtume Muhammad s.a. w akutana na Bahira

Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 11

Soma Zaidi...
Historia ya Dhulqarnain
Historia ya Dhulqarnain

Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: โ€œMwenye Pembe Mbiliโ€.

Soma Zaidi...
Vita vya Al Fijar na sababu zake
Vita vya Al Fijar na sababu zake

Historia na shida ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 12. Hapa utajifunza kuhusu kutokea kwa vita vya al fijar.

Soma Zaidi...
Historia ya kujengwa kwa Alkabah (Maka)
Historia ya kujengwa kwa Alkabah (Maka)

Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a.

Soma Zaidi...
Bara arabu enzi za jahiliyyah, jiografia ya bara arabu
Bara arabu enzi za jahiliyyah, jiografia ya bara arabu

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mbinu walizotumia makafiri wa kiqureish katika kuupinga uislamu makkah
Mbinu walizotumia makafiri wa kiqureish katika kuupinga uislamu makkah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...