Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.
- Maqureish wa Makkah walitumia kila mbinu kuhakikisha kuwa ujumbe wa Uislamu haufiki na kukubalika katika jamii yao, miongoni ni hizi zifuatazo;
- Makafiri walimdhihaki Mtume (s.a.w) na waumini wachache kwa
kumuita majina mabaya kama; mwendawazimu, mtunga mashiri,
aliyepagawa na mashetani, mchawi, n.k.
- Pamoja na kusimangwa huko Mtume (s.a.w) na waislamu hawakukata
tamaa, waliendelea kuutangaza Uislamu katika jamii yote.
- Wakuu wa Maquraish walimuagiza Abu Talib amkataze Muhammad
(mwanae) kuendelea kuutangaza Uislamu kwa kumbadilishia mtoto
mwingine la sivyo watamshambulia yeye na Muhammad (s.a.w).
- Mbinu hii haikufanikiwa badala yake Abu Talib alimuunga mkono
Mtume (s.a.w) kwa kazi yake baada ya kujua msimamo wake.
- Maquraish walitumia diplomasia kwa kumtaka Mtume (s.a.w) aache
kazi ya kuutangaza Uislamu kwa kumpa kati ya vitu vifuatavyo;
utajiri, mwanamke mzuri, madaraka au yote kama akitaka.
- Mtume (s.a.w) aliwakatalia vyote hivyo kwa kumsomea aya za Qur’an
(41:1-37) mjumbe aliyetumwa kazi hiyo, Utbah bin Rabi’ah.
- Maqureish walimletea Mtume (s.a.w) pendekezo kuwa washirikiane
katika ibada kwa awamu, mwaka mmoja wamuabudu Mungu mmoja
kwa pamoja na mwaka unaofuatia waabudu miungu yao pamoja pia.
- Hapo ndipo iliposhuka suratul-Kafiruun kuvunja pendekezo lao hilo la
kushiki katika ibada na Mtume akawasomea aya za Qur’an kukataa.
Rejea Qur’an (109:1-6) na (10:15).
- Baada ya Maqureish kuona mbinu zote zimefeli, walianza kutumia
nguvu na mabavu kuwatesa, kuwanyonga na kuwaua Waislamu
waliong’ang’ani imani yao kama akina; Bilal bin Rabbah, Sumaiyya,
Ammar bin Yasir na baba yake, n.k.
- Pamoja na mateso na mauaji, waislamu walibakia na msimamo wao
bila kutetereka na kukata tamaa.
- Maquraish kwa kuhofia ujumbe wa Qur’an kuenea kwa watu,
walianza kuzuia watu kwenda kuonana na Mtume (s.a.w) kwa
kuwashawishi kuwa wasisikilize aya za Qur’an kwani ni uchawi,
mashairi ya Muhammad.
- Walizidi kufitinisha kwa kumzuia Mtume (s.a.w) kuswali na
kuwaambia watu kuwa Muhammad anapinga ibada na miungu wenu,
lakini mbinu na ushawishi wao ulifeli pia.
Rejea Qur’an (31:6), (41:26), (10:38), (11:13) na (96:9-19).
- Maquraish walizidi kuongeza mateso kwa waislamu kwa kutenga na
kuwafukuza Makka na kwenda kuishi katika jangwa la Shi’ab miaka
mitatu bila chakula wala mahusiano mengine ya kijamii.
- Mbinu pia ilifeli baada ya baadhi ya Maquiesh kuona huruma kwa
ndugu zao waliotengwa bila sababu za msingi, hivyo wakavunja
mkataba wa kuwatenga.
- Maquish waliazimia kumuua Mtume (s.a.w) na rafiki yake Abubakar
(r.a) walipogundua kuwa waislamu wamehamia mji wa Madinah.
- Mbinu hii pia ilifeli baada ya Allah (s.w) kuwanusu katika pango yeye
na sahibu yake Abubakar (r.a).
Rejea Qur’an (9:40).
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Makafiri wa Kithamud hawakuishia tu kwenye kuukataa ujumbe wa Nabii Salih(a.
Soma Zaidi...Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma.
Soma Zaidi...