HISTORIA YA NABII AYYUUB(A.S)

HISTORIA YA NABII AYYUUB(A.S)

Ayyuub(a.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

HISTORIA YA NABII AYYUUB(A.S)

HISTORIA YA NABII AYYUUB(A.S)


Ayyuub(a.s) ni katika Mitume wa Allah(s.w) waliotajwa katika Qur-an kwa umadhubuti wake katika imani juu ya Allah(s.w) na Subira.

Ayyuub(a.s) aliishi Kaskazini Mashariki ya Bara Arabu. Alikuwa tajiri sana mwenye mali nyingi, watoto wengi na watumishi wengi. Lakini hakutakabari bali alimuabudu Mola wake na kumshukuru ipasavyo

Mitihani Iliyomfika Ayyuub(a.s)


Nabii Ayyuub(a.s) alitahiniwa na Mola wake kama ifuatavyo:

(1) Mali yake, watoto wake na watumishi wake wote walipatwa na majanga wakatoweka. Akabakia yeye na mkewe ambaye naye alikuwa mcha-Mungu.

(2) Pamoja na kupotelewa na mali yake na watu wake wote, alishikwa na maradhi mabaya ya kuota vidonda mwili mzima kuanzia kichwani hadi miguuni. Alijaribu kutumia dawa zote alizoweza, lakini hakupata nafuu yoyote


Nabii Ayyuub(a.s) hakutetereka katika imani yake kutokana na majanga yaliyomfika bali alisubiri na kuwa karibu zaidi na Mola wake kuliko hata wakati alipokuwa katika hali yake ya mwanzo ya utajiri na afya nzuri. Na Allah(s.w) anamsifu mjawake, Ayyuub kama ifuatavyo:

β€œβ€¦. Bila shaka tulimkuta ni mwenye subira mja mwema; kwa hakika alikuwa mnyenyekevu sana.” (38:44)

Nabii Ayyuub(a.s) aliona kuwa aliyempa mali, watoto na wale watumishi aliokuwa nao ni Allah(s.w) kama amana. Hivyo, aliona hapakuwa na kosa lolote kwa Allah(s.w) kuchukua amana yake. Pia aliridhika na hali ya ugonjwa aliyokuwa nayo. Kwa ujumla Nabii Ayyuub (a.s) aliridhika na kusubiri juu ya matatizo yote yaliyomfika na kupata matunda ya subira kama Allah(s.w) anavyotubashiria:

Na tutakutieni katika msukosuko wa (baadhi ya mambo haya); hofu na njaa na upungufu wa mali na wa watu na wa matunda. Na wapashe habari njema wanaosubiri.(2:155) Ambao uwapatapo msiba husema: β€œHakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye tutarejea (atatupa jaza yake).(2:156)

Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao na rehema; na ndio wenye kuongoka. (2:157)



                   

Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 3386

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Mafunzo yatokanayo na hijrah ya mtume na maswahaba wake
Mafunzo yatokanayo na hijrah ya mtume na maswahaba wake

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu
Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu

Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu.

Soma Zaidi...
KUCHIMBWA UPYA KWA KISIMA CHA ZAMZAMA NA KUNYWA MAJI YA ZAMZAMA KISIMA KILICHO BARIKIWA
KUCHIMBWA UPYA KWA KISIMA CHA ZAMZAMA NA KUNYWA MAJI YA ZAMZAMA KISIMA KILICHO BARIKIWA

KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba.

Soma Zaidi...
Msimamo wa Nabii Nuhu(a.s) Dhidi ya Makafiri
Msimamo wa Nabii Nuhu(a.s) Dhidi ya Makafiri

Pamoja na upinzani mkali alioupata kutoka kwa viongozi wa makafiri, Nabii Nuhu(a.

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)

Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a.

Soma Zaidi...
Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume
Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume

Uchaguzi wa β€˜Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.

Soma Zaidi...
Madhumuni ya dola ya uislamu
Madhumuni ya dola ya uislamu

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...