Pamoja na upinzani mkali alioupata kutoka kwa viongozi wa makafiri, Nabii Nuhu(a.
Pamoja na upinzani mkali alioupata kutoka kwa viongozi wa makafiri, Nabii Nuhu(a.s) aliendelea kwa hima kulingania Dini ya Allah(s.w) na kuuweka wazi msimamo wake kama ifuatavyo:
βWasomee habari za Nuhu alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Ikiwa kukaa kwangu na nyinyi na kukumbusha kwangu Aya za Mwenyezi Mungu kunakuchukizeni, basi mimi nategemea kwa Mwenyezi Mungu. Nanyi kusanyeni mambo yenu na hao washirika wenu. (Kusanyikeni mje kunidhuru, mimi sijali).
Tenashauri lenu hilo lisifichikane kwenu (fanyeniu kwa dhahiri; mimi sijali tu). Kisha mpitishe kwangu (hilo mnalotaka kupitisha). Wala msinipe nafasi (hata kidogo. Mimi sijali, namtegemea Mwenyezi Mungu tu).β (10:71)
Nabii Nuhu(a.s) aliendelea kuwausia watu wake na kudhihirisha msimamo wake.
βNa enyi watu wangu! Mimi sikuombeni mali juu ya (jambo) hili; sina ujira wangu ila kwa Mwenyezi Mungu; na mimi sitawafukuza walioamini (kama mnavyotaka kwangu niwafukuze hao madhaifu ndipo msilimu nyinyi watukufu. Sitafanya hivyo); maana wao watakutana na Mola wao (awalipe kwa mema yao na mabaya yao). Lakini mimi nakuoneni nyinyi ni watu mnaofanya ujinga. (Mnakataa kuifuata haki kwa kuwa imefuatwa na madhaifu)! (11:29).
β’ Nabii Nuhu(a.s) hakumchelea yeyote au chochote katika kulingania Dini ya Allah(s.w), bali alimtegemea Allah(s.w).
β’ Alilingania Dini ya Allah kwa kutarajia malipo kutoka kwake tu.
β’ Aliwapokea na kuwakumbatia wote waliomuamini bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Nabii Nuhu(a.s)alilingania Uislamu katika mazingira magumu ya upinzani mkubwa bila ya kukata tamaa kwa muda wa miaka 950.
Alipoona kuwa viongozi wa makafiri wanazidi kuweka mikakati ya kuzuia watu kusilimu kila uchao na kuwashinikiza kurudi kwenye ukafiri hata wale walioamini kwa kuwafanyia vitimbi mbalimbali, Nabii Nuhu(a.s) alilazimika kuomba msaada wa Allah(s.w) dhidi ya makafiri kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
βNa (wakumbushe) Nuhu alipotulingania zamani (kutuomba) nasi tukamuitikia, na tukamuokoa yeye na watu wake katika shida (msiba) kubwa hiyo.(21:76)
Na tukamnusuru juu ya watu waliozikadhibisha aya zetu. Hakika wao walikuwa watu wabaya. Basi tukawatotesha (gharikisha) wote.β (21:77)
Kabla yao kama tulivyoona watu wa Nuhu walikadhibisha nao. Walimkadhibisha mja Wetu na wakasema ni mwendawazimu; na akawa anatolewa maneno makali. Ndipo akamuomba Mola wake (akasema): βKwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru.(54:9-10)
Mara tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayomiminika (kwa nguvu kabisa). Na tukazibubujisha maji chemchem zilizo katika ardhi; na maji (ya juu na chini) yakakutana kwa jambo lililokadiriwa (na Mungu).(54:11-12)
Na Tukamchukua (Nabii Nuhu) katika ile(jahazi) iliyotenge nezwa kwa mbao na misumari. Ikawa inakwenda mbele ya macho, (hifadhi) Yetu. Hii ni tunzo (tuzo) kwa yule aliyekuwa amekataliwa (amekanushwa). (54:13-14)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa Nabii Nuhu(a.s) pamoja na waumini wachache aliokuwa nao walipata ushindi mkubwa juu ya makafiri waliokuwa wengi na uwezo mkubwa kwa msaada wa Allah(s.w). Allah(s.w) alitumia jeshi la βmajiβ kuwaangamiza makafiri na akawanusuru waumini kwa jahazi. Hii inatukumbusha kuwa:
βNa majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na
Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu, mwenye hikima.β (48:7)
Umeionaje Makala hii.. ?
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Tumeona katika historia yake kuwa Nabii Ibrahiim(a.
Soma Zaidi...Kutokana na histoira ya Nabii Sulaiman (a.
Soma Zaidi...Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.
Soma Zaidi...Ukombozi wa mji wa Makka (Fat-h Makka) mwaka 8 A.
Soma Zaidi...HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba.
Soma Zaidi...