image

Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu

Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu.

Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu

Mafunzo Yatokanayo na mambo Aliyofanya Mtume (s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu

Kwanza, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii hatunabudi kuanzisha na kuendeleza vituo vya harakati, misikiti ikiwa ndio vitovu. Kila palipo na fursa nzuri ni muhimu kuibadili misikiti iliyopo na kuifanya vituo vya harakati. Lakini ichukuliwe tahadhari kubwa ili tusije tumbukia kwenye kosa la kuvamia misikiti ya watu kabla ya kufikia kipindi cha kuikomboa – Fat-h-Makka.



Pili, hatunabudi kujenga mshikamano wa Waislamu kwa njia ya kupendana na kuhurumiana na hasa kwenye matatizo na shida. Rejea udugu baina ya Answar na Muhajiriina. Hatunabudi kujenga mazingira na tabia ya kufanya kazi za bega kwa bega (za kitamasha) katika kuendeleza shughuli mbali mbali kwa ajili ya maendeleo ya Uislamu.



Tatu, hatunabudi kukaa vizuri na wasiokuwa Waislamu hasa wale wasiotupiga vita bayana.Tuwaheshimu, tuwatendee haki na tusiwatukanie miungu yao wala kuidhihaki dini yao. Tuwalinganie kwa hekima na tuwape changamoto ya hoja na mawaidha mazuri.




Waite (waite watu) katika njia ya Mola wako kwa hikima na mauidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora (siyo kwa kuwatukana wao au kutukana Dini yao. Kwa njia hii huwezi kumvuta mtu). Hakika Mola wako ndiye anayemjua aliyepotea katika njia yake, naye ndiye anayewajua walioongoka. (16:125)



Nne, hatunabudi kuwajua vema maadui wa Uislamu na Waislamu na kuzijua vyema hila na mbinu zao katika kuuhujumu Uislamu. Kila Muislamu anatakiwa awe msalama kwa kumjua ni nani adui wa Uislamu, yuko wapi na anafanya nini dhidi ya Uislamu.



Tano, kila Muislamu mwanamume hanabudi kuwa mkakamavu na jasiri aliyetayari kuingia vitani ili kuihami Dini ya Allah(s.w).

Basi waandalieni (wawekeeni tayari) nguvu mziwezazo (silaha), na mafarasi yaliyofungwa tayari (mipakani), ili kwazo (nguvu hizi) muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, (mnaowajua) na pia (maadui zenu) wengine wasiokuwa wao, msiowajua nyinyi (lakini) Mwenyezi Mungu anawajua. Na chochote mtakachokitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu (kama hii misaada ya vita vya Jihadi) mtarudishiwa kamili wala hamtadhulumiwa. (8:60)



Sita, ili tuweze kusimamisha Uislamu katika jamii yetu, hatuna budi kuimarisha uchumi wetu.Uchumi ndio raslimali kuu ya kusimamishia Uislamu katika jamii. Kila kitu cha kimaendeleo kinahitaji matumizi ya mali. Hatunabudi kuhuisha na kuimarisha ukusanyaji na ugawaji wa Zakat na Sadaqat kijamii.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 345


Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰2 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Hadhi na haki za Mwanamke katika jamii za Mashariki ya Kati bara la arabu hapo zamani
Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 05
Soma Zaidi...

Waliomuamini Nabii Nuhu(a.s)
Waliomuamini Nuhu(a. Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 03
Soma Zaidi...

tarekh 02
FAMILIA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUTI
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII IBRAHIIM(A.S) NA KUANDALIWA KWAKE:
Nabii Ibrahiim(a. Soma Zaidi...

Njama za Kumuua Nabii Yusufu(a.s)
Kwa tabia zake njema Yusufu(a. Soma Zaidi...

Khalifa β€˜Umar bin Abdul Aziz
Soma Zaidi...

tarekh11
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Soma Zaidi...

Kuandaliwa kwa Muhammad kabla ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

HISTORIA NA VISA VYA MITUME, MANABII NA WATU WEMA WALIOTAJWA KWENYE QURAN
Soma Zaidi...