Mafunzo yatokanayo na hijrah ya mtume na maswahaba wake

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Mafunzo yatokanayo na Hijrah ya Mtume (s.a.w) na Maswahaba wake.

  1. Hatuna budi kutunza na kurejesha amana za watu kwa wenyewe bila kujali uadui wao kwetu.

 

  1. Waislamu hawanabudi kuweka mipango na mikakati madhubuti juu ya namna ya kutekeleza mambo yao kabla ya utekelezaji wake.

 

  1. Waislamu hawana budi kuchukua tahadhari katika kuendesha harakati za kidini kwa kuzingatia kuwa dini ya Uislamu ina maadui wengi.

 

  1. Nusura ya Allah (s.w) na Ushindi hupatikana tu baada ya kufanyika jitihada za dhati katika kuusimamisha Uislamu katika jamii na kumtegemea yeye pia.

 

  1. Waislamu wanalazimika kufanya jitihada ya dhati ya kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo kwa kila kipengele cha maisha yao, kama mazingira yatakuwa ndio kikwazo hawanabudi kuhama (kuhajiri) kwenda sehemu (ardhi) yenye wasaa.

Rejea Qur’an (4:97-99).

 

  1. Kuhajiri (kuhama) kwa ajili ya Uislamu sio ukimbizi, bali ni katika mikakati na mipango ya kwenda kujiimarisha huko na hatimaye kuja kukomboa sehemu mlikotoka.

 

  1. Kutokana na Hijrah ya Mtume (s.a.w), tunajifunza kuwa waislamu wote ni ndugu mmoja bila ya kujali kabila, rangi, taifa, n.k.

 

  1. Uislamu siku zote hauwezi kusimama katika jamii mpaka waislamu tuwe tayari kujitoa muhanga kwa mali na nafsi zetu kadri ya uwezo wetu.

 

  1. Ni haramu kwa muislamu kuishi katika nchi ya kikafiri au utawala wa kikafiri isipokuwa, itakapokuwepo jitihada ya kuundoa ukafiri na kuutawalisha Uislamu au yatakapokuwepo maandalizi ya kuhama sehemu hiyo
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1478

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi

Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri.

Soma Zaidi...
Kulingania Uislamu kwa Jamii Nzima

Baada ya miaka mitatu ya Utume, Muhammad(s.

Soma Zaidi...
Maryam Apewa Habari ya Kumzaa Isa(a.s)

Baada ya maandalizi hayo ya kimalezi pamoja na hifadhi ya Allah(s.

Soma Zaidi...
Kujengwa upya al Kabah baada ya kuwa na mipasuko.

Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 18. Hapa utajifunza kuhusu tukio la kujengwa upya kwa al kaaba 🕋

Soma Zaidi...