KUCHIMBWA UPYA KWA KISIMA CHA ZAMZAMA NA KUNYWA MAJI YA ZAMZAMA KISIMA KILICHO BARIKIWA
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba.
![]()
![]()
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAM
Kwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Basi akachimba na ndipo akakuta chini ya kisima vitu ambavyo vilifukiwa pamoja na kisima. Walofukia vitu hivi ni watu kutoka kabila la Jurhum. Hawa pindi walipolazimika kuondoka Maka walikifukia kisima cha zamzam na kufukia baadhi ya vitu vya thamani kama mapanga, nguo za vita, na dhahabu. Baada ya hapo mlango wa alkaβaba ukatengenezwa kwa hii dhahabu waloipata. Na unyweshwaji wa maji ya zamzam kwa mahujaji ukarudi upya.
Basi kisima cha zamzam kilipoanza kutoa maji, watu kutoka kabila la quraysh walitaka kufanya makubaliano juu ya maji yale lakini Abdul Al-Muttalib alikataa kwa kudai kuwa Allah amempa mamlaka yeye tu. Basi wakakubaliana wakamuulize kuhani kutoka ukoo wa Bani Saβad juu ya swala hili. Basi Allah akawaonesha alama za ukweli juu ya madai ya Abdul Al-Muttalib. Baada ya hapo mzee Abdul Al-Muttalib kwa shukran yake kwa Allah akaapa kumtoa kafara mtoto wake kwa Mwenyezi Mungu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Bongolite - Game zone - Play free game π2 Kitabu cha Afya π3 ai web app π4 kitabu cha Simulizi π5 Madrasa kiganjani π6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Msimamo wa Nabii Nuhu(a.s) Dhidi ya Makafiri
Pamoja na upinzani mkali alioupata kutoka kwa viongozi wa makafiri, Nabii Nuhu(a.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Adam(a.s)
(i) Utukufu wa mtu katika Uislamu hautokani na nasaba, rangi,kabila,utajiri ila uwajibikaji kwa Allah(s.
Soma Zaidi...Kusilimu kwa Wachawi wa Firaun
Mawaziri waliokuwa washauri wakuu wa Firauni wakataka wakusanywe magwiji waliobobea katika uchawi nchi nzima, kisha wapambanishwe na Nabii Musa(as).
Soma Zaidi...