17.
17. Kuepuka kujisifu na kujitukuza
Waislamu tumekatazwa kujisifu sisi wenyewe na pia tumekatazwa kuwasifu wengine kupita kiasi.Mtume (saw) amekataza jambo hili katika Hadith zifuatazo:
Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (saw) amependekeza kwetu kuwa tumtupie mchanga (vumbi) usoni yule anayejihusisha na kuw asifus ifu w atu kupita kiw ango kinachos tahili. (Tirim idh).
Abu Bakar (ra) amesimulia kuwa mtu mmoja alimsifu mtu mwingine mbele ya Mtume (saw). Mtume (saw) alisema mara tatu. “Ole wako umekata kichwa cha ndugu yako!” (Kisha anasema Mtume); Yeyote miongoni mwenu ambaye ataona hapana budi kumsifu mwingine na aseme; Nafikiri fulani yuko hivi na hivi ( ana sifa hizi na hizi) na Allah (sw) atamuhesabu hivyo kama kweli mbele yake anastahiki sifa hizo. Lakini asithubutu mtu kumpachika yeyote sifa ya Ucha-Mungu(wema) juu ya Allah.” (Bukhari na Muslim)
Aidha Allah (sw) ametukataza kujisifu sifu katika aya ifuatayo:
“…Yeye (Allah) ndiye anayekujueni sana tangu alipokuumbeni katika ardhi na mlipokuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msizitakase nafsi zenu; Yeye (Allah) anamjua sana aliyetakasika ”. (53:32)
Kuwasifu sana watu kupita kiasi huwapelekea wale wenye kusifiwa kuvimba vichwa na kujihisi kuwa wao ni watukufu na bora zaidi kuliko wengine katika jamii. Tunayaona madhara makubwa yaliyojitokeza katika jamii ya waislamu kutokana na sifa za kupita kiasi tulizowapachika masheikhe zetu na watu wengine tuliowapachika usharifu, uwalii, ucha-mungu,n.k. Mgawanyiko wa waislamu tunaoushuhudia hivi leo kwenye madh-habu, twarika na matapo mengine mbali mbali, unatokana na dhambi hii ya kuwasifu viongozi wa hayo makundi kupita kiasi.
Pia tunajifunza katika historia kuwa chanzo cha Mitume wa Allah (sw) na watu wema kushirikishwa na Allah (s.w) ni kuwasifu kupita
kiasi. Katika Qur’an (9:30) tunafahamishwa kuwa kuwaiga washirikina waliowatangulia katika kuwasifu kupita kiasi viongozi wao, Mayahudi walimfaya Uzair (Mtu mwema) mwana wa Mungu na wakristo wakamfanya Isa Bin Maryam mwana wa Mungu. Kwa kuchelea watu wa Ummah nao wasijetumbukia kwenye shirki hii ya sifa, Mtume (saw) anatuasa katika Hadith ifuatayo:
“ Imepokelewa kutoka kwa Umar(r.a) kuwa amesema Mtume wa Allah (saw) Msizidishe kwenye kunisifu kama walivyozidisha wakristo ( manasara) katika kums ifu mwana wa Maryam. Mimi ni mja wa Allah tu; kwa hiyo niiteni ;”Mja wa Allah na Mtume wake ”. (Bukhari)
Hivyo muumini wa mkweli hanabudi kujiepusha na kujisifu sifu au kuwasifusifu watu. Na ikiwa hapana budi kumsifu mtu tuzingatie mipaka na tuseme kama alivyotuelekeza Mtume (saw) katika Hadith tuliyoirejea hapa juu. Tabia ya kujisifusifu au kuwasifusifu watu ni tabia ya uwongo, unafiki na ushirikina.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Makala hii inakwenda kukutajia majina ya vijana saba wa pangoni
Soma Zaidi...عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم ...
Soma Zaidi...Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote.
Soma Zaidi...Mwenendo wa kati ni mwenendo ulioepukana na kibri na majivuno kwa upande mmoja na ulioepukkana na udhalili na unyonge kwa upande mwingine.
Soma Zaidi...Ni ipi haki ya mwanamke kwenye mirathi endapo atafiwa na mume wake, ilihali yeye ni mke wa pili?
Soma Zaidi...Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE.
Soma Zaidi...