15.
15. Kujiepusha na Matusi
Mtu anayetukana ana lengo la kumdhalilisha mwingine. Waislamu tumekatazwa kutukanana na hata kuitana majina tusiyoyapenda kwa k ej eli.
“.... Wala msitukanane kwa kabila wala msiitane majina mabaya (ya kejeli). Jina baya kabisa kuitwa mtu ni “Fasiqi” baada ya kuwa yeye ni Muislamu. Na wasiotubu basi hao ndio madhalimu ”. (49:11)
Fasiq ni yule aliyebobea katika uasi. Yaani mtu anayejizatiti kumuasi Allah (s.w) kwa namna mbali mbali kama vile mwizi, mlevi,
mzinzi na kadhalika. Ni vibaya mno mbele ya Allah (s.w) kumsingizia au kumwita Muislamu ”mwizi” na huku si mwizi au kumwita “mnafiki” au “kafir” na huku ni Muislamu kamili. Tabia hii imekemewa vikali katika Qur-an:
“Kwa yakini wale wanaopenda uenee uovu kwa wale walioamini watapata adhabu iumizayo katika dunia na katika akhera, na Allah ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui”. (24:19).
Kutokana na makemeo haya, Muumini wa kweli hana budi kujiepusha na tabia ya kuwaita watu kwa majina mabaya kwani kufanya hivyo mtu hujilaani mwenyewe kiasi kwamba hayo majina mabaya yatamgeukia, kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Abu Dh-dhari(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Hapana mtu atakayemsingizia mwingine uasi kwa Allah au akamwita “kafiri”, ila hayo yatamgeukia yeye mwenyewe iwapo huyo aliyemsingizia hayuko hivyo”. (Bukhari)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowWaumini wa kweli huepuka kabisa tabia ya ugomvi na mabishano.
Soma Zaidi...Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada.
Soma Zaidi...Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Uadilifu ni usimamizi wa ukweli na kutoa haki kwa kila anayestahiki kulingana na ukweli.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukutajia majina ya vijana saba wa pangoni
Soma Zaidi...