Tanzu (makundi) za hadithi

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

-  Kutokana na usahihi, hadith zimegawanyika makundi manne;

  1. Hadith Sahihi.

                -  Ni Hadith zenye wasimulizi wote wenye sifa zilizokamilika na kuwa na  

                    matini sahihi.

 

  1. Hadith Hasan.

   - Ni Hadith zenye matini sahihi lakini baadhi ya wasimulizi wake 

      wamekuwa dhaifu.   

 

  1. Hadith Dhaifu.

      -  Ni Hadith yenye matini sahihi lakini miongoni mwa wasimulizi wake 

          wanakasoro kubwa zilizojitokeza.

      -  Hadith za namna hii haziaminiki na si za kutegemea.   

 

  1. Hadith Maudhu’u.

      -  Ni Hadith ya uwongo ambayo Mtume (s.a.w) amezuliwa nayo.

      -  Hizi ni Hadith zinazopingana na Qur’an na Hadith zilizo sahihi pia.

 

-  Kutokana na Umashuhuri, Hadith zimegawanyika makundi mawili;

  1. Hadith Mutawatir.

-  Ni Hadith yenye kusimuliwa na watu wengi kwa nyakati tofauti, wanne 

    au zaidi wote wakiwa na sifa kamili. 

-  Hadith hizi ni ndio zenye kukubalika na watu wote.

 

  1. Hadith Ahad.

-  Ni Hadith ambayo ina wasimulizi wenye sifa zilizokamilika, lakini 

    hawana mfungamano au msururu wa wasimulizi una mapengo kati kati.


                    -  Ni Hadith zisizokubalika kwa watu wengi, ni za mashaka mashaka na si                             za kutegemea.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Dini File: Download PDF Views 2790

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

quran na sayansi

2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.

Soma Zaidi...
Husaidia wenye matatizo katika jam ii

Huwa wepesi wa kutoa msaada kwa hali na mali kwa wanaadamu wenziwe wanaohitajia msaada.

Soma Zaidi...
(ix)Wenye kuhifadhi swala

Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu shuruti zote za swala nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume (s.

Soma Zaidi...
Uandishi wa hadithi wakati wa tabiina (wafuasi wa maswahaba)

Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za Funga

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...