Mwenendo wa kati ni mwenendo ulioepukana na kibri na majivuno kwa upande mmoja na ulioepukkana na udhalili na unyonge kwa upande mwingine.
Mwenendo wa kati ni mwenendo ulioepukana na kibri na majivuno kwa upande mmoja na ulioepukkana na udhalili na unyonge kwa upande mwingine. Kama ilivyo vibaya kwa mtu kujikweza na kujivuna mbele ya wengine ndivyo ilivyo vibaya kwa mtu kujidhalilisha na kujinyengesha mbele ya wengine. Muislamu anahaki ya kujidhalilisha na kujinyengesha kwa mmoja tu, ambaye ni Allah (s.w). Hivyo kujinyengesha na kujidhalilisha kwa yeyote awaye ni Shirk.
(j)Kushusha sauti
‘……na uteremshe sauti yako; bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote" (31:19)
Kushusha sauti ni kuzungumza kwa sauti ya heshima ambayo itawavuta wasikilizaji na kuwawezesha kupata ujumbe uliokusudiwa kwa dhana iliyo kusudiwa. Sauti ya punda ni sauti ya kufoka au kuonesha dharau, sauti ambayo haiwezi kufikisha ujumbe uliokusudiwa katika dhana iliyo kusudiwa. Pia katika kuzungumza na watu tunatakiwa tuchukue sauti ya kati na kati. Tusizungumze kwa kufoka au kupaza sauti kiasi cha kuwakera wasikilizaji, pia tusizungumze kwa sauti ndogo na ya kunyanyapaa kiasi cha kuwafanya wasikilizaji wasisikie vizuri au kuelewa dhana halisi ya ujumbe uliokusudiwa kufikishwa. Mlinganiaji ujumbe, hanabudi kuifahamu vyema hadhira yake na kuifikishia ujumbe anaokusudia kwa heshima na kwa sauti ya wazi inayozingatia had hi ra.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MZEE WA KWANZA NA MBUZI WAKE.
Soma Zaidi...Wakati wa Wafuasi wa masahaba (Tabi'ina)101-200 A.
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...