Faida za kula uyoga

Faida za kula uyoga

Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya

Faida za kula uyoga

20. Uyoga (mushroom)
Uyoga pia ni katika vyakula vya asili, ijapokuwa upatikanaji wake umekuwa mchache siku hizi. Shukrani ziwaendee wataalamu wa kilimo, kwa sasa tunaweza kuzipata mbegu za uyoga kutoka maabara na kulima uyoga popote pale. Wataalamu wa mimea wanaamini kuwa uyoga si katika mimiea kwani uyoga upo katika kundi la viumbe liitwalo fungi (kingdom fungi). ila tunapozungumzia vyakula uyoga tunauweka kwenye kundi la mbogamboga. Uyoga una virutubisho vingi na vizuri kwa afya.

Kulinda mwili zidi ya cancer, Kama ilivyokuwa kwenye matunda na mboga zingine kuwa kuna antioxidant ambayo hii ni chembechembe inayopambana na sumu na kemikali ambazo zinaweza kuathiri seli za mwili wako. Basi kwenye uyoga pia kuna antioxidant kama iliyo karoti na matunda mengine tuloona hapo juu. Hii husaidia kwa kiwango kikubwa kupambana na kuuwa seli za kansa au saratani ambazo zinatengenezwa mwilini.

Mna kwenye uyoga madini yanayoitwa selenium, madini haya huwezi kuyapata kwenye matunda mngi sana na mbogamboga nyingi lakini haya utayapata kwa urahisi kwenye uyoga. Madini haya husaidia katika kuuwa seli sa saratani, pia kuzuia kuota kwa uvimbe unaosababishwa na saratani na aina zingine za vimbe.

Uyoga una vitamin D, ambavyo hivi pia husaidia katika kupambana na kuthibiti kukuwa kwa seli za saratani mwilini. Vitamin D husaidia katika utendaji mwema wa kazi za DNA. Itambulike kuwa saratani huanza kuathiri DNA ndio baadae huendelea kukuwa ndani ya mwili na baadae kuathiri sehemu za mwili. Hivyo uyoga una chembechembe hizi ambazo husaidia katika kupamba na nsa saratani.

Uyoga husaidia katika kuthibiti na kupamabana na kisukari hususan type 2 diabetes. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa ulaji wa vyakula vyenye kambakamba (fiber) husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Hivyo husaidia katika kuimarisha afya ya itengenezwaji wa insulin.

Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo, uwepo wa lkambakamba, madini ya potassium pamoja na vitamin C husaidia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha afya ya moyo (cardiovascular health). ulaji wa vyakula vyenye madini ya potassium kwa wingi pamoja na sodium kwa kiwango kidogo husaidia katika kupunguza shinikizo la damu hivyo husaidia kwa wale wenye presha ya kupanda ya damu.

Husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga mwilini (immune system). madini ya selenium yaliyomo kwenye uyoga kusaidia katika kushawishi na kustimulate mfumo wa afya mwilini katika kupambana na wadudu wavamizi. Madini haya husaidia katika kusahwishi T-cell au CD4 katika kupambana na wadudu wavamizi kama bakteria, virus na fangas. Beta-glucan inayopatikana kwenye ukuta wa seli za uyoga husaidia katika kuufanya mwili upambane vyema na wavamisi na kupamba nna na vijidudu vya maradhi.


                   

Bongoclass
Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 1556

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Hizi ndio kazi za madini mwilini mwako
Hizi ndio kazi za madini mwilini mwako

Post huu inakwenda kukupa orodha ya madini muhimu kwa ajili ya afya yako.

Soma Zaidi...
Faida za kula mayai
Faida za kula mayai

Posti hii inahusu zaidi faida anazozipata mtu anayekula mayai hasa wakati wa kifua kinywa, tunajua wazi kuwa mayai yana kiwango kikubwa cha protini pamoja na hayo kuna faida nyingi za kutumia mayai hasa wakati wa asubuhi kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Papai lililo  iva ni salama kwa mama mjamzito au halifai
Papai lililo iva ni salama kwa mama mjamzito au halifai

Papai ni moja kati ya matunda yenye vitamini C na virutubisho vinginevyo. Lakini papai pia ni moja kati ya vyakula ambavyo mjamzito anatakiwa awe makini navyo.

Soma Zaidi...
Zijue kazi za madini ya chuma mwilini
Zijue kazi za madini ya chuma mwilini

Posti hii inahusu zaidi kazi za madini ya chuma mwilini,Ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini na pia utokana na vyakula mbalimbali ambavyo upatikana kwenye wanyama na mimea. Zifuatazo ni kazi za madini ya chuma.

Soma Zaidi...
Faida za kula tango
Faida za kula tango

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za peaz/ peas
Faida za kiafya za peaz/ peas

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula peazi/peas

Soma Zaidi...
Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini
Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini

hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini

Soma Zaidi...
Fahamu tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari
Fahamu tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari

Post hii inahusu zaidi tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari ni tiba ambayo utumiwa sana na wagonjwa wa kisukari na walio wengi na wamefanikiwa kupona

Soma Zaidi...