FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA BAMIA (OKRA)

Makala hii inakwenda kukuonyesha faida za kula bamia kwa afya afya

FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA BAMIA (OKRA)

21. FAIDA ZA KIAFYA ZA KULA BAMIA (OKRA)


Bamia ni katika matunda ambayo ni mboga na karibia maeneo mengi mboga hii inapatikana. Bamia ni katika mboga muhimu sana kwani ina faida nyingi sana. Ndani ya bamia kuna vitamin, madini na kambakamba. Bamia hutumiwa kuanzia majani, mbegu, bamia lenyewe , maua, kikonyo na matawi. Kwa ufupi mbamia wote ni mboga na huliwa.



Ndani ya bamia kuna fiber (kambakamba), folate, vitamin K na madini. Bamia husaidia katika kuboresha na kuimarisha afya ya moyo pia hulinda mwili dhini ya saratani. Jitahidi ukinunua bamia lisikae zaidi ya siku tatu ama nne. Madini ya potassium na sodium hupatikana katika bamia bila ya kusahau vitamin A ambavyo hupatikana pia kwenye bamia.



Ndani ya bamia kuna aina ya protin inayoitwa lectin, ambayo pia huweza kupatikana kwenye maharage na nafaka nyingine. Wataalamu wa afya walitumia lectin inayozalishwa na bamia kwa ajili ya kutibu seli za saratani ya matiti (breast cancer). matokeo ya utafiti huu ulionesha kuwa seli za saratani zilipunguwa kwa asilimia 63 na zilikufa kwa asilimia 73. tafiti nyingi zinahitajika kufanywa kuhusu swala hili.



Pia ndani ya bamia kuna folate. Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa watu ambao hawapati kula fotate za kutosha wapo hatarini zaidi ya kupata saratani ya matiti, nyia ya uzazi, ini na aina zingine za saratani. Pia baadhi ya tafiti zilizofanya mwaka 2016 zainaonesha kuwa fotate inaweza kuzuia athari za saratani ya matiti.



Tafiti pia zinaonesha kuwa folate ambayo hupatikana kwenye bamia husaidia katika kuzuia matatizo wakati wa ujauzito. Tafiti zinaonesha mwanamke ambaye hana folate za kutosha anakuwa hatarini kupoteza ujauzito wake au mtoto akajapata matatizo ya kiafya baadaye. Fotate ni muhimu sana kwa mwanamke wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha.



Mwaka 2011 tafiti za kisayansi zilikuwa zikichunguza athari ya bamia kwa wenye kisukari. Wataalamu walitengeneza poda kutokana na maganda ya bamia na mbegu zake. Kisha wakatumia katika kutibu kisukari kwa panya kama majaribio. Panya huyu alikuwa na tatizo la sukari ya kushuka. Matokeo haya yakaleta athari chanya. Hivyo inashauriwa kwa wenye kisukari kutumia sana bamia.



Tafiti zilizofanya na AHA (American Heart Association) zimesema kuwa kula chakula chenye kambakamba (fiber) hupunguza athari hasi za cholesterol ndani ya damu. Vyakula hivi pia hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na stroke (kupalalaizi).



Tafiti zinaonesha kuwa vyakula vyenye vitamin K kwa wingi kama bania ni mujarabu sana katika kuimarisha afya ya mifupa. Vitamin hivi husaidia mifupa kufyonza madini ya calcium. Watu wenyekula vitamin K kwa wingi wana mifupa imara na isiyokuwa na mipasuko (hii ni nadharia tu).



Bamia husaidia katika kuzuia kupata tatizo la kukosa choo kwani kuna kambakamba ndani ya bamia, hizi husaidia katika mmeng’enyo wa chakula na kusafiri kwa chakula kutoka tumboni kuelekea maeneo mengine kwenye almentary canal. Bamia hupunguza hamu ya kula, hivyo husaidia katika kupunguza uzito.



Pia itambulike kuwa zipo athari hasi za kula bamia kwa kupitiliza. Kwa mfano bamia hupunguza hamu ya kula, pia bamia huweza kupelekea kujaa gesi tumboni na kujaza tumbo. Kula bamia nyingi zaidi huweza kupelekea kupata vijiwe ndani ya figo kwani bamia zina madini ya calcium kwa wingi.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 3268

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia, sababu zake na dalili zzake

Hapa utajifunza sababu za kupatwa na maumivu ya tumbo kwa chini upande wa kulia

Soma Zaidi...
Vyakula vya protini na kazi zake

Hapa utajifunza kuhusu kazi za protini mwilini na vyakula vipi vina protini kwa wingi

Soma Zaidi...
Vyakula vya wanga

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za vyakula vya wanga na umuhimu wake mwilini

Soma Zaidi...
Majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi

Posti hii inahusu zaidi kazi ya majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi, pamoja na kutibu saratani mbalimbali na upambana na fangasi na bakteria kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za spinachi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach

Soma Zaidi...
Faida za kula tikiti

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tikiti

Soma Zaidi...
Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake

Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake

Soma Zaidi...
Vyakula vya vitamin A

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin A

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula biringanya (eggplant)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula biringanya eggplant)

Soma Zaidi...
Faida za nazi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nazi

Soma Zaidi...