Post hii inakwenda kukufundisha maana ya kusimamisha swala kama inavyotumika kisheria.
Maana ya Kusimamisha Swala
Kusimamisha swala ni tofauti na kuswali. Kuswali ni kufanya vitendo vya swala kama vile kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, n.k. Kusimamisha swala ni kuitekeleza swala kwa kuchunga na kutekeleza kwa ukamilifu yafuatayo:
(i)Sharti zote za swala.
(ii)Nguzo zote za swala.
(iii)Kuwa na khushui (unyenyekevu) wakati wote wa kutekeleza sharti na nguzo za swala.
Mtu akiswali bila ya kuzingatia na kutekeleza kwa ukamilifu mambo haya matatu, ataonekana kuwa kaswali, lakini atakuwa hajasimamisha swala na atastahiki kuadhibiwa vikali na Mola wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:
“Basi adhabu kali itawathibitikia wanaoswali, ambao wanapuuza swala zao (kwa kutozisimamisha), ambao hufanya ria ”. (107:4-6)
Kupuuza swala ni pamoja na kutotekeleza ipasavyo sharti za swala, nguzo za swala, na kutokuwa na unyenyekevu wakati wa kutekeleza sharti na nguzo za swala.
Hivyo, swala inayokubalika mbele ya Allah (s.w) ni ile iliyosimamishwa kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
“Hakika wamefuzu w aumini ambao katika swala zao ni wanyenyekevu ”. (23:1-2)
“Na ambao swala zao w anazihifadhi” . (23:9)
Kuhifadhi swala ni kutekeleza kwa ukamilifu sharti na nguzo zote za swala.
Umeionaje Makala hii.. ?
Mambo haya yanaweza kuharibu funga ya mtu ama kupunguza malipo ya funga.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi.
Soma Zaidi...Kuchunga au kutekeleza ahadi ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza nguzo kuu za swaumu. Kama hazitatimia nguzo hizi basi swaumu itakuwa ni batili.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha namna ya kutwaharisha Najisi.
Soma Zaidi...