Kusimamisha swala.
Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala.
6.3.Kusimamisha Swala.
- Maana ya Swala.
- Kilugha: Ombi au dua.
Kisheria: Ni maombi maalum kwa Allah (s.w) kwa kutekeleza nguzo na masharti maalumu kupitia mafundisho ya Mtume (s.a.w).
Maana ya Kuswali.
- Ni kufanya (kutekeleza) matendo ya swala kama vile; kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, kusoma dhikiri, n.k.
- Maana ya Kusimamisha Swala.
- Ni kuswali kwa kutekeleza kikamilifu nguzo na sharti zote za swala, kuwa na unyenyekevu (khushui) na kudumu nayo maishani.
Rejea Qur’an (107:4-5), (23:1-2), (23:9), (70:23) na (19:31).
- Sharti za Swala.
Ni mambo ya lazima kuchungwa na kutekelezwa na muislam kabla hajaanza kuswali
- Twahara.
- Sitara
- Kuchunga Wakati.
- Kuelekea Qibla.
- Twahara.
Maana ya Twahara
Kilugha: - Ni utakaso au
- Ni usafi wa nje unaohusiana mwili na nguo na wa ndani unaohusiana na nafsi
Kisheria: - Ni usafi wa roho, mwili na nguo.
- Ni kujitakasa kwa kujieepusha na kila aina ya najisi na hadath (uchafu).
Rejea Qur’an (2:222), (9:108)
- Mtu aliyetakasika ni yule aliyejitwaharisha na kila aina ya najisi na hadath katika mwili, nguo na nafsi kutokana na shirki, kibri, ukafiri, dharau, n.k.
- Najisi.
- Najisi maana yake ni uchafu.
- Baadhi ya vitu vilivyonajisi ni:
- Haja ndogo na kubwa ya binaadamu au mnyama.
- Damu
- Usaha
- Matapishi
- Pombe aina zote
- Mzoga wowote isipokuwa wa binaadamu, samaki na nzige na jamii yake.
- Maziwa ya mnyama asiyeliwa mfano: punda wa nyumbani, farasi, n.k.
- Kiungo cha mnyama kilichokatwa na hali yuko hai, mfano; mkia wa kondoo, n.k.
- Mbwa na nguruwe na kila kinachotokana nao.
- Cha kujitwaharishia.
Tunajitwaharisha kutokana na najisi na hadathi kwa kutumia;
- Maji safi - katika hali ya kawaida au
- Udongo safi - katika hali ya dharura.
- Maji safi.
- Ni yale yanayofaa kujitwaharishia.
Makundi ya maji safi.
1.Maji Mutlaq (maji ya asili)
- Ni maji yanayofaa kujitwaharishia yaliyo katika asili yake katika rangi, ladha na harufu. Mfano; maji ya kisima, chem chem, mito, maziwa, n.k.
2.Maji mengi.
- Ni maji yaliyokusanywa au yaliyokusanyika yenye ujazo wa kuanzia ndoo 12 au lita 240 au ‘Qulatain’
- Maji mengi hayaharibiki kwa kujitwarishia ndani au kuingiwa na najisi ila yakibadilika rangi, harufu au ladha yake.
3.Maji machache.
- Ni maji yenye ujazo chini ya ndoo 12 au lita 240 au ‘Qulatain’.
Mfano: maji ya vidimbwi, ndoo, mtungi, n.k.
- Maji haya huharibika na kutofaa kujitwaharishia iwapo;
- Yataingiwa na najisi ijapo kidogo sana
- Yalitumika kujitwaharishia najisi au hadathi ndani yake.
- Yametumika kufulia, kuoshea vyombo au kuogea ndani yake.
- Yataingiwa na kitu na kubadili asili yake katika rangi, ladha au harufu.
4.Maji makombo.
- Ni maji yaliyonyewa na binaadamu au mnyama (asiye najisi) na kubakishwa. Maji haya yanafaa kujitwaharishia pia.
5.Udongo Safi.
- Ni ule ulioepukana na najisi (uchafu) na uko katika asili yake usiochanganyikana na majivu, vumbi la mkaa au mbao, unga, n.k.
- Makundi ya najisi na namna ya kujitwaharisha.
Rejea Hadith EDK Kitabu cha 1, Sekondari, Uk. 69-72.
- Najisi kubwa.
- Ni najisi inayotokana na mbwa na nguruwe.
- Imeitwa hivyo kutokana na uzito wa kujitwaharisha kwayo.
- Namna ya kutwaharisha paliponajisika ni kuosha mara saba osho (kosho) mojawapo kwa kutumia mchanga (udongo) safi.
2.Najisi ndogo.
- Ni aina zote za najisi isipokuwa ya mbwa na nguruwe.
- Namna ya kujitwaharisha /kutwaharisha penye najisi ni kuosha kwa maji safi mpaka patakate kwa kuondoka harufu na rangi ya najisi.
3.Najisi hafifu.
- Ni mkojo wa mtoto mchanga wa kiume ambaye hajaanza kula chakula isipokuwa kunyonya maziwa ya mama tu.
- Imetwa hivyo kutokana na uhafifu wa kujitwaharisha kwayo.
- Namna ya kujitwaharisha ni kumwagia maji safi paliponajisika bila ya kusugua.
- Hadath
- Ni uchafu wa kihali (kinafsi) usiomruhusu mtu kuswali au kutufu Ka’abah.
- Makundi ya Hadath
- Hadath ndogo
- Hadath ya kati na kati
- Hadath kubwa
1.Hadath ndogo
- Ni hali ya kutokuwa na udhu.
- Hali hii huondoka kwa kutia udhu kamili kwa kuzingatia masharti na nguzo za udhu kama ifuatavyo;
- Masharti ya Udhu kabla ya kuanza kutawadha.
- Kuwa na maji safi na ya kutosha kuweza kutiririka kwenye viungo vya udhu na sio kupakazwa.
- Kutokuwa na kitu kilichogandamana na kinachozuia maji kupenya kwenye ngozi katika viungo vya udhu kama ulimbo, lami, rangi, n.k.
- Kutokuwa na vumbi au uchafu wowote unaoweza kubadili rangi na ladha ya maji unapotia udhu.
- Kuondoa kila aina yoyete ya najisi juu ya viungo vya udhu kabla ya kuanza kutawadha.
- Kutokuwa (kukata) kucha ndefu.
- Nguzo (faradh) za udhu.
- Kutia nia moyoni kuwa unatwadha.
- Kuosha uso kikamilifu.
- Kuosha mikono miwili mpaka vifundoni.
- Kupaka maji kichwani.
- Kuosha miguu miwili mpaka vifundoni (kongo mbili).
- Kufuata utaratibu huu (i – v) kwa mfuatano.
Rejea Qur’an (5:6).
- Sunnah za udhu.
- Kupiga mswaki kabla ya kuanza kutawadha.
- Kuanza kutawadha kwa kuosha viganja vya mikono kwa kusema “Bismillaah”
- Kusukutua na kupandisha maji puani.
- Kupaka maji shingoni wakati wa kupaka kichwani.
- Kuosha masikio mara tu baada ya kupuka maji kichwani.
- Kuosha kila kiungo cha udhu mara tatu.
- Kuanza kuosha viungo vya kulia kisha kushoto.
- Kuelekea Qibla na kuomba dua baada ya kutawadha.
Rejea EDK Kitabu cha 1, Sekondari, Uk. 73-74.
- Yaliyoharamishwa kwa asiye na udhu.
- Kuswali.
- Kutufu (kuizunguka) Ka’abah.
- Mambo yanayotengua (yanayoharibu) udhu bila hitilafu yeyote kati ya Waislamu.
- Kutokwa na kitu chochote katika utupu wa mbele au nyuma kama vile; upepo, maji maji, haja ndogo au kubwa, n.k.
- Kutokwa na fahamu kwa kulala au kusinzia bila kukaa kwa kumakinisha makalio ardhini.
- Kushika au kugusa sehemu za siri kwa kiganja cha mkono bila kizuizi chochote.
- Kugusana na mwanamke na kutokwa maji maji kwenye utupu kwa matamanio, vinginevyo udhu hautenguki.
2 .Hadathi ya kati na kati (Janaba).
- Ni hali ya mtu kupatwa na Janaba kwa kufanya tendo la jimai (tendo la ndoa) au kutokwa na manii kwa kuota au namna nyingineyo.
- Mambo yaliyoharamishwa kufanya kwa mwenye Janaba.
Rejea Qur’an (4:43) na (5:6)
- Kuswali.
- Kutufu Ka’abah
- Kukaa msikitini
- Kuisoma Qur’an hata kimoyo moyo.
Ibn Umar (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema:
“Wenye hedhi na wenye Janaba hawatasoma chochote kutoka kwenye Qur’an” (Tirmidh)
3.Hadathi Kubwa
- Ni hali ya kupatwa hedhi (damu ya mwezi) au nifasi (damu ya uzazi) kwa wanawake tu.
- Mambo yaliyoharamishwa kufanya kwa mwenye hedhi au nifasi.
- Kuswali au Kutufu Ka’abah
- Kukaa msikitini
- Kugusa au kubeba msahafu (ila kwa dharura sana)
- Kufunga
- Kufanya tendo la ndoa (jimai)
- Kutalikiwa (kupewa talaka)
- Kujitwaharisha kutokana na Janaba na hedhi au nifasi ni kuoga kwa maji safi kwa kutekeleza masharti na nguzo za kuoga josho la wajibu kama ifuatavyo;
- Masharti ya kuoga
- Masharti ya kuoga ni sawa na yale ya udhu.
- Nguzo za kuoga
- Nguzo za kuoga ni mbili;
- Kutia nia moyoni kuwa unaoga
- Kueneza maji mwili mzima.
- Kutayammamu
- Ni kitendo cha kujitwaharisha kwa kutumia mchanga au udongo safi.
- Dharura (sababu) za kuruhusiwa kutayammamu
- Ugonjwa usioruhusu kutumia maji.
- Kuwa safarini na kukosa maji.
- Kuwa katika mazingira ya kizuizi (yasiyorusu) kutumia maji.
- Kukosekana maji.
Rejea Qur’an (5:6)
- Masharti ya kutayammamu
- Ili tayammamu ikubalike lazima yazingatiwe masharti yafuatayo;
- Ipatikane dharura ya kutoruhusu kutumia maji katika kujitwaharisha.
- Pawe na hitajio la kutayammamu kama vile; kuswali, kutufu, n.k.
- Tayammamu ifanyike baada ya kutimia muda wa swala, kutufu, n.k.
- Pawepo na udongo safi, uliotwaharika, mkavu na wenye vumbi vumbi.
- Nguzo za Tayammamu
- Nia (kukusudia udongo safi)
- Kupaka uso
- Kupaka mikono
- Kufuata utaratibu huu (i-iii) kwa mfuatano
- Mambo yanayotengua udhu wa tayammamu
- Kufikwa na kila lenye kutengua udhu wa kawaida
- Kupatikana maji kabla ya kuswali au kutufu
2.Sitara
- Ni sharti la pili la kusimamisha swala ambalo muislamu anatakiwa azingatie kabla kuanza kuswali.
Rejea Qur’an (7:31) na (24:31)
- ​​​​​​​ Sitara ya mwanamume
- Uchi wa mwanamume ni sehemu baina ya kitovu na magoti kisheria.
- Katika hali ya kawaida muislamu anatakiwa kujisitiri na kujipamba kikamilifu wakati wa kuswali ila muda wa dharura tu.
- ​​​​​​​Sitara ya mwanamke.
- Mwili wote wa mwanamke ni uchi, hivyo stara yake ni kujifunika mwili mzima isipokuwa uso na viganja vya mikono muda wa swala na wakati wote.
- Sharti za sitara (vazi) la mwanamke na mwanamume wa kiislamu
- Vazi la mwanamke lazima lifunike mwili mzima isipokuwa uso na viganja vya mikono.
- Vazi lazima lisibane na kuweza kuonesha ramani (viungo) ya mwili wa mwanamke.
- Vazi lazima liwe zito kiasi cha kutoweza kuonesha rangi ya ngozi au umbo la mwanamke.
- Vazi la mwanamke lisiwe la kuvutia sana kuweza kusababisha ushawishi kwa wanaume.
- Vazi la mwanamke lisiwe la kifahari sana la kuleta majivuno, kibri, kujiona, n.k.
- Vazi la mwanamke wa kiislamu lisifanane na vazi la mwanamume.
3.Kuchunga wakati
- Hili ni sharti la tatu la kusimamisha swala.
- Ibada ya swala za faradh kwa waislamu ni imepangiwa wakati maalumu.
Rejea Qur’an (4:103), (2:187), n.k.
Rejea EDK Kitabu cha 1, Sekondari, Uk. 87-93.
- Swala za faradh ni tano;
- Adhuhuri – Ina rakaa 4, huingia baada ya kupinduka jua kuelekea magharibi.
- Alasir – Ina rakaa 4, huingia baada ya kuisha muda wa adhuhuri.
- Magh’rib – Ina rakaa 3, huanza mara baada ya kuzama jua.
- Ishaa – Ina rakaa 4, huanza baada ya kuingiza kiza halisi hadi alfajir.
- Alfajir – Ina rakaa 2, huanza mwisho wa usiku hadi kabla ya kuchomoza jua.
- Nyakati zilizoharamishwa kuswali
- Kuswali Sunnah baada ya swala ya Alfajir mpaka jua litakapochomoza.
- Wakati jua linachomoza.
- Wakati jua lipo katikati utosini
- Kuswali Sunnah baada ya swala ya Alasir
- Wakati wa kuzama jua
4.Kuelekea Qibla
- Hili ni sharti la nne la kusimamisha swala.
- Maana ya Qibla
Kilugha: Ni kukabili uelekeo au upande.
Kisheria: Ni uelekeo mahali ilipo nyumba tukufu ya Al-Ka’abah, Makkah - Saudia Arabia.
Rejea Qur’an (2:115), (2:149-150).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 web hosting 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Kujiepusha na ria na masimbulizi
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Misingi ya fiqh
Kwenye kipengele hichi tutajifinza vyanzo mbalimbali vya sheria ua kiislamu.
Soma Zaidi...