Ni nini maana ya twahara na kujitwaharisha?

Posti hii inakwendabkukujiulisha maana ya twahara na jinsi ya kujitwaharisha.

Maana ya Twahara:

“Twahara” ni neno la Kiarabu lenye maana ya usafi wa nje ulioambatana na usafi wa ndani ya mtu. Usafi wa nje unahusiana na usafi wa mwili na nguo na usafi wa ndani unahusiana na utakaso wa nafsi. Mwili na nguo hutwaharika kwa kusafisha kwa kufuata maelekezo

 

ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ama nafsi hutwaharika kwa kumtii Allah na Mtume wake kwa kufuata maamrisho yao na kuacha maovu na machafu waliyotukataza. Watu waliotwaharika kwa mtazamo huu hupendeza mbele ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:

 

“...Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa (wanaojitwaharisha)” (2:222)

 

“...Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wajitakasao”. (9:108)
Kwa ujumla tunaweza kusema twahara kwa mtazamo wa Qur-an ni usafi wa nguo zetu, miili yetu, hisia zetu, mawazo yetu na mwenendo na tabia zetu kwa mujibu wa maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

 


Pamoja na maana hii ya ujumla, Muislamu aliyetwaharika na kuwa tayari kusimama kwenye swala ni yule aliyeepukana na Najisi na Hadathi. Hivyo tunapojitwaharisha kwa ajili ya swala tunajishughulisha na kuondoa Najisi na Hadath.

 

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1474

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana: