Menu



Jinsi uislamu ulivyokomesha biashara ya utumwa wakati na baada ya mtume Muhammad (s.a.w)

 

Jinsi Uislamu Ulivyokomesha Biashara ya Utumwa wakati na baada ya Mtume Muhammad (s.a.w).

Uislamu baada ya kuenea na kuongoza sehemu mbali mbali, ilikuwa ndio mwanzo wa kukomesha biashara ya utumwa na kumkomboa mwanaadamu kiutu, (kiroho), kifikra na kisaikolojia kupitia njia na sera mbali mbali kama ifuatayo:

 

- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w).

 

-  Uislamu ulijenga uhusiano wa udugu na upendo baina ya watu bila kujali hadhi, nafasi, rangi, taifa la mtu.

 

- Uislamu ulisisitiza kuwa ubora wa mtu unatokana na ucha-Mungu wake na pia mtumwa au mtu huru anastahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo

Rejea Quran (49:13) na (4:25).

 

-  Utumwa katika Uislamu ulikuwa jambo la kupita na sio taasisi ya kudumu inayojenga matabaka ndani ya jamii.

 

- Uislamu uliweka mikakati ya kulinda haki, utu na hadhi ya watumwa kwa kuwafanyia wema na ihsani kama wanaadamu wengine.

Rejea Quran (4:36) na (49:13).

 

-   Watumwa walikuwa na haki ya kuamini na kufuata mila au dini waipendayo bila kushurutishwa.

Rejea Quran (2:256).

 

-   Watumwa walikuwa wanapata huduma za kijamii kama mavazi na malazi sawa na mabwana au wanaadamu wengine.

 

- Mtumwa alikuwa akikosea alisamehewa badala ya kuadhibiwa, Mtume (s.a.w) alisema mtumwa asamehewe hata mara sabini kwa siku.

 

-   Mtumwa alistahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo maadamu ni muislamu na Mcha-Mungu. Mtume (s.a.w) amesema msikilizeni na mtiini kiongozi hata akiwa ni mtumwa wa kutoka uhabeshi, maadam anafuata njia ya haki”

 

- Uislamu unalinda hadhi ya mtumwa kwa kutomuita Ewe mtumwa wangu badala yake anaitwa Ewe kijana wangu. 

 

- Watumwa walikuwa na haki ya kujikomboa na huru kwa njia mbali mbali zikiwemo:

Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote inayokubalika.

Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na maadui.

Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye manufaa kwa jamii ya   waislamu. 

Rejea Quran (47:4).

-  Mtume (s.a.w) na Maswahaba waliwaachia watumwa huru na kuwakomboa wengine kisha kuwaacha huru kama ifuatavyo:

Mtume (s.a.w) mwenyewe aliwaacha huru watumwa 63.

Bi Aisha (r.a) mkewe Mtume (s.a.w) aliwaacha huru watumwa 67.

Ibn Abbas aliwaachia huru watumwa 70.

Abdallah bin Umar aliwaacha huru watumwa 1,000.

Abdul-Rahman bin Auf alinunua watumwa 30,000 na kuwaacha huru.

 

Mpaka kufikia mwisho wa uongozi wa Makhalifah wa nne Waongofu, suala la Utumwa lilibakia kuwa historia katika ulimwengu wa Kiislamu.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 1242

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Hijja na umrah

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Maana ya shahada

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Taratibu za kutaliki katika uislamu.

Hapa utajifunza taratibu zinazofuatwa wakati wa kukusudia kumuacha mke. Pia utajifunza sababu za kiwepo kwa eda baada ya kuachwa mwanamke.

Soma Zaidi...
Mafungu ya mirathi katika uislamu

Mafungu ya urithi yaliyotajwa katika haya sita yafutayo:1.

Soma Zaidi...
NAMNA YA KUCHINJA KATIKA UISLAMU

عَنْ أَبِي يَعْلَى شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "إنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِح...

Soma Zaidi...
Jinsi ya kutawadha kama aalivyotawadha Mtume Muhammad (s.a.w)

Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume

Soma Zaidi...