Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata Maambukizi kwenye mifupa,
Walio katika hatari ya kupata Maambukizi kwenye mifupa.
1. Waliopata ajali na kushambuliwa kwa mifupa.
Hawa waliopatwa na ajali na mifupa ikishambuliwa wapo kwenye hatari ya kupatwa na ugonjwa huu wa Maambukizi kwenye mifupa, kwa sababu wadudu au bakteria wakishaingia kwenye mifupa na wakakuta tayari kuna udhaifu fulani na pengine mgonjwa hakutibiwa vizuri ipasavyo hali ya kuwepo kwa Maambukizi inakuwepo kwa kiasi kikubwa , kwa hiyo mtu aliyepata ajali anapaswa kutibiwa vizuri na kujilinda mda wote hasipatwe na magonjwa yoyote.
2. Kuwepo kwa vyuma kwenye mfupa au kitu chochote ambacho kimo na hakipaswi kuwepo kwenye mifupa kwa kitaalamu tunaweza kusema foreign body, kwa Sababu vitu hivi sio mahali pake vilipo pengine vimekuwepo ili kusaidia kazi mbalimbali kwenye mwili kwa sababu ya udhaifu, kwa hiyo watu wenye vitu kama hivi wana asilimia kubwa kupatwa na Maambukizi kwenye mifupa kwa hiyo wanapaswa kuwa makini ili kuepuka na maambuy kwenye mifupa .
3. Kushuka kwa kinga ya mwili.
Tunajua wazi kuwa kinga ya mwili ikishuka usababisha magonjwa mengi kuwepo kwa hiyo watu wale ambao kinga zao za mwili zimeshuka wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha wanajikinga na ugonjwa huu wa Maambukizi kwenye mifupa, kwa hiyo wale walio na magonjwa yanayopunguza kinga ya mwili kama vile HIV na mengineyo wahakikishe kuwa wanatumia dawa ili kuweza kuweka kinga yao sawa na kuepuka ugonjwa huu wa Maambukizi kwenye mifupa.
4. Wenye umri mkubwa nao wana hatari ya kupata ugonjwa wa Maambukizi kwenye mifupa.
Tunajua kubwa umri ukiongezeka na baadhi ya viungo vinapungua kufanya kazi kwa hiyo wale wenye umri mkubwa ute ute uisha kwenye mifupa na baadhi yao mifupa uanza kuuma kwa hiyo kiasi cha kushambuliwa na bakteria inakuwa kubwa, kwa hiyo wenye umri mkubwa wanapaswa kula vyakula vya kuongeza ute ute kwenye mifupa na kula vyakula vya kuongeza kinga mwilini.
5. Kwa hiyo tukumbuke kwamba ugonjwa huu ukitibiwa mapema unatibika na pia tuwe na utaratibu wa kwenda hospitali mara baada ya kusikia mabadiliko kwenye mwili na tunaweza kupunguza magonjwa mengine ambayo ni nyemelezi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowSomo hili linakwenda kukuletea njia za kujilinda na kujikinga na UTI
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha namna ya kujizuia,Mambo ya Hatari,na na Mambo yanayopelekea Ugonjwa wa ukosefu wa mkojo
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kutambua Dalili za macho makavu, kama tulivyotangulia kuona kubwa macho kuwa makavu Usababishwa na sehemu ya kuzalisha maji kwenye jicho kushindwa kufanya kazi na jicho hilo huwa kavu na Dalili zake ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...postii hii inshusiana na dalili na matatizo ya pepopunda. Pepopunda ni ugonjwa hatari wa kutishia maisha unaosababishwa na sumu ya tetanospasmin inayozalishwa katika majeraha yaliyoambukizwa na kizuizi cha bacillus clostridia. Bakteria ya pepopunda hu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo,ni njia ambazo mtu anaweza kutumia Ili kuzuia uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.zifuatazo ni njia zinazoweza kutumika kama mtu amepata uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna ya kumsaidia mgonjwa aliyepungukiwa na damu kwa sababu ya minyoo.
Soma Zaidi...