Makundi yaliyo katika hatari ya kupata Ugonjwa wa ngiri.


image


Posti hii inahusu zaidi makundi ambayo yapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa ngiri, ni hatari kwa sababu tunajua kuwa ngiri utokea kwa sababu ya kuta au tishu zinazoshikilia viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwepo kwa uwazi na kufanya viungo hivyo kutoshikilia vizuri katika sehemu inayostahili, kwa hiyo kwa sababu mbalimbali makundi yafuatayo yako kwenye hatari ya kupata tatizo hilo kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwapa huduma na uangalizi wa karibu kadri iwezekanavyo ili kuepuka Tatizo la kupata ngiri.


Makundi yenye hatari ya kupata ngiri.

1. Kundi la kwanza ni mama wajawazito.

Tunajua kuwa akina Mama wajawazito wako katika hatari kubwa kwa sababu tunajua kabisa mwili na viungo vya akina mama vinakuwa vimebeba mzigo ambao una uzito kwa kiwango fulani kwa hiyo ni rahisi kupata ngiri.

 

2. Kundi la pili ni wazee.

Tunajua kuwa mtu mzima au umri ukienda kila kitu kinapungua nguvu kwa hiyo ni rahisi na viungo vya mwili kukosa nguvu na hatimaye kupata tatizo la ngiri.

 

3. Wanaovuta Sana sigara.

Kwa sababu sigara zina tabia ya kudhoofisha mapafu kwa hiyo kwa hiyo baada ya mishipa kukosa nguvu inaweza kulegea na hatimaye ngiri inaweza kutokea.

 

4. Wagonjwa wenye uvimbe tumboni.

Pia na wenye uvimbe wako kwenye hatari ya kupata tatizo hili la ngiri kwa hiyo kama mtu akigundua kuwa ana uvimbe anapaswa kwenda hospitalini mara moja ili kufanyiwa matibabu kabla ya tatizo la ngiri halijatokea.

 

5. Watoto waliozaliwa na uzito mdogo au wale waliozaliwa kabla ya wakati, tunajua wazi kwamba watoto wa namna hiyo kinga yao ni ndogo kwa hiyo ni rahisi sana kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara.

 

6.kwa hiyo haya makundi yanapaswa kulindwa sana ili kuweza kuepuka tatizo la ngiri na kuwapatia huduma muhimu ambazo zitaweza kuwasaidia kuepukana na hali hii ya tatizo la ngiri kwa watoto na akundi ambayo yako kwenye hatari ya kupata tatizo hili.

 

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    2 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    3 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani offline    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Njia za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha.
Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini vinavyohitajika kwa sababu dawa hizo uingiliana na uzalishaji wa maziwa. Soma Zaidi...

image Mabadiliko ya uzito kwa mjamzito
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya uzito kwa mjamzito, hii ni hali ya kubadilika kwa uzito kwa Mama akiwa na Mimba Soma Zaidi...

image Fikra potofu kuhusu vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya fikra potofu kuhusu vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

image Faida za kusafisha vidonda.
Posti hii inahusu zaidi faida za kusafisha vidonda, ni faida ambazo Mgonjwa mwenye vidonge uzipata kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Zijue sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji
Post hii inahusu zaidi sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji kina sehemu kuu nne na sehemu hizo ufanya kazi tofauti tofauti kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Namna ya kumwosha Mgonjwa vidonda
Posti hii inahusu zaidi njia za kutumia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda, ni njia muhimu ambazo ni lazima kuzipitia unapotaka kumwosha Mgonjwa vidonda. Soma Zaidi...

image Dalili za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

image Magonjwa madogo madogo kwa Mama wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi magonjwa madogo madogo kwa akina Mama wajawazito, ni magonjwa ambayo hayawezi kupelekea kupoteza maisha kwa Mama mjamzito, magonjwa haya upotea ikiwa Mama atajifungua. Soma Zaidi...

image Dalili za kisukari aina ya type 2
Kisukari cha Aina ya 2, ambacho wakati mmoja kilijulikana kama Kisukari cha watu wazima au kisichotegemea insulini, ni ugonjwa sugu unaoathiri jinsi mwili wako unavyobadilisha sukari (glucose), chanzo muhimu cha nishati ya mwili wako. Soma Zaidi...

image Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa walioingiliwa na uchafu puani.(foreign body).
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa alieye ingiwa na uchafu puani (foreign body) Soma Zaidi...