Sababu za Maambukizi kwenye mifupa.
Post hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ni Maambukizi ambayo hutokea kwenye mifupa kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha ugonjwa huu.
Sababu za Maambukizi kwenye mifupa.
Kwanza kabisa Maambukizi kwenye mifupa yanaweza kuwa ya mda mfupi au pengine yanakuwa ya mda mrefu, Maambukizi haya ushambulia hasa sehemu za mikono, miguu na sehemu za kwenye kiuno ambapo mtu uhisi sana maumivu na pengine ikitokea mgonjwa akapatiwa matibabu mapema anaweza kupona na kuendelea kwenye hali yake ya kawaida, kwa hiyo iwapo mtu akasikia maumivu yasiyo ya kawaida kwenye mikono , miguu na kiuno anapaswa kuwaona wataalamu wa afya kwa matibabu zaidi.
1. Maambukizi haya usababishwa na bakteria, bakteria hao kwa kitaalamu huitwa staphylococcus Aureus na aina nyingine ya bakteria ambao nao kwa kitaalamu huitwa group B streptococcus, bakteria hao upitia sehemu mbalimbali za mwili na kuingia kwenye mifupa na kusababisha madhara makubwa. Kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi haya yanayosababishwa na bakteria dawa mbalimbali utumika kutibu maambukizi haya, Ili mradi mgonjwa anapaswa kuwahi hospitali ili kupata matibabu mapema.
2. Pia ugonjwa huu usababishwa na Maambukizi kutoka sehemu mbalimbali za mwili kama vile Maambukizi kwenye mfumo wa hewa, Maambukizi kwenye sehemu ya ndani ya sikio, tonsis ambazo ni kali kuoza kwa meno haya Maambukizi yakikaa mwilini na usababisha na mifupa kupata Maambukizi kwa sababu bakteria hao waliopo kwenye sehemu nyingine za mwili wanaweza pia kusambaza na kushambulia mifupa na kusababisha ugonjwa huu. Kwa hiyo tunapaswa kutibu Maambukizi yoyote kwenye mwili ili kuepuka kuwepo kwa madhara mengine.
Kuwepo kwa aina yeyote ya uwazi kwenye mifupa.kitendo cha kuwepo kwa uwazi wowote kwenye mifupa usababisha Maambukizi kwenye mifupa, kwa mfano kuwepo kwa kidonda kilicho wazi, kuvunjika ambapo wadudu wanaweza kupita na kuharibu mfupa
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Watu walio hatarini kupata UTI
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya makunfi ya watu walio hatarini kupata UTI
Soma Zaidi...Njia za Kuongeza Mbegu za Kiume
​Uzazi wa mwanaume unategemea kwa kiasi kikubwa ubora na wingi wa mbegu za kiume. Makala haya yanalenga kutoa mwongozo wa njia za asili na mabadiliko ya mtindo wa maisha yanayoweza kusaidia kuongeza uzalishaji na kuboresha ubora wa mbegu hizo.
Soma Zaidi...Dalili za mtoto Mwenye UTI
Posti hii inahusu zaidi dalili za mtoto Mwenye UTI,ni dalili ambazo uwapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa macho mekundu (Conjunctivitis): Jinsi ya kujikinga.
Ugonjwa wa macho mekundu, kitaalamu Conjunctivitis (au Pink eye), ni uvimbe wa utando mwororo unaofunika sehemu nyeupe ya jicho na ndani ya kope. Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na virusi, bakteria, au mzio (allergy). Kwa kuwa ni rahisi sana kuambukiza, elimu kuhusu usafi wa kibinafsi na mbinu za kuzuia usambazaji ndizo nguzo kuu ya kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huu ndani ya jamii.
Soma Zaidi...Dalili kwa mtu anayeharisha
Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuharisha, kuharisha ni kitendo Cha kupitia kinyesi chenye maji inawezekana kina damu au kisichokuwa na damu.
Soma Zaidi...