Dalili za Maambukizi kwenye mifupa

Dalili za Maambukizi kwenye mifupa

Posti hii inahusu zaidi dalili za Maambukizi kwenye mifupa, ni dalili ambazo ukionyesha kwa mtu mwenye Maambukizi kwenye mifupa.

Dalili za Maambukizi kwenye mifupa

1. Maumivu makali wakati wa kutembea.

Ni maumivu ambayo utokea kwa mtu ambaye ana Maambukizi kwenye mifupa, hali hii ya maumivu utokea kwa sababu bakteria wanakuwepo kwenye mifupa usababisha mashambulizi ambayo umfanya mtu kuumia pale anapotembea au pengine bakteria usababisha ute ute ambao upo kwenye mifupa kukauka kabisa na pengine mifupa kusagika na hivyo mtu akiwa anatembea uhisi maumivu makali. Kwa hiyo tunashauriwa kutumia dawa za maumivu ili kupunguza maumivu yanayojitokeza.

 

2. Pengine mgonjwa anaweza kuwa na homa.

Tunajua wazi kuwa kama kuna Maambukizi yoyote kwenye mwili usababisha homa ya mtu kupanda au kushuka kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi ya aina hii homa ya mwili upanda. Kwa hiyo mgonjwa anapotumia dawa za kutibu maambukizi anapaswa pia kutumia dawa za kushusha homa ili kuepuka matatizo mengine hasa kwa watoto kama vile degedege na kuishiwa damu kwa sababu ya joto la mwili kupanda.kwa hiyo tunapaswa kuwa makini kwenye ugonjwa huu wa Maambukizi kwenye mifupa.

 

3. Kushindwa kutembea kwa Mgonjwa.

Pengine kama Maambukizi yamekuwa makali mgonjwa ushindwa kutembea na pengine kuwa mlemavu kabisa, hali hii usababishwa na Maambukizi kwa sababu bakteria uharibifu mifupa na mifupa ushindwa kufanya kazi yake ya kila siku na baada mgonjwa hushindwa kutembea kabisa.kwa hiyo tunapaswa kutumia dawa mbalimbali za mifupa ili ziweze kusaidia kupunguza matatizo yanayoweza kujitokeza.

 

4.kuchechemea wakati wa kutembea.

Pengine mgonjwa mwenye tatizo la Maambukizi kwenye mifupa mara nyingi uonekane anachechemea wakati wa kutembea kwa sababu pengine ya maumivu anayekuwa nayo au wakati mwingine mgonjwa ubadilisha mwondoko na kutembea kusiko kwa kawaida na hali hii usababishwa na maumivu kwa sababu mgonjwa anatafuta jinsi ya kutembea inayofanya kupoteza maumivu.

 

5 . Kwa upande wa watoto utaona wanalia tu iwapo ukimshika sehemu yenye Maambukizi kwa sababu ya kuwepo kwa maumivu, kwa hiyo kwa upande wa watoto hasa wale ambao hawaongei tunapaswa kuwasikiliza ni wapi wanaumia ili tuweze kuwasaidia na kutibu mapema kwa sababu ugonjwa huu usipotibiwa mapema unaweza kusababisha madhara makubwa zaidi.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 2629

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰4 ai web app     πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

KUJIANDAA KWA AJILI YA KUMUONA DAKTARI

KUJIANDAA KWA AJILI YA KUMUONA DAKTARI Fanya miadi na daktari wako wa kawaida ikiwa una ishara au dalili zinazokupa wasiwasi.

Soma Zaidi...
Faida za kufanya mazoezi kila siku

​Katika somo hili, tunaangazia jinsi mazoezi ya kila siku yanavyochangia katika kuimarisha mfumo wa moyo, kudhibiti uzito, kuboresha afya ya akili, na kuongeza nguvu ya mwili. Tunaeleza faida hizi kulingana na ushahidi wa kisayansi na kutoa mwongozo mfupi wa jinsi ya kuanza mazoezi ili kupata matokeo bora

Soma Zaidi...
Ninashida Kuna mtu anaumwa pressure Kila anap pima Iko juu il mwil aumuumi at kidg n dawa anatumia unawez kunisaidiaj

Kama unasumbuliwa na presha post hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakuoatia ushauri kutokana na swali alilouliza mdau wetu.

Soma Zaidi...
Homa za mara kwa mara: Chanzo chake na nini cha kufanya.

Homa sio ugonjwa; ni silaha ya mwili wako. Inapopanda, inamaanisha mfumo wako wa kinga unawaka moto kupambana na adui aliyepo ndani. Lakini, je, inakuwaje unapopata homa hizo mara kwa mara? Homa za mara kwa mara ni kengele ya onyo kwamba kuna kitu hakiko sawa ambacho hakijatibiwa kikamilifu. Makala haya yanakusaidia kutambua nini cha kufanya ili kuondokana na mzunguko huu wa maumivu

Soma Zaidi...
Matatizo ya tezi ya shingo (Thyroid disorders): Dalili zake.

Tezi ya shingo (Thyroid gland) ni kiungo kidogo chenye umbo la kipepeo kilichopo sehemu ya mbele ya shingo. Ingawa ni ndogo, ina kazi kubwa sana ya kuzalisha homoni zinazodhibiti kila kitu kuanzia kasi ya mapigo ya moyo, joto la mwili, hadi namna tunavyochoma kalori. Matatizo ya tezi hutokea pale tezi hii inapozalisha homoni nyingi sana (Hyperthyroidism) au kidogo sana (Hypothyroidism). Makala haya yanachambua dalili za hali hizi mbili ili kukusaidia kuelewa ishara za mwili wako.

Soma Zaidi...
MALARIA NI NINI? NI WATU WANGAPI WANAKUFA KWA MALARIA DUNIANI

Malaria ni katika maradhi yanayosumbua sana na kusababisha maradhi ya watu wengi sana duniani.

Soma Zaidi...