Vyumba vidogo vidogo kwenye chumba cha upasuaji
Post hii inahusu zaidi juu ya vyumba vidogo vidogo ambavyo Vimo kwenye chumba cha upasuaji, ingawa chumba cha upasuaji ni kimoja ila kuna vyumba vingine vidogo ambavyo vinatumika kwa kazi mbalimbali kama tutakavyoona.
Vyumba vidogo vidogo kwenye chumba cha upasuaji.
1.chumba cha mapokezi na kuruhusu mgonjwa kutoka kwenye upasuaji.
Hiki ni mojawapo ya vyumba vidogo ambavyo Vimo kwenye chumba cha upasuaji katika chumba hiki mgonjwa upokelewa na kuangalia kama ana sifa za kuingia kwenye upasuaji na vile vile kwenye chumba hiki mgonjwa akimaliza kufanyiwa upasuaji upitia hapa ili kuhakikisha kuwa kama mgonjwa yu hai au ana tatizo lolote lililompata kama mgonjwa yuko vizuri huweza kupelekwa kwenye chumba muhimu kwa ajili ya kupona.
2.Chumba cha mtoa dawa ya usingizi,
Hiki ni chumba maalum ambako mtoa huduma ya usingizi ukutana na mgonjwa na kumuuliza pamoja na kujadiliana kuhusu dawa ya usingizi anayotaka kupewa kama ni ya mwili mzima au niya nusu kwa hiyo Mgonjwa uweza kuchagua, pamoja na uchaguzi wa mgonjwa na mtoa huduma hii anapaswa kumshauri kulingana na hali halisi ya mgonjwa.
3.Chumba cha kupumzika Mgonjwa baada ya upasuaji.
Hiki ni chumba ambacho mgonjwa anapumzika baada ya upasuaji katika chumba hiki mgonjwa uangaliwa zaidi na kupewa huduma zote mpaka pale atakapopona na kurudia kwenye hali yake ya kawaida kwenye chumba hiki panapaswa kuwepo na gasi ya oxygen, maji ya kutosha kwa ajili ya mgonjwa mgonjwa anapaswa kuwa makini ili kuepuka matatizo baada ya upasuaji kama vile kuishiwa damu na mengine kama hayo.
4.Chumba maalum cha kusafishia vifaa.
Hiki ni chumba ambacho vifaa vyote vinavyotumika wakati wa upasuaji vinasafishiwa kwa hiyo chumba hiki kinapaswa kuwepo kwa maji safi ya sabuni, maji yenye chlorine, maji ya kusuuzia na baada ya kutoa uchafu huu vinapaswa kupelekwa ili kuingizwa na kuua bakteria wote na mtu anayefanya kazi kwenye chumba hiki anapaswa kuwa na Elimu ya kutosha na awe amesomea kazi hiyo kwa kufanya hivyo wadudu wote wataweza kufa na kuzuiliwa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
5. Chumba cha kubadilishia nguo.
Tukumbuke kuwa kabla ya kuanza upasuaji ni lazima kubadilisha nguo za nyumbani na kuvaa nguo za upasuaji hii ufanyika ili kuzuia kusambaa kwa bakteria kutoka kwa mhudumu kwenda kwa mgonjwa kwa hiyo ndo maana kuna chumba maalum kwa ajili ya kubadilisha nguo
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 web hosting 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Jinsi ya kuhesabu siku za hatari za kupata mimba.
Kujua siku zako za hatari (siku ambazo una uwezekano mkubwa wa kupata mimba) ni njia muhimu sana kwa wanandoa wanaopanga kupata mtoto. Siku hizi hutegemea mchakato wa kupevuka kwa yai (ovulation), ambapo yai huachiliwa kutoka kwenye ovari ili kurutubishwa. Makala hii inaelezea mbinu rahisi ya kalenda unayoweza kutumia.
Soma Zaidi...Zijue sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji
Post hii inahusu zaidi sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji kina sehemu kuu nne na sehemu hizo ufanya kazi tofauti tofauti kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Vipi kinyesi cha haja kubwa kinaelezea afya ya mtu
Katika somo hili tutajifunza ni Kwa namna gani afya Yako inaweza kuelezewa kupitia kinyesi
Soma Zaidi...Dua Sehemu ya 01
Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
Soma Zaidi...