Zijue sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji
Post hii inahusu zaidi sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji kina sehemu kuu nne na sehemu hizo ufanya kazi tofauti tofauti kama ifuatavyo.
Sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji.
1.sehemu ya kwanza ni sehemu ambayo kila mtu anaweza kuingia kwa kitaalamu huitwa unrestricted zone, hiii sehemu hata ndugu wa mgonjwa wanaweza kukaa na kusubiria mgonjwa wao na nguo za nyumbani uweza kutumika katika sehemu hii na watu hawakatazwi kuingia kwenye sehemu huu kwa ujumla huitwa sehemu ambayo haijafanyiwa usafi unaopaswa kitaalamu.
2.Sehemu ya pili ni sehemu ambapo wahudumu wa afya wanaohusika na upasuaji ubadilisha mavazi yao na kuvaa mavazi rasmi ya kwa ajili ya kazi ya upasuaji kwa hiyo watu wengine hawapaswi kufika sehemu hii sehemu hii huwa karibu sana na uelekea sehemu ya upasuaji kwa hiyo hii sehemu imetengwa na watu hawapaswi kuingia kwa sababu ya kuweza kuingiza wadudu kwenye chumba cha upasuaji na kusababisha madhara mengine ambayo hayakutarajiwa.
3.Sehemu inayofuata ni sehemu ya chumba cha upasuaji chenyewe, katika chumba hiki wahudumu wa afya ndio wanapaswa kuingia na wakiwa wamevaa mavazi rasmi na pia mgonjwa mwenyewe anakuwa na mavazi rasmi na vyombo vyote vya kwenye chumba hiki huwa kwenye hali ya usafi, hiki chumba kinatengewa kwa sababu ya kuzuia wadudu na uchafu mwingine kuingia kwa mgonjwa na kusababisha madhara yasiyotarajiwa kwa mgonjwa.
4.Chumba kingine na cha mwisho ni chumba cha kuhifadhia uchafu , sehemu hii huwa na ndoo tatu na box moja kwa ajili ya kuhifadhia uchafu mbalimbali ndoo ya kwanza huwa na uchafu wa karatasi za kawaida ambayo ina rangi ya kijani, ndoo ya pili ina rangi ya njano ambayo ina uchafu wenye maji maji na ndoo ya tatu ni nyekundu yenye uchafu uliochanganyika na damu na box linakuwa na takataka zenye ncha kali kama vile sindano.
5.Tunapaswa kujua sehemu hizo nne za chumba cha upasuaji ili kuepuka kuingilia chumba hiki endapo tuna wagonjwa na kujua kuwa wanafunzi wanaojifunza mambo ya afya wanapaswa kujua sehemu hizo ili kuepuka hali ya kuleta wadudu na vitu vingine kwa wagonjwa
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
AFYA YA UZAZI NI NINI?, PIA UTAJIFUNZA MATATIZO YA HEDHI, KUTOKUPATA UJAUZITO, ULEZI WA MIMBA NA MTOTO, TEZI DUME NA NGIRI MAJI, NGUVU ZA KIUME
AFYA YA UZAZI Afya ya uzazi huweza kufungamana na mambo mengi sana.
Soma Zaidi...Athari za ukosefu wa usingizi kwenye afya ya akili.
Usingizi mara nyingi huchukuliwa kama "kitu cha ziada" ambacho tunaweza kukipunguza ili tuwe na muda mwingi wa kufanya kazi au starehe. Hii ni hatari kubwa. Usingizi sio tu kupumzisha mwili, bali ni muda muhimu kwa ubongo kujisafisha na kurekebisha hisia. Makala haya yanaelezea jinsi ukosefu wa usingizi unavyoathiri moja kwa moja afya yako ya akili na jinsi mzunguko huu unavyoweza kuwa hatari.
Soma Zaidi...TAHADHARI KWENYE VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Msongo wa mawazo kazini na jinsi ya kuukabili.
Kazi ni sehemu muhimu ya maisha yetu, lakini inapogeuka kuwa chanzo cha hofu, uchovu, na kutoridhika, inakuwa hatari kwa afya yako. Msongo wa mawazo kazini (workplace stress) ni changamoto inayowapata wengi, kuanzia wafanyakazi wa ngazi za chini hadi viongozi. Makala haya yanakupa mbinu za kitaalamu za kutambua dalili za msongo na hatua za vitendo za kuurejesha usawa katika maisha yako ya kikazi.
Soma Zaidi...