Posti hii inahusu zaidi Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, tukumbuke kuwa mtu aliyefanyiwa upasuaji anakuwa kwenye riski sana ya kupata magonjwa na mambo mengine mbalimbali kwa hiyo kuna dalili zikijitokeza kwa mgonjwa aliyepasuliwa Zinapaswa kuf
Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji.
1. Kutokwa na damu sehemu iliyopasuliwa.
Hii ni mojawapo ya Dalili ya hatari kwa sababu kwa kawaida sehemu iliyopasuliwa haipaswi kutokwa na damu kama damu ikitoka ni lazima kuiripoti mara moja, wahudumu wa afya wanapaswa kuwa makini na kujaribu kuzuia damu isitoke na ikiendelea kutoka mgonjwa anapaswa kurudishwa kwenye chumba cha upasuaji na pia damu ikiendelea kutoka mgonjwa anapaswa kuwekewa damu nyingine. Kwa kufanya hivyo tunaweza kuzuia kuzimia kwa mgonjwa.
2. Kuzimia hii pia ni Dalili ya hatari kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji. Kuzimia utokana na kupungua kwa damu na maji mwilini, Dalili zake ni pamoja na kubadilika kwa rangi ya vidole na macho kuwa vya njano, presha kushuka, mgonjwa kutotulia , kwa hiyo Dalili za kuzimia inabidi kutambuliwa mapema ili kuweza kumsaidia mgonjwa kwa sababu kuzimia usababisha matatizo kwenye figo, ubongo na moyo.
3. Kupungua kwa kiwango cha gasi ya oxygen kwenye damu.hii pia ni Dalili mojawapo ambayo haifai kabisa kwa mgonjwa mwenye upasuaji, hali hii ikitokea mtungi wa hewa ni lazima uwekwe kwa mgonjwa na kuendelea kupima mara kwa mara, hali hii utokea kwa mbambali kwa mfano kusukuma vitu kwenye mfumo wa hewa wakati wa upasuaji, ulimi kuanguka nyuma na kuziba hewa kwa hiyo Mgonjwa anapaswa kuangaliwa na kutambua sababu za kukosa hewa.
4. Kuwepo kwa damu au majimaji yoyote kwenye mfumo wa hewa.
Hii pia ni Dalili ya hatari kwa mgonjwa aliyepasuliwa kwa sababu hali hii utokea kwa sababu mgonjwa ukalishwa kwenye mkao mbaya wakati wa upasuaji kwa hiyo maji maji yanaenda kwenye mfumo wa hewa kwa hiyo tunapaswa kumweka mgonjwa kwenye mkao mzuri na wa uhakika ili kuepuka kurudi kwa maji au damu kwenye mfumo wa hewa, kwa hiyo wataalamu wa afya wanapaswa kuepusha hali hii ili kuokoa maisha ya mgonjwa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu Mambo ya kiafya yanayozungumzwa na umoja wa mataifa
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji ni tofauti na vyumba vingine kwenye hospitali kwa hiyo vinahitaji uangalizi wa hali ya juu sana ili kuepuka aina yoyote ya uchafu kuwepo kwenye chumba hicho, zifuatazo ni na
Soma Zaidi...