Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula vyenye madini kwa wingi
VYAKULA VYENYE MADINI KWA WINGI
Kwa kuwa umesha jifunza kazi za madini zilizotajwa hapo juu, basi tambuwa kuwa kuna aina nyingi za madini ambazo baadhi yake zimetajwa hapo juu. Madini haya unaweza kuyapata kwenye mchanganyiko wa vyakula vingi. Lakini kuna vyakula ambavyo madini huwa ni mengi kuliko vyakula vingine. Hapa chini ninakuletea vyakula ambavyo vina madini kwa wingi ambavyo ni:-
1. Kwenye mbegu kama mbegu za maboga. Mbegu za maboga zina madini mengi sana. Unaweza kula mbegu za maboga kwa kutafuna, kutumia unga wake kama kiungo cha mboga ama kukaanga na kula kama bisi. Mbegu za maboga na m,begu nyingine zenye mfano wake kama mbegu za matango zina madini kama magnesium, zinc, manganese, copper, selenium, na madini ya phosphorus.
2. Kwenye samaki hasa samaki wenye magamba magumu kama kobe (shellfish) jamii ya tondo. Kama umeshawahi kula tondo, utakuwa unaelewa nini klimaamnishwa.kama hutambui nitakujuza. Angalia mfano wa konokono, basi samaki wenye kufanana na konokono wanatembea na majumba yao, ukimshituwa anaingia ndani. Samaki hawa ndio wanaozungumziwa hapa. Samaki hawa wana madini kama selenium, zinc, copper na chuma
3. Mboga za majani jamii ya kabichi. Mboga hizi zina madini kama magnesium, potassium, manganese na calcium
4. Kwenye nyama hasa nyama za viungo maalumu kama maini na figo. Nyama hizi zina madini kama selenium, zinc, madini ya chuma, na phosphorus.
5. Mayai ni moja kati ya vyakula vyema virutubisho vingi sana. Katika mayai kuna madini ya chuma kwa wingi sana, phosphorus, zinc na selenium.
6. Maharagwe, maharage ya na madini kama cailcium, magnesium, madini ya chuma, phosphorus,potassium, madini ya shaba na zinc.
7. Palachichi, tunda hili lina madini kama magnesium, potasium, manganese na madini ya shaba.
8. Maziwa yana madini kama cailcium, potassium, phosphorus, zinc na selenium.
9. Viazi mbatat vina madii kama potassium, magnesium, manganese, calcium, madini ya chuma na madini ya shaba.
10. Pia madini kama potassium, manganese, shamba na magnesium tunaweza kuyapata kwenye matunda kama, ndizi, fenesi, machungwa, pasheni, nanasi na mapera.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Homa ya dengue hupatikana sana Afrika, Asia na baadhi ya maeneo ya Caribbean.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kitunguu maji
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa faida kuu 5 za kula karanga mbichi katika afya ya mwili wako.
Soma Zaidi...zijuwe faida za kula njegere kiafya na umuhimu wa kula jegere pia jifunze njegere zina kazi gani mwilini?
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua
Soma Zaidi...