Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu orodha ya madini chanzo chake na faida zake
ORODHA YA MADINI NA CHANZO CHAKE NA FAIDA ZAKE.
Kwa ufupi ninakuletea orodha ya madini mablimbali na vyakula ambavyo hupatikana. Pia utajifunza kazi za kila aina ya dini ndani ya miili yetu.
1. Madini ya sodium (table salt) Madini haya unaweza kuyapata kwenye spinach, maharage,punje za maboga n.k.
2.Madini ya chuma. Haya hupatikana kwenye maini, nyama, maharage, na mboga za majani. Madini haya ni muhimu kwa utengenezwaji wa hemoglobin yaani chembechembe nyekundu za damu.
3.Madini ya kashiam(calcium). Haya hupatikana kwenye maziwa,maini, mboga za majani na cheese. Madini haya husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno, misuli na utengenezwaji wa neva. Husaidia piaa kuwezesha kuganda kwa damu kwenye majeraha. Husaidia katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa kuzifanya enzymes kuwa active.
4. Madini ya phosphorus, haya hupatikana kwenye nyama, maziwa, samaki, na mayai. Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.
5. Madini ya Potashiam (potassium) Hupatikana kwenye ndizi, machungwa,nyama na kaa. husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini.
6.Madini yakopa ( copper) Haya hupatikana kwenye nyama, samaki, na maini.husaidia katika mifupa na utengenezwaji wa hemoglobin (chembechembe nyekundu za damu).
7.Madini yamanganese Madini haya hupatikana kwenye figo,maini, chai na kahawa. Husaidia katika utengenezwaji wa mifupa, na katika mmeng'enyo wa chakula kwa kufanya enzymes ziwe active.
8.Madini ya iodine Madini haya hupatikana kwenye chumvi na vyakula vya baharini kama samaki. Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii itakupa elimu kuhusu mfumo wa mmrng'enyobwa chakula unavyo fanyankazi
Soma Zaidi...Mpaka sasa hakuna dawa ya kuponyesha saratani wala kinga ya saratani. Hata hivyo vipo vyakula ambavyo vinakadiriwa kuwa hupunguza hatari ya kuweza kupata saratani. Je unadhani uyoga ni moja ya vyakula hivyo?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu faida za kunywa maji kabla hujula kitu chochote,tunajua kabisa kabla ujala au kunywa chochote sumu nyingi mwilini zinakuwa hazijachanganyikana na chochote kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa kuna faida kubwa nyingi za kunywa maji kama ifuatavy
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukuonyesha faida za kula bamia kwa afya afya
Soma Zaidi...