Nabii Yunus(a.s) Amuomba Allah(s.w) Msamaha


Ndani ya tumbo la samaki, Nabii Yunus(a.s) akiwa hai na akili timamu aligundua kosa lake la kuwakimbia watu wake bila ya ruhusa kutoka kwa Mola wake. Ilibidi Yunus (a.s) alalame ndani ya tumbo la samaki kumuomba msamaha Mola wake na kuomba msaada wake.Na (Mtaje) Dhun-Nun (Yunusi) alipoondoka hali amechukiwa, na akadhani ya kwamba hatutatamdhikisha. Basi (alipozongwa)aliita katika giza (akasema):“Hakuna aabudiwaye isipokuwa Wewe Mtakatifu hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu (nafsi zao).” (21:87)Allah(s.w) alimsamehe mja wake Yunus(a.s) na kumuokoa katika janga lile kwa kumuelekeza samaki amrudishe pwani na kumtapika.“Basi tukampokelea (toba na dua yake) na tukamuokoa katika huzuni ile. Na namna hivyo ndivyo tuwaokoavyo walioamini.” (21:88)Lakini tukamtupa ufukoni (kwa kutapikwa na huyo samaki) hali ya kuwa mgonjwa.” (37:145)Baada ya kufikishwa pale pwani, Yunus (a.s) alikuwa mgonjwa na dhaifu asiyejiweza kwa lolote. Mola wake alizidi kumrehemu kwa kumuoteshea mti wa mbarikhi ambao aliula ukampa afya ya kumuwezesha kuwarudia watu wake ambao aliwakuta wameshaamini na wanamngojea kwa hamu ili awape mafunzo na maelekezo waweze kumuabudu Mola wao inavyostahiki:Na tukamuoteshea mmea wa mbarikhi (akawa anakula). (37:146) “Na tulimpeleka kwa (watu) laki moja au zaidi, (wale wale watu wake). Basi wakaamini na tukawastarehesha mpaka muda wao wa kufa.” (37:147-148)